Baada ya kupanda mafuta,nauli kwenda mikoani nazo zapanda. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya kupanda mafuta,nauli kwenda mikoani nazo zapanda.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gumzo, Sep 11, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HALI ya usafiri katika Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo (UBT), Jijini Dar es Salaam imekuwa tete baada ya shule kufunguliwa.Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi jana asubuhi katika kituo hicho, ulibaini nauli ya kwenda Morogoro ni Sh6,000 lakini jana ilikuwa Sh8,000 hadi 9,500.

  Nauli ya kwenda Moshi ni Sh20,000 lakini hivi sasa ni Sh25,000 hadi Sh35,000,Iringa ni Sh20,000 lakini imepanda hadi kufikia Sh25,000 hadi 35,000.
  Mikoa mingine iliyopanda ni Tanga ambapo bei yake halali ni Sh11,000 lakini hivi sasa imefika Sh15,000 ,Dodoma ni Sh15,000 hivi sasa ni Sh17,000 hadi Sh20,000.
  Hali hii ya usafiri kuwa adimu inatokana na likizo fupi ya wanafunzi kupisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza usiku wa kuamkia Agosti 26 na kuhitimishwa Septemba 8 mwaka huu.
  Mwananchi ilishuhudia umati wa watu wakiwa wakihangaika kutafuta usafiri bila ya mafanikio na wengine wakidiriki kurudi nyumbani kutokana na kukosa huduma hiyo.
  Jonh Mkenda aliyekuwa akisafiri kuelekea Moshi alisema hali hiyo imedhihirisha kuwa Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), ilivyoshindwa kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi.
  "Haiwezekani nauli zinapandishwa hivi, hata kama abiria ni wengi kwa nini Sumatra wasije kuweka kambi hapa ili kuweza kuwachukulia hatua wale wote wanaopandisha ovyo" alihoji Mkenda.
  Mkaguzi wa Sumatra,Mshuti Juma alisema hatua ya kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaopandisha nauli inawezekana lakini mpaka kuwepo na ushahidi.

  CHANZO: GUMZO LA JIJI
   
Loading...