Baada ya kuona status yangu nakunywa bia, amenipenda kwa kasi ya ajabu

Kajeba

JF-Expert Member
Oct 15, 2020
800
1,921
Habari wakuu

Hakika wanawake kuwaelewa ni ngumu mno, ni mwezi mmoja umepita tangu nilivyomuapproach mtoto mmoja hapa jiji la joto na akanitolea nje.

Nikapambana kila namna lakini mtoto hakunielewa ndani ya siku 4 nikajikatia tamaa. Ilibaki tunaonana kupitia status za wasap pasipo kucoment chochote

Wikiend hii nilijichanganya kiwanja nikatulia napiga zangu Serengeti lite..Tungi lilipozidi nilijikuta nimepost selfie niko na bia kama tano hivi.

Hapohapo yule mtoto alipoiview tu basi akili yake ikamruka...hee kumbe unakunywa bia? Nikajisemea tu napunguza mawazo..Hapo ndio akajiset na kuuliza lini niwe nae anipe kile nataka.

Hapa najiuliza hivi ni hizi bia tu ndio zimemfanya mtoto adate kiasi hiki, maana sio kwa sms na calls za fujo.

Hivi wanawake nini kinawapendeza? Mwanzo nilikuingia kiuchungaji ukazingua, kuona bia tu basi mambo yamekubali.

Wanawake mueleweke vipi lakini.

1622459904231.png

 
Mkuu umenikumbusha kitu. Kuna Binti mmoja mtaani kwetu alikuwa akisifika kwa uhuni, mitusi, ugomvi na ulevi hadi wazazi wake wakawa wamenyoosha mikono maana walimshindwa kwa tabia zake ameshalala sana Mahabusu na kutolewa.

Sasa kuna Jamaa alijitokeza kutaka kumuoa. Wazazi walikataa kupokea Mahari wakamruhusu jamaa achukue mke tu. (Wazazi waliona ni kama wametua mzigo na walijua huyu ataachwa tu siku si nyingi)

Cha ajabu hadi sasa ishapita miaka 10 yule binti bado yupo na mumewe na ana watoto wawili. Wote wawili mke na mume ni walevi wazuri sana.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom