Baada ya kuona Makala zangu niandikazo humu zinasambaa hovyo na wengine kujipa Umiliki, sasa nimezisajili COSOTA

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Ni ushauri tu kwa wale wanaopenda kupita humu na kudokoa makala za watu na kuzitupia kwenye blog zao au kwenye magrupu ya Whattsup.

Baada ya kuona makala zangu ninazoweka humu zinasambaa hovyo na wengine wakijidai ni wao ndiyo waandishi wa makala hizo hivi sasa nimesajili makala zangu zote katika taasisi ya haki miliki yaani COPYRIGHT SOCIETY OF TANZANIA (COSOTA).

Kwa hiyo muambizane na muwe makini kuna watu wana kesi ngumu mahakamani sijawahi kuona na kwa bahati nzuri taasisi hii imejaa wasomi wanasheria na siyo wababaishaji.

Mwenye masikio na asikie na mwenye kusoma asome na kuelewa huu ujumbe.

Mzee Mtambuzi.
 
Inamaana huzitaki pesa za wezi wa kazi zako hadi utoe taarifa kwa wezi kuacha kuiba, au huu ujumbe ni tisha toto? I don't get it!...
 
Nimefurahi sana kwa hii post mkuu. Watu wataheshimu articles kutoka JF coz wengi walipafanya kama SHAMBA LA BIBI aisee. Nilishaibiwa articles humu nikazikuta kwenye blogs nyingi tu mpaka wengine wakawa wanatumiana kwenye groups zao za whatsapp.

Ila niliskia kuwa chochote kinachoandikwa na kuwekwa hapa JamiiForums kinakuwa chini ya umiliki wa JF...?. Hili suala likoje lina ukweli ndani yake...?
 
ngoja waje wakuombe uweke vielelezo vya cosota ili waamini kama kweli upo serious
 
We mwenyewe mwizi wa makala!!!! Hakuna kipya chini ya jua,vyote vishaandikwa!!!
ubunifu ndiyo unatofautiana.
Mfano.
Ww ukipewa kazi ya kumuuelezea Melo na mwingine akapewa the same task lazima mtofautiane.
Kwahiyo ukichukua maelezo ya mwandishi A yakawa yako ni kosa kwahiyo inabidi utumie akili yako.
Kila kitu kipo, ubunifu ndiyo unaotofautiana.
Anzisha kiwanda cha kuzalisha soda za cocacola au jamii forum sasa tuone km ujanyea debe. Si hakuna kitu kipya chini ya jua.
Acha mawazo mgando.
Mtoa uzi nakuunga mkono 100%
 
Hivi ukiweka makala humu inakuwa mali yako, mali ya jamii media au ni free kwa mtu yoyote kutumi? Mamods mtueleze.
 
What ever we write here, we give as the gift to the World. Kinachotakiwa unapo copy cha mtu, basi unatakiwa umu acknowledge!
 
Back
Top Bottom