Tuna mengi sana ya kujifunza Kenya na uchaguzi wao.
1. Uwazi
2. Uhuru wa media zao
3. Incumbent president Uhuru hana kauli yoyote kuhusu uchaguzi
4. Katiba yao inaruhusu haya yanayotokea
5. etc etc etc
Summary nzuri ameifanya Askofu Bagonza kama ilivyo hapa chini!
UCHAGUZI MKUU KENYA
KUPIGA KURA Vs KUCHAGUA
Uchaguzi Mkuu wa Kenya unakaribia kukamilika ninapoandika uzi huu; Nimejifunza mengi:
1. Kenya wanapiga kura na kuchagua. Penginepo tunapiga kura, hatuchagui.
2. Kenya wana imani na mfumo wao wa uchaguzi. Penginepo hata wanaoshida wanashangaa wameshindaje.
3. Kenya mgombea akinadiwa na rais anayeondoka anakataliwa. Penginepo mgombea akinadiwa na anayeondoka anadeka.
4. Kenya wakifanya uchaguzi majirani tunakesha. Penginepo tukifanya uchaguzi majirani wanalala mapema maana matokeo wanayajua tayari.
5. Kenya kuna vurugu zinazoletwa na katiba nzuri. Penginepo kuna utulivu unaoletwa na katiba mbaya.
6. Kenya kuna ukabila unaongoza demokrasia. Penginepo kuna itikadi ya vyama zenye nguvu kuliko katiba.
7. Kenya katiba ina nguvu kuliko nchi. Penginepo kuna watu wana nguvu kuliko nchi. Hili ni tata sana.
8. Kenya wanachagua wezi kidemokrasia. Penginepo wezi wananyimwa kura na kuchaguana wenyewe.
9. Kenya wanachagua shetani anageuka kuwa malaika. Penginepo wanachagua malaika anageuka kuwa shetani.
10. Kenya unaweza kumshtaki mtu kabla hajatenda kosa. Penginepo hata aliyetenda kosa tayari unamuomba ruhusa kumshtaki.
KENYA IMESHINDA, WAGOMBEA WAMESHINDWA. PENGINEPO KWA MAJIRANI WANAOGOPA KUJARIBU SUMU KWA KUIONJA.
Hatutajua chochote iwapo hatutahoji na kudadisi