Baada ya kuoa Wanawake waliokuwa wananikataa wote wananitaka

Kajeba

JF-Expert Member
Oct 15, 2020
818
1,959
Habari wakuu,

Katika maisha sisi tunaotongoza hukubaliwa au kukataliwa hii haina ubishi, sasa nimeoa kwa ndoa ya kanisani kabisa lakini ajabu ni kwamba wale waliokuwa matawi na hawanitaki sasa wananitaka

Wakuu hivi hili suala kiutalamu nalihandle vipi au ndio niwamalize maana nikifikiria penzi lote lipo kwa ndoa changa hii

Hivi wanawake huwa mnawaza nini baada ya wanaume zenu kuoa halafu ninyi mnabaki mkidanga?
 
Habari wakuu
Katika maisha sisi tunaotongoza hukubaliwa au ku?
Waoe wote tu mkuu, sema usiwasogeze tu, ila pia siku ukichomwa moto na miongoni mwao ukabahatika kupona usisahau kuleta mrejesho ili iwe fundisho kwa wavulana wenzako.
 
Wanaume waliooa; Hawana wivu sana kwa michepuko, Sio ving'ang'anizi, hata anapogundua dem ana mahusiano na mwanaume mwingine anaweza asikupige wala kukuacha ndio sababu Wanawake wadangaji hupenda wanaume waliooa
 
inaitwa woman nature. huwa wanataka wasichoweza kukipata.

walipokuwa hawakutaki walikuwa wanakuona ni low value man. lakin sasa umeoa wanakuona ni high value man. so watafanya lolote wakupate.

Si wanawake wote wako hivi. hao ulionao ni malaya.. ni tamaa zao. wakwepe kabla hawajakuharibia ndoa
 
Nikianza kueleza sababu ya hiyo hali naweza sema ni 'Desire'au kwa kiswahili ni Hamu au Tamaa zao ndizo zinawapelekea kuwa hivyo.

Kiasili Tamaa au 'Desire' hutukumba wanaadamu wote, kama mtaalam mmoja alivyowahi sema; Tamaa namna ilivyo huchochewa na mambo makuu mawili...

a) Tamaa huchochewa na Uigaji (imitation)
Hapa wanaadamu hupenda au hutaka vitu kwa sababu tu tunaona watu wengine wanavitaka. Mathalani waweza kwenda mahali kupata chakula ukakuta migahawa miwili, Mmoja una watu wengi wanapata chakula ndani na mwingine hauna watu... Kikawaida akili hutuamuru kwenda kwenye ule wenye watu. Hii inatokana na imani yetu kuwa kwakuwa watu wengine wameupenda basi lazima utakua mzuri na huduma zitakuwa nzuri tu, nasi hujikuta tunatamani kuingia kupata huduma na kuukwepa ule mgahawa mtupu hata Kama wakati mwingine huu mtupu huwa na chakula bora zaidi.

b) Tamaa huchochewa na Ushindani.
Maisha ya mwanadamu yamejaa Ushindani kila mahali, toka kwenye familia watoto hushindana kupata makini au 'atensheni' ya wazazi, wafanyakazi hutafuta 'atensheni' ya mabosi maofisini n.k.
Asili yetu hii ya Ushindani ya KUTAKA KUCHUKUA VITU AMBAVYO WENGINE WANAVYO hutupa furaha na kutufanya kujisikia ufakhari pale tunapofanikiwa.

Hivyo, ktk kisa chako ni dhahiri hao akina dada wanakutaka kwa sababu wameona kuna mtu kakubali kuolewa nawe nao vichwani mwao wanaamini kuwa 'ni lazima huyu mtu atakua na kitu cha ziada mpk fulani kakubali kuolewa nae'
Na pia ktk fikra zao watakuwa wanaendeshwa na tamaa ya kumpokonya mwanamke mwenzao kitu alichonacho (mume) na kuchukua wao ili tu kujifakharisha.

Ndio asili yetu wanaadamu.

CHA KUFANYA:
Hii ni juu yako sasa, kwa maana ushajua wanachokitafuta na kinachowasukuma kukufuata...
Namna bora ya kuamua ni kuchanganua faida na hasara za maamuzi utakayoyachukua.

Kama utaamua kuwala au kulinda ndoa yako kikamilifu.

Kama unaithamini ndoa zaidi basi ni muhimu kuwaacha ila kama una shauku ya kujaribu vitu vipya basi hii ndio fursa adhim kabisa...ila jua huyu mwanamke uliyemuoa ndio karata yako ya dhahabu pindi utakapomuacha huo mvuto kwa hao WENGINE taratibu utapungua.

Kila la kheri.
 
Hicho ni kipimo cha utimilifu wa kiapo cha ndoa katika macho ya kiroho..........kushindwa mtihani huo ni hatua moja kuelekea kwenye uharibifu.......kuendelea kwa jambo hilo ni uelekeo wa maangamio kutokana na laana ya kiapo cha ndoa katika mizania ya kiimani......

NB
Kuchukua muda na kutafakari jambo hilo ndio njia mojawapo ya kuliendea jambo hilo...........
 
Back
Top Bottom