Baada ya kunikosa mimi sasa anamtaka dada yangu kimapenzi

Beauty Eva

Senior Member
Jul 22, 2016
131
374
Habari zenu ndugu! Ushauri wenu ni muhimu sana

Kuna mkaka mmoja mstaarabu sana kwa muonekano wake na hata katika mazungumzo yake. Kaka huyu tunatoka nae sehemu moja, ameoa na ana watoto. Shughuli zake anafanyia Arusha.

Mkaka huyu siku za nyuma baada ya kugundua nipo chuoni alikuwa anakuja kunitembelea na kuniletea zawadi ndogo ndogo kama vile ma-apple, chocolate, maziwa ya Azam etc . Nilikuwa nazipokea zawadi hizo kwa moyo mkunjufu maana nilikuwa namchukulia kama kaka yangu.

Siku moja akaniuliza walipo ndugu zangu hususan dada yangu tunaefuatana nae, nikamueleza kuwa dada yangu yupo hapa Arusha na nikampa namba za huyo dada yangu.

Siku zikapita, ukaka ukazidi na zawadi zikawa zinapokelewa. Nilikuja kushtuka siku alipoanza kunitumia msg ambazo zilikuwa zinaonesha kuwa ananivuta kimapenzi na haukupita Musa akaniletea zawadi ya underwears (night 👗 na pant). Baada ya hapo ndipo rasmi akaanza mchakato wa kunipata kimapenzi. Thanks to God kwamba, nilimkatalia na akanielewa japo kwa shingo upande. Tulikata mawasiliano kabisa

Baada ya mimi kumkatalia, kumbe akaanzisha harakati kumpata dada yangu. Binafsi nilikuwa sifahamu kuwa wanawasiliana, hadi juzi hapa ndipo nimebaini kuwa wana uhusiano wa karibu na muda si muda huenda wakamaliza kila kitu. Na nilibaini baada ya dada yangu kunieleza kuwa jamaa anamtaka na dada anasema, tayari moyo wake kwa kiasi kikubwa umetekwa na huyo kaka.

Sasa najiuliza, nimweleze dada kuwa huyo kaka hata mimi alinitaka nikamkataa au niwaache waendelee na hamsini zao?
 
Mmmh sio kwamba karoho kana kuuma
IMG_20181210_212844_711.jpeg
 
Duuh kumbe ana watoto jamaa??? sikusoma vizurii
Unamuachaje dada yako aendelee kuongopewa na huyo mume wa mtu?
Mi naona bora umwambie dada yako kilichopo alafu umuache afanye maamuzi ya kuendelea nae ama amuache
 
Aisee hata usijiulizee Huyo jamaa Kaoa na ana familiaa so atamchezea tu cster akoo labda Dada ako amdange tu ilaa Asidate nae maana Atavunja ndoa ya huyo kakaa.. Pia anaweza pigwa mimba akajutaa hata vihela alivyopokea...

MWAMBIE DADA AKO LEOOO...UKWELI WOTEE.. KAMA KUSUKA AU KUNYOA AAMUE YEYE..!
 
ACHANA NAO COZ SIO KILA UNAYETEMBEA NAE ATAKUA BIKRA (HANA MTU, MTOTO, MPENZI)
USIOYAJUA USIYAFUKUNYUE YATAKUUMIZA
 
Back
Top Bottom