Baada ya kunidhalilisha kwa maneno "wee mwanaume au mvulana kauka nikuvae utanipa nini.."miaka 16 iliyopita leo ananiona wa dhamani

KIUNGOMCHEZESHAJI

Senior Member
Oct 4, 2013
120
254
Linapokuja suala la mahusiano, wengi wetu tumeshawahi kutendwa, kusalitiwa, kupigwa kibuti, kuchunwa na kuachwa solemba na mengine yanayofanana na hayo. Katika kuishi kwangu, nimegundua hilo siyo tatizo kabisa, ni kawaida sana na ni sehemu ya maisha. Wengi wetu tunashindwa kuhimili msongo unaotokana na hali hiyo, wengine huvuka mipaka hata kwenda kumdhuru mtu, kuua au kujiua. Katika hali kama hiyo, ni vyema sana ukamwamini Mungu sana na ndo kipindi cha kumshikilia sana Mungu, hujui ni kitu gani Mungu amekuandalia mbeleni kwa ajili yako na huyo mtu wako.

Mwaka 2002, nikiwa najiunga na chuo kikuu mlimani nilipata kufahamiana na dada moja, kwa mwonekano wa nje alionyesha kunipenda sana kipindi hicho mimi hata sijawahi kulala na mwanamke, sijui mapenzi yana rangi gani wala shape nikaingia kichwa kichwa nakumbuka nililala nae mara moja tuu wiki iliyofuata rafiki zangu wakawa wananipa story, tukiwa pale Mabibo. day 1.. wananiambia wamemwona kuna jamaa kaja kumchukua na gari chuo..... Day 2... hivyo tena.. Day 3... Wamemwona disco na jamaa nikachoka. Wakati huo na ushamba wangu na ulokole wangu aaah, sijui club wala disco, alafu yeye nikionana naye anajifanya mlokole sana daaaah, roho iliniuma sana.

Ikafika siku nikamfanyia surprise nikakuta madudu ya kutisha kwenye simu yake baada ya hapo tuligombana sana. kilichoniuma alinitukana sana na kunidhalilisha sana kimsingi niligundua ni umaskini wangu ndo kisa cha kufanyiwa yote haya, na akatamka kabisa, "wee mwanaume au mvulana.... kauka nikuvae utanipa nini..". niliumia nililia, nikawa nashinda kusikiliza nyimbo za gospel kwaya.

Maisha yakasonga, tukamaliza chuo sikumtukana wala kumfanyia kitu mbaya nikapata kazi, naye akapata kazi Mungu si Athumani mimi nilipata kazi nzuri kuliko yeye baada ya hilo, nikaoa siku moja tukakutana tena chuoni UDSM 2008 nasoma masters. Daaah, akanishangaa sana, nimebadilika, nimependeza, na picha ya familia yangu na mtoto roho ikamuuma sana, tena alivyo mropokaji akatamka kabisa kujuta kunipoteza.

Hapo yeye bado hajaolewa. To make story short, alikuja kuolewa baadaye sana kwa kuchelewa, i think 2011 ndo aliolewa. ajabu ni kuwa mwaka huu 2018 amenikomalia sana kila wakati anataka tuonane, twende outings, nikajifanya mjinga kumkubalia akanipa wazo tupange chumba hapa Dar mimi na yeye tutakuwa tunakwenda kugegedana atakuwa anatoroka job, then jioni anarudi kwake.
Duuuh, kweli dunia tambara mbovu.
Over my dead body... Miaka 16 imepita tangu unitukane na kunidhalilisha, leo unaona mimi wa thamani siyo? umekuwa used and overused, leo unaniletea makapi kama siyo bwawa siyo? Wanawake kuweni na huruma basi.
 
Nyinyi si walokole bado? Kwa hiyo mnataka mkakumbushane mambo ya kale?
 
Nahisi ujumbe atakuwa ameupata maana naye yupo humu JF.

Ila sio vizuri kuja kumchana mbele ya kadamnasi mngemalizana kimya kimya tu.
 
Mbona sijaiona kisasi apa, haya ni maisha tu japo yanaenda kasi sana
 
Back
Top Bottom