Baada ya kumvua Uongozi Zitto...Mbowe, Dk. Slaa wapigwa Maruufuku kukanyaga Ardhi ya Mwanza...!!

Status
Not open for further replies.
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,097
Likes
389
Points
180
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,097 389 180

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa, wamepigwa marufuku kukanyaga jijini Mwanza.

Pamoja na onyo hilo, pia viongozi hao wametakiwa kufanya kila wanaloweza ili aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na wenzake waliovuliwa madaraka, warudishwe madarakani ndani ya siku nne kuanzia jana.

Kauli hizo zilitolewa jana na Mwenyekiti wa Vijana Kanda ya Magharibi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi ya CHADEMA, Mkoa wa Mwanza, Robert Gwanchele, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Gwanchele, yeye na wenzake wamelazimika kuchukua uamuzi huo kwa kuwa wanapinga kitendo cha kuvuliwa madaraka kwa viongozi hao kwa kuwa kilifanyika kinyume cha Katiba ya chama hicho.

“Pamoja na kuwapiga marufuku kukanyaga mkoani Mwanza viongozi hao wa kitaifa, kama Zitto, Dk. Mkumbo Kitila pamoja na Samson Mwigamba wasiporejeshwa madarakani, hadi Desemba 4 mwaka huu, vijana Kanda ya Magharibi tutaandaa maandamano yasiyo na ukomo kushinikiza Dk. Slaa na Mbowe wajiuzuru ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

“Chadema tumeingiliwa na mdudu aitwae ubinafsi kwani kuna baadhi ya viongozi wa chama ni makuwadi wa viongozi wetu wa ngazi za juu kufanya wanayotaka bila kuchukuliwa hatua.

“Chadema ni chama kinachojali watu wa upande fulani wa nchi, hivi viongozi kama Godbless Lema (Mbunge wa Arusha Mjini) pamoja na Kileo ambao waliamua kumshambulia Zitto kupitia mitandao ya kijamii wamechukuliwa hatua gani na chama?.

“Tutahakikisha tunawaondoa viongozi wote wa ngazi za juu kwa nguvu ya umma kwani Chadema sio mali ya mtu binafsi, chama hiki nicha wanachama.

“Hatutaki kuyumbishwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi, hao wanapaswa kukaa pembeni kwanza kupisha uchunguzi na kama hawataki kupisha nguvu ya umma itawaondoa na ndio maana sisi vijana wa Kanda ya Magharibi, tumeamua kuwapiga marufuku Mbowe na Dk. Slaa wasikanyage Mwanza kwani wao tayari wameamua kujijengea himaya yao isiyoguswa katika mikoa ya kaskazini, sasa Mwanza wanakuja kutafuta nini.

“Mbowe na Dk. Slaa ni watuhumiwa hawapaswi kuendelea kuwa viongozi wa Chadema, hao wanapaswa kujiondoa ili nao wachunguzwe juu ya matumizi mabaya ya fedha za chama,” alisema Gwanchele.

Pamoja na kuwashambulia Mbowe na Dk. Slaa, Gwanchele pia aliwarushia kombora wabunge wa Chadema wanaotoka Mkoa wa Mwanza kwa kile alichosema nao wameshiriki katika kuvuliwa madaraka kwa Zitto, Dk. Kitila na Mwigamba.

Kutokana na hali hiyo, alisema wabunge hao, Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiel Wenje (Nyamagana) na Salvatory Machemli (Ukerewe), wamepoteza uhalali wa kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Mwanza.

“Wabunge wa chadema Mkoa wa Mwanza hivi sasa wanajiona wako juu ya chama na wamekuwa wakitoa matamko ya kuunga mkono kuondolewa kwa Zitto na wenzake wakati sisi wananchi hatukuwatuma kufanya hayo.

“Kwa hiyo, nao wanapaswa kuondolewa madarakani mara moja kwa usaliti wao kwa wapiga kura wao,”alisema.
 
O

Oyono

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2013
Messages
222
Likes
5
Points
35
Age
26
O

Oyono

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2013
222 5 35
Acha wakome!, kwaio wataandamana wanamuandamania nani?, olewao watuletee msongamano ndo watalijua jiji!
 
Kibo10

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Messages
11,287
Likes
3,721
Points
280
Kibo10

Kibo10

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2013
11,287 3,721 280
Aache ujinga huyo dogo hii inshu ya cc ya cdm imewachanganya sana gambazzzzz
 
spencer

spencer

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
2,861
Likes
1,466
Points
280
spencer

spencer

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
2,861 1,466 280
Wewe dogo na wewe tembea kivyako.
Watu wa kanda ya ziwa tunafahamu misingi iliyokifanya chama hiki kiheshimike nje na ndani hadi kufikia mkakati wa kupandikiza hawa jamaa zako wa wanaonunulika kirahisi. Tembea hatujali Tembea hata msiage, wote vimeo mmeshajichanganya na jamaa yenu.

Hakuna lolote, tunamgojea atie maguu akione cha moto.:croc:
Anatuzingua hachukui posho kumbe ashajilipa NSSF/PPF zetu, tembeeni tu hatuwataki. ktk muda huu ni bora kubaki na msimamo wetu kama chama kuliko kujipaka oil chafu.

:nono:
 
Lokissa

Lokissa

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2010
Messages
7,216
Likes
297
Points
180
Lokissa

Lokissa

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2010
7,216 297 180
post zingine za kitoto
nani mwenye uwezo wa kuwapiga marufuku viongozi wa vyama kutembelea mikoa wanayotaka?
katiba ya nchi inaruhusu free movement of people na kuishi popote watakapo
watanzania hatuna utambuzi tumejaa kukariri hata ujinga.
 
spencer

spencer

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
2,861
Likes
1,466
Points
280
spencer

spencer

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
2,861 1,466 280
Huu ni mtandao wa kiasi, waache wameshaanza kutapatapa wakati mkakati kuwaondoa unanukia.
Kila itu soon kitawekwa hadharani.

Siku zao za kumiliki kadi za chama zinahesabika
 
M

MAWERE

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2012
Messages
453
Likes
4
Points
35
M

MAWERE

JF-Expert Member
Joined May 24, 2012
453 4 35
kajisaidie ulale dhafu ,siasa zako za maji taka....mziki ni ule ule..ukileta umarufu kwenu..haturembi cdm!kavae gamba lumumba
 
K

kinauche

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
7,684
Likes
850
Points
280
Age
68
K

kinauche

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
7,684 850 280
post zingine za kitoto
nani mwenye uwezo wa kuwapiga marufuku viongozi wa vyama kutembelea mikoa wanayotaka?
katiba ya nchi inaruhusu free movement of people na kuishi popote watakapo
watanzania hatuna utambuzi tumejaa kukariri hata ujinga.
Kweli nakubali Zitto alikuwa msaliti wa kuda mrefu. Nadhani walimchelewesha sana kumwajibisha na kama wasingeshtuka hali ingekuwa ni mbaya zaidi. Ushauri wangu ni kwamba waliojiunga na chama kumfuata Zitto waondoke naye.
 
spencer

spencer

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
2,861
Likes
1,466
Points
280
spencer

spencer

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
2,861 1,466 280
Kweli nakubali Zitto alikuwa msaliti wa kuda mrefu. Nadhani walimchelewesha sana kumwajibisha na kama wasingeshtuka hali ingekuwa ni mbaya zaidi. Ushauri wangu ni kwamba waliojiunga na chama kumfuata Zitto waondoke naye.
Tena wamechelewa waende,
Huyo anawakiliosha mwanza ipi???
Mbona watu wazima tuko hapa hakuna hata anayemuonea huruma huyu ndumila kuwili.
Let them Go..............
 
W

Wimana

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Messages
2,453
Likes
23
Points
145
W

Wimana

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2012
2,453 23 145
post zingine za kitoto
nani mwenye uwezo wa kuwapiga marufuku viongozi wa vyama kutembelea mikoa wanayotaka?
katiba ya nchi inaruhusu free movement of people na kuishi popote watakapo
watanzania hatuna utambuzi tumejaa kukariri hata ujinga.
Kuna watu hata ukiwaita kuwa ni wapumbavu, bado utakuwa unawapa sifa. Huyo Gwalihenzi sijui anatoa wapi huo uwezo ambao hata Rais wa nchi hana. Ni upuuzi uliopita viwango vya upumbavu.
 
kamtu33

kamtu33

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2012
Messages
979
Likes
196
Points
60
kamtu33

kamtu33

JF-Expert Member
Joined Mar 15, 2012
979 196 60
Huyo anangea kama yeye au kwa niaba ya wananchi wa Kanda ya Magharibi kama alivyodai?
Zzk pole sana kama hao ndo uliowaweka wawe watetezi wako ndo wanaokumaliza kila uchwao kwa matamko! haya sasa Dec 4 ni kesho kutwa tusubili maamuzi ya matamko!.
 
lyinga

lyinga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2013
Messages
2,501
Likes
64
Points
0
lyinga

lyinga

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2013
2,501 64 0
Hahahahaaaa wachumia tumbo huku wengi sana yaani umeamka asubuhi hata hujanawa uso ushaanza kutoa matamko ya familia unasingizia wana mwnza kaazi kwelikweli cdm mwendo mdundo haturudi nyuma
 
Janjaweed

Janjaweed

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Messages
9,855
Likes
1,267
Points
280
Janjaweed

Janjaweed

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2010
9,855 1,267 280
Hahqhaaaaaa.... Kweli Hii safisha safisha ilikua muhimu, hivi kuna mtanzania anayeweza kuzuia mtanzania mwingine kufika eneo fulani?
 
salimkabora

salimkabora

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2012
Messages
2,449
Likes
84
Points
145
salimkabora

salimkabora

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2012
2,449 84 145

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa, wamepigwa marufuku kukanyaga jijini Mwanza.

Pamoja na onyo hilo, pia viongozi hao wametakiwa kufanya kila wanaloweza ili aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na wenzake waliovuliwa madaraka, warudishwe madarakani ndani ya siku nne kuanzia jana.

Kauli hizo zilitolewa jana na Mwenyekiti wa Vijana Kanda ya Magharibi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi ya CHADEMA, Mkoa wa Mwanza, Robert Gwanchele, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Gwanchele, yeye na wenzake wamelazimika kuchukua uamuzi huo kwa kuwa wanapinga kitendo cha kuvuliwa madaraka kwa viongozi hao kwa kuwa kilifanyika kinyume cha Katiba ya chama hicho.

“Pamoja na kuwapiga marufuku kukanyaga mkoani Mwanza viongozi hao wa kitaifa, kama Zitto, Dk. Mkumbo Kitila pamoja na Samson Mwigamba wasiporejeshwa madarakani, hadi Desemba 4 mwaka huu, vijana Kanda ya Magharibi tutaandaa maandamano yasiyo na ukomo kushinikiza Dk. Slaa na Mbowe wajiuzuru ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

“Chadema tumeingiliwa na mdudu aitwae ubinafsi kwani kuna baadhi ya viongozi wa chama ni makuwadi wa viongozi wetu wa ngazi za juu kufanya wanayotaka bila kuchukuliwa hatua.

“Chadema ni chama kinachojali watu wa upande fulani wa nchi, hivi viongozi kama Godbless Lema (Mbunge wa Arusha Mjini) pamoja na Kileo ambao waliamua kumshambulia Zitto kupitia mitandao ya kijamii wamechukuliwa hatua gani na chama?.

“Tutahakikisha tunawaondoa viongozi wote wa ngazi za juu kwa nguvu ya umma kwani Chadema sio mali ya mtu binafsi, chama hiki nicha wanachama.

“Hatutaki kuyumbishwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi, hao wanapaswa kukaa pembeni kwanza kupisha uchunguzi na kama hawataki kupisha nguvu ya umma itawaondoa na ndio maana sisi vijana wa Kanda ya Magharibi, tumeamua kuwapiga marufuku Mbowe na Dk. Slaa wasikanyage Mwanza kwani wao tayari wameamua kujijengea himaya yao isiyoguswa katika mikoa ya kaskazini, sasa Mwanza wanakuja kutafuta nini.

“Mbowe na Dk. Slaa ni watuhumiwa hawapaswi kuendelea kuwa viongozi wa Chadema, hao wanapaswa kujiondoa ili nao wachunguzwe juu ya matumizi mabaya ya fedha za chama,” alisema Gwanchele.

Pamoja na kuwashambulia Mbowe na Dk. Slaa, Gwanchele pia aliwarushia kombora wabunge wa Chadema wanaotoka Mkoa wa Mwanza kwa kile alichosema nao wameshiriki katika kuvuliwa madaraka kwa Zitto, Dk. Kitila na Mwigamba.

Kutokana na hali hiyo, alisema wabunge hao, Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiel Wenje (Nyamagana) na Salvatory Machemli (Ukerewe), wamepoteza uhalali wa kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Mwanza.

“Wabunge wa chadema Mkoa wa Mwanza hivi sasa wanajiona wako juu ya chama na wamekuwa wakitoa matamko ya kuunga mkono kuondolewa kwa Zitto na wenzake wakati sisi wananchi hatukuwatuma kufanya hayo.

“Kwa hiyo, nao wanapaswa kuondolewa madarakani mara moja kwa usaliti wao kwa wapiga kura wao,”alisema.
Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi labda wangekuja huko mwanza wangeuwawa kwa bomu la chupa ya petroli; lililo muhimu kwa sasa kwa cdm ni kuhakikisha huyo Slaa haendi kigoma wala mahali popote kwa sasa kwa kuwa ataingia kwenye mtego; picha kubwa ya harakati zote hizi tangu waraka wa siri wa zzk hadi matukio yanayoendelea sasa watu kutafuna pesa na kutoa matamko ya hovyohovyo ni ili kuonyesha chadema kuna mfarakano mkubwa na hata kesho au keshokutwa wakiuwawa viongozi wa juu wa chama itaonekana ni chadema tu wanashughulikiana. Mimi naona hili kama ndio mkakati wenyewe ingawa wenye kuupanga hawajui tu kwamba hiyo ni kuivuruga amani ya nchi na kuiingiza katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Wao ofcourse wana pesa watakimbilia nje lakini je bado watabakia kuwa watawala? hebu tujaribu kuwa na upeo jamani.
 
M

minze manonu

Member
Joined
Nov 27, 2013
Messages
50
Likes
1
Points
0
Age
28
M

minze manonu

Member
Joined Nov 27, 2013
50 1 0
Hvi hawa watu wanaojitokeza na kutoa matamko wamerogwa au wamechanganyikiwa, mna mamulaka gani juu ya Nguvu ya Umma mpaka mnadiriki kusema hvyo, ama kweli kuongozwa na masikin wa Pesa, akili na kiroho ni sawa na kuvuka mto ukiwa umefumba macho
 
piper

piper

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2012
Messages
3,255
Likes
12
Points
135
piper

piper

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2012
3,255 12 135
Hvi hawa watu wanaojitokeza na kutoa matamko wamerogwa au wamechanganyikiwa, mna mamulaka gani juu ya Nguvu ya Umma mpaka mnadiriki kusema hvyo, ama kweli kuongozwa na masikin wa Pesa, akili na kiroho ni sawa na kuvuka mto ukiwa umefumba macho
Well stated
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,252,104
Members 481,989
Posts 29,795,473