Baada ya kumuadhibu Ndala kisawasawa.. TFF tupeni kombe letu.

sembo

JF-Expert Member
May 25, 2011
4,351
2,000
Baada ya ushindi wa jana tuliopata dhidi ya Ndala... ilibidi nirejee katika "makablasha" yangu.. na kuangalia je kuna kizuizi chochote kilichobakia "barabarani"?!
Katika "makablasha" yangu, nimekuta wafuatao wanasubiri stahiki yao toka kwa Mnyama.

1. Simba SC Vs. Mbeya City
2. Kagera Sugar Vs. Simba SC
3. Mbao FC Vs. Simba SC
4. Toto African Vs. Simba SC
5. Simba SC Vs. African Lyon
6. Simba SC Vs. Mwadui FC

Ukiangalia hizo mechi, utagundua hakuna kizuizi chochote katika safari yetu ya kutawazwa kua mabingwa wa Vodacom Premier League, 2016/2017.. huku tukiwa tumebakiza mechi 2.. Sababu ni nyingi saaaana.. ila kwa leo nitatoa 2 tu [namba ya ushindi]..

1. KiAMa kukamilika.
[Ki - Kichuya.. A-Ajibu.. Ma-Mavugoal]. Na hii ni baada ya yule Mavugoal mwenye rekodi za kina CR7 na Messi, mechi moja goli moja ninayemjua mimi kurejea katika ubora wake. Mpaka sasa katika mechi 4 za VPL zilizopita katupia kambani goli 4.. Kuhusu Ajibu kila mtu anamfahamu.. Huyu Kichuya kawaongezea wanasayansi kazi nyingine tena.. mpaka napoandika mda huu, wanajiuliza.. jamaa anawezaje kufunga magoli ambayo katika "impossible angles"?!

2. Mtani Kuyumba.
Baada ya kuangalia makablasha yangu, nikaamua nichungulie kwa jirani.. Nilichokikuta kule ni hatari.. Huyu jamaa atatufanya tutangazwe mabingwa mapema saana. Kwa kiwango alichonacho kwa sasa na mechi alizobakiza na mechi alizobakiza ambazo zote ni za moto, huyu jamaa anatufanya tuanze sherehe mapema.. Picha linaanza mechi ijayo anapokutana na "ndugu zetu".. Azam FC.

Narudia tena kauli aliyoitoa Haji Manara, baada ya mechi jana.. "Hakuna wa kutuzuia kuchukua ubingwa msimu huu.. naaani?! narudia tena naaani?!" ...na sherehe za kusherekea ubingwa zianze.
 

miamia7

Senior Member
Jan 11, 2016
196
250
Mapema sana mikia,btw hili litakua kombe lenu la pili kuchukua baada ya lile mlilochukua zanzibar
 

WAIKORU

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
1,383
2,000
nimepend hapo ulipowaita Azam "ndugu zetu""...


kuhusu vyura fc...hata wakishuka daraja mimi roho yangu itaburudika sana...

Mnyama anatisha babaake...

vyura mwaafaaa
 

Man Thom

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
732
1,000
Tarehe 5 mwezi wa 3 ni Yanga na Mtibwa na sio Azam kama ulivyosema, mechi itapigwa uwanja wa taifa saa kumi kamili jioni! Yetu sie macho tu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom