Uchaguzi 2020 Baada ya kumsikiliza Tundu Lissu akiwa kwenye mkutano wa ACT-Wazalendo, nimejiridhisha ni mgombea dhaifu zaidi awamu hii

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Amesema:
1. CHADEMA wataisaidia ACT-Wazalendo kushinda Zanzibar
2. Baada kupona akiwa Ubelgiji ametembea sana na kwamba Tanzania ya Magufuli haina rafiki hata mmoja nje eti Mkapa hakuzikwa na mataifa ya nje
3. Wakienguliwa kugombea wataingia barabarani
4. Chadema wameweka wagombea Ubunge majimbo yote nchini

Kwa kauli hizi za Lissu , Watanzania mnachopaswa kujifunza hapa ni kuwa Lissu hakuna kitu kabisa. Lakini kauli zake zaidi zinatufundisha yafuatayo:-

1. CHADEMA wanawaogopa sana ACT-Wazalendo na wanaiona nafasi yao ya Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni ikipokonywa na ACT.na ndiyo maana Lissu alijikita sana kuejikanyaga kuelezea nia yao ya kuiunga mkono ACT kwa upande wa Zanzibar lengo ni ACT-Wazalendo kulegeza kamba kwa upande wa Bara, janja ileile ya Muungano wa UKAWA, ACT-Wazalendo komaeni. Kama Lissu anaamini katika umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu , basi awamu hii iwe ni zamu ya CHADEMA kuunga mkno mgombea wa chama lingine cha upinzani katika nafasi ya URAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tukifuata uhalisia Membe ni zaidi ya Lissu.

2. Kuna kila dalili kuwa uteuzi wa Lissu kuwa mgombea urais kupitia CHADEMA kuna mkono wa mabeberu kwa maana ya ufadhili(pesa, magari, vifaa vya Tehama kwa lengo la kuharibu uchaguzi), kufadhili machafuko n.k. hili linadhihirishwa na kauli yake kuwa.amezunguka sana nje na kwamba wakienguliwa wataingia barabarani. Waasisi wa machafuko ya Libya na Misri yaliowaondoa madarakani Ghadafi na Mubarak walianza na kuzunguka nchi za magaribi na kuhakikishiwa kufanikisha machafuko kwa maslahi ya nchi hizo na siyo kwa maslahi ya Libya na Misri.

Tukumbuke.kuwa wakati Rais Magufuli anapambana na kuhakikisha tunanufaika na madini yetu, ni Lissu huyu huyu aliyesema mabeberu yatatushitaki. Mabeberu yatashindwaje kumtumia wakati tangu awali alishaonesha nia ya kuwa kibaraka wao? Huko alikokuwa anazunguka alikuwa akizunguka kwa fedha za nani? Nadhani kauli zake zimetujibu. Uchaguzi wa Mwaka huu ni uchaguzi baina ya mzalendo na mabeberu (uchaguzi wa mleta maendeleo dhidi ya mfadhiliwa wa kuleta. Vurugu .nchini)

3. Wale waliokuwa wanajiita marafiki wa Tanzania ambao leo Lissu anasema siyo marafiki zetu eti kwasababu ya utawala.wa serikali ya awamu ya tano ni wanafiki, walikuwa wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa wakati tukisifika kuongoza kwa umasikini, hawawezi kupendezwa na Tanzania kuingia katika orodha ya nchi zenye uchumi wa kati, hawawezi kupendezwa na kusikia Tanzania inajenga Reli ya mwendokasi, tanzania ina Ndege 13, Tanzania ina Viwanda, Tanzania inajenga barabara za juu nk. Hawa ni sawa na Mtu anayefurahia kumnyenyekea/kumpigia magoti ukimuomba masaada kila wakati lakini kawe hawezi kufurahia kuona na wewe umepata. na huna haja na msaada wake/wewe siyo wa kumpigia magoti tena.

TUNDU LISSU NI DHAIFU , HANA HOJA NA WATANZANIA SIYO WALIBYA WALA WAMISRI
 
Sasa mkuu kama ni mgombea dhaifu , ACT wakomae nini tena badala ya kuwaombea ACT wamsapoti mgombea dhaifu ili nyie mpate mserereko, mshinde kwa kishindo?.

Huko alikozunguka, alizunguka kwa pesa za sisi walalahoi tuliomchangia cent 5 zetu tulizonazo ili atibiwe na zilizobaki atumie kuilisha familia yake na kuzunguka atakako.
 
Mnateseka sana... NI YEYE !!!
hqdefault-1.jpg


Jr
 
1. historia ndo mwalimu mzuri Lissu alianza kupambania madini kabla ya magu
2. angekuwa dhaifu hasingejaribiwa kuuwawa
3. kama una kumbukumbu nzuri maboresho ya sheria mama makinda alilitaja jina la lisu kuliko mwanasheria kipind kile bungeni
5. vuguvugu la mageuzi kwa nchi za uarabuni kumbukumbu unaongea wazi yalianzia Tunisia Kama siyo moroko kwa yule kijana muhitimu chuo kujichoma Moto kwa petroli baada ya kuvunjiwa kibanda chake Cha matunda.
6. huhisi act wanawahitaji zaidi chadema?haswa kwa upande wa bara?

so calm down chief wananchi ndo mwamuzi na siyo chama Kama kweli Kuna alilofanya hawezi kuwa na hofu na ulinzi kibao huku wakitangaza hii nchi ya amani,ifike kipind nyeupe tuseme nyeupe,pathetic
 
Unaogopa safari za Lissu nje ya nchi wakati nyie na genge lenu la mafia ndio mlisababisha apelekwe huko nje kwa matibabu, kama hamkutaka aende nje msingemjeruhi kwa risasi.

Hebu tulia, usichagulie watu wanaojitambua mgombea wao, nyie tayari mna Magufuli wenu mliyempitisha kwa fomu moja kama sultani.

Mwisho unamalizia kwa kusema Lissu hana hoja wakati kila akishika "mic" vyombo vya habari vinakatisha matangazo ghafla, au vinapunguza sauti makusudi nondo zake zisiwafikie huko lumumba.
 
CCM mnamuogopa sana Lissu,kutwa kucha mnajaza server kuanzisha nyuzi zinazomhusu Lissu, na hapa kampeni bado mnaanza kujinyea nyea,naona wote kibwagizo chenu ni kuenguliwa, mumezoea ushindi wa mezani. CCM bila mbeleko ya NEC na mabavu ya vyombo vya dola ni nyepesi kama TLP ya Mrema.
 
Back
Top Bottom