#COVID19 Baada ya Kumsikiliza na Kumuelewa vyema Dk. Seche Malecela, Kesho najipeleka mwenyewe Kupata Chanjo yangu ya UVIKO 19 niwe salama zaidi

Unakunywa pombe kila siku hujachunguza madhara ya pombe.

Unavuta sigara kila siku, hujachunguza madhara ya sigara.

Unapasha chakula kwenye microwave kila siku- huna wahi kuchunguza athari za mionzi.

Unapigwa na jua kila siku- hujachunguza madhara ya mionzi ya jua kwenye ngozi.

Unavuta polluted air kila siku

Condom hujui hata bei yake.
Jua halina madhara kwa Muafrika ambapo jua huwaka masaa 12 kila siku . Wadhungu ndio linawadhuru kutokana na mazingira ya kwao
 
Kuna Watu ambao achilia mbali tu Elimu zao kubwa bali hata uwezo wao mkubwa wa IQ na Kuchambua Masuala ya Kitaalam na Kitaaluma wakisema mambo GENTAMYCINE huwaamini na Kushawishika.

Kwa Ufafanuzi mzuri nilioupata kutoka kwa Mwanamama na Daktari Nguli Seche Malecela ( Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samuel Malecela ) kuhusu Chanjo hii ya UVIKO 19 Kesho asubuhi naanza Kuzunguka Hospitalini Kote Mkoani Dar es Salaam ili nikachanjwe nayo.

Nawatakieni kila la kheri wale Wote mnaomuamini Kibwetere aliyechangamka aliyeko Ubungo Mkoani Dar es Salaam ambaye anajinasibu ni Mchunga Kondoo wa Bwana wakati kumbe ni Tapeli tu wa Kiroho na Kiimani huku pia akiwa ni Muigizaji mzuri wa Sinema za Ngono Mitandaoni.

Ahsante sana Rais Samia kwa Chanjo hii.
Mimi bado nina mashaka sana na aliyoyasema kuhusu chimbuko la hii chanjo:-

1. Kwanini wataalamu wengine wakiwemo waliotengeneza hizi chanjo hawajawahi kusema kwamba chimbuko la chanjo yao ni utafiti wa huyo mwanasayansi wa tangu 2003!?

2. Kama kweli aliyoyasema ni sahihi kwamba hii chanjo utafiti wake ni mwendelezo wa utafiti ulioanza 2003 na hauhusishi vimelea vya kirusi cha corona kwanini huo ufafanuzi usitolewe na WHO wenyewe ili kuhamasisha jamii zichanjwe maana inaonekana itakuwa chanjo salama zaidi kuwahi kutokea duniani

3. Kwanini asijibu na hoja ya chanjo za magonjwa mengine Kama HIV na Maralia kushindikana hadi leo japo ugonjwa upo siku nyingi na huu wa corona wa juzi tu imewezekana!?
 
Pitia clinical authorities publications za chanzo, Gwajima yupo sawa kabisa, ila kuchanja ni hiari.
 
Mimi bado nina mashaka sana na aliyoyasema kuhusu chimbuko la hii chanjo:-

1. Kwanini wataalamu wengine wakiwemo waliotengeneza hizi chanjo hawajawahi kusema kwamba chimbuko la chanjo yao ni utafiti wa huyo mwanasayansi wa tangu 2003!?

2. Kama kweli aliyoyasema ni sahihi kwamba hii chanjo utafiti wake ni mwendelezo wa utafiti ulioanza 2003 na hauhusishi vimelea vya kirusi cha corona kwanini huo ufafanuzi usitolewe na WHO wenyewe ili kuhamasisha jamii zichanjwe maana inaonekana itakuwa chanjo salama zaidi kuwahi kutokea duniani

3. Kwanini asijibu na hoja ya chanjo za magonjwa mengine Kama HIV na Maralia kushindikana hadi leo japo ugonjwa upo siku nyingi na huu wa corona wa juzi tu imewezekana!?
Ukimsikiliza kwa makini Dr. Mwele, halafu ukasikiliza hotuba ya Bush ya 2005 na ya Obama ya 2008 kuhusu flue like pandemic, ni uthibitisho kuwa covid19 pandemic ni tukio la kupangwa, kwa hiyo everything is hoax, and the chanjo is just like a mouse trap.
 
Wengi wetu hatuna utamaduni wa kufatilia habari na mambo ya msingi.

Mwaka 2015 Wizara ya Afya ya Tz ilitutahadharisha kuhusu kirusi cha Corona kilochokuwa kimeshambulia Asia mwaka 2014. SOMA HAPA.

Na hapa JF taarifa ililetwa. Coronavirus disease: Mnaujua huu ugonjwa? SOMA HAPA

Mwaka 2013 Wizara ya Afya ilishatutaka tujihadhari na kirusi cha Corona kilichoshambulia Asia mwaka 2012
Taarifa ya wizara hii hapa. SOMA HAPA

Mwaka 2002 ugonjwa wa Corona ulipiga Asia hasa China. SOMA HAPA
 
Ukimsikiliza kwa makini Dr. Mwele, halafu ukasikiliza hotuba ya Bush ya 2005 na ya Obama ya 2008 kuhusu flue like pandemic, ni uthibitisho kuwa covid19 pandemic ni tukio la kupangwa, kwa hiyo everything is hoax, and the chanjo is just like a mouse trap.
Mkuu, ugonjwa ulikuwepo hata kabla ya hizo hotuba. Hata Wizara ya Afya ya Tanzania ilikuwa na taarifa hizo.
 
Ndugu yangu !!Afya yako ni muhimu sana.Ili jambo jambo halihitaji kukurupuka.Kwa sasa tuna bahati sana.Habari zote zipo Kiganjani mwetu.Sawa umemsikia Dr Malechela.

Lakin pia umesikia taarifa za huko USA jana ijumaa?Asilimia 75 ya waliochoma chanjo wanaumwa Covid serious. CDC imesema kati ya hao wengine walichoma chanjo mbili.Huu muda watanzania tujitahid kusoma taarifa Mara kwa Mara.Sio kama zamani tulivyodanganywa.
US imeachanja zaidi ya raia milion 300 ,una maanisha asilimia 75% ya hao wamepata covid19? Chanzo cha hii habari yako ni kipi?
 
Mkuu, ugonjwa ulikuwepo hata kabla ya hizo hotuba. Hata Wizara ya Afya ya Tanzania ilikuwa na taarifa hizo.
Mkuu nadhani ile ilikuwa Sars cov1.Hii ya sasa ni Sars cov 2 ingawa zote ni jamii za coronavirus ila zina utofauti kidogo.Hii ya sasa haijawahi kuwa contagious kwa binadamu kabla ya Wuhan cases.
 
Mkuu nadhani ile ilikuwa Sars cov1.Hii ya sasa ni Sars cov 2 ingawa zote ni jamii za coronavirus ila zina utofauti kidogo.Hii ya sasa haijawahi kuwa contagious kwa binadamu kabla ya Wuhan cases.
Ni kweli mkuu. Kirusi cha Corona ni familia kubwa, ndani yake kuna mamia ya virusi vya Corona ambavyo vimegawanywa katika familia ndogo kuu 4 na zote zinafahamika, hivyo kiongozi anaweza toa tahadhari ya kesho.
 
Nawatakieni kila la kheri wale Wote mnaomuamini Kibwetere aliyechangamka aliyeko Ubungo Mkoani Dar es Salaam ambaye anajinasibu ni Mchunga Kondoo wa Bwana wakati kumbe ni Tapeli tu wa Kiroho na Kiimani huku pia akiwa ni Muigizaji mzuri wa Sinema za Ngono Mitandaoni.
umeenda vyema lakin Tatizi limeanzia hapa
 
Nimemsikiliza kwa makini daktari bingwa Malecela.

Ameelezea vizuri sana ila tu kuna sehemu mbili zinahitaji mjadala zaidi.

Suala la hizi chanjo za mRNA kuwepo kwa muda mrefu kabla ni sahihi lakini kwa kiasi kikubwa kipindi hicho anachosema kilikuwa Exploratory and pre-clinical stage.

Chanjo inapokuwa developed inapitia stage kuu kama tatu hivi;Exploratory stage,kipindi ambacho wataalamu wanaumiza vichwa kwa research za kugundua na kutengeneza dawa/vidudu pandikizi ambazo zitaendelezwa na kufanyiwa testing ili kuona kama zinafaa kukinga magonjwa fulani wanayoyalenga.

Then wakishazitengeneza wanaanza kuzifanyia testing maabara kwa kuzipandikiza kwenye vitu fulani vinaitwa culture pamoja na wanyama ili kuona kama zina ufanisi kwa kusudio husika.Hii inaitwa pre-clinical stage.

Chanjo ikivuka hapo ndipo inakwenda kutafutiwa kibali cha kufanya majaribio kwa binadamu halisi(clinical development) ambayo nayo huwa na stages kuanzia watu wachache hadi kuhusisha watu wengi.

Sasa nadhani watu wanapozungumzia muda mfupi wa chanjo hizi za covid wanamaanisha clinical development stage.(na nadhani wana hoja ya msingi sana hapa).

Kirusi cha covid kimegunduliwa mwaka 2019.Kabla ya hapo kilionekana kwa popo kikiwa hakina uwezo wa kuhamia kwa human host.
So hili ni somo jipya kwa wanasayansi ambalo lilihitaji muda wa kutosha kuelewa nini kinaendelea kwa mgeni huyu kuingia kwa binadamu.

Suala la pili ni pale aliposema kuwa habari ya chanjo hizi kuathiri DNA ni arguments za mitandaoni..with all due respect hapana..huu ni mjadala wa kisayansi umeanzishwa na wanasayansi na unahitaji majibu ya kisayansi.It's not a mere belief,its scientific argument.

Sayansi ya mRNA vaccine imechukua advantage ya sayansi ya mwili ili kufanya matibabu mwilini.How?

Katika seli kuna kitu kinaitwa nucleus,ndio makao makuu ya seli ambamo chembe ndogo inayobeba taarifa zote za uundaji na uendelezaji wa kiumbe husika inahifadhiwa.Chembe hiyo huitwa DNA.Sayansi yote ya binadamu imo ndani ya DNA.Ramani nzima ya utu wako imo humo.If anybody tamper with it,then you are finished.

Inapotokea mwili unataka kufanyika kitendo fulani cha uundaji au maintenance,DNA hutoa taarifa za kinachotakiwa kufanyika na kuiweka taarifa hiyo kwenye muundo fulani unaoweza kusomeka(message) na sehemu nyingine za seli.Huo muundo unaitwa RNA.
RNA(message) inakwenda kwenye sehemu nyingine ya seli inayohusika na utengenezaji inaitwa cytoplasm.Ndani ya cytoplasm kuna kitu kinaitwa ribosomes ndicho kinadecode RNA message na kutengeneza protein (matofali) zinazokwenda nje ya seli kufanya ujenzi au tukio lililokusudiwa.

Covid 19 virus anachofanya ni kuingia kwenye seli ya mwili na kutuma RNA zake kuinstruct seli itengeneze genetic materials kuunda more viruses.Kwa maana zaidi ni kuwa anaiteka na kuigeuza seli kuwa kiwanda cha kuzalisha virus wenzie zaidi.

Katika kufanya ufedhuli wake huo huyu virus anatumia kiungo fulani mwilini mwake kujiunganisha na seli ya host wake.Hicho kiungo kinaitwa spike protein.Ni kama hook fulani ambayo anainasisha kwenye cell surface ya host na kuigeuza mrija wa kupitishia RNA zake.So presence ya spike protein kwenye mwili wa virus ndio silaha kuu ya kujipenyeza na kuidhibiti seli ya host wake.

Mfumo wa ulinzi wa mwili huchukua muda kutambua mgeni huyu ambaye hajawahi kuonekana kabla.So wakati immune system inajivuta kumwelewa ili imshughulikie yeye muda huo anautumia kuathiri seli nyingi zaidi na kuzalisha virus wengi.Ndio maana natural immunity kama iko chini inakuwa shida kupambana na corona sababu hii by the time imetambua adui na kuanzisha vita inakuwa tayari viral load ni kubwa sasa kama mtu ana weak immunity ndio tatizo linakuwa kubwa zaidi.

Chanjo ya mRNA nayo inautumia mfumo ule ule kuusaidia mwili mapema kupambana kabla hali haijawa mbaya.

Yenyewe inaipa immune system uwezo wa kutambua virus mapema ili kumshughulikia mapema kabisa asisambae. So timing is the key.

Wazungu walichunguza genetic codes za virus wakachukua kipande kidogo cha information zinazohusu namna anavyounda ile spike protein yake wakatengeneza RNA yao maabara na kuiweka kwenye vaccine.

So hiyo RNA ya vaccine imebeba instruction ya kutengeneza ile sehemu ya kirusi inayotumika kujiunganisha na seli(spike proteins).

Unapodungwa vaccine ile RNA (mRNA) iliyowekwa humo inakwenda kwenye cytoplasm ya seli mwilini na kuinstruct seli itengeneze spike proteins.
As a result seli inatengeneza spike proteins nyingi lakini sababu ni hizo spikes tu na sio mdudu kamili inakuwa haina madhara kwa mwili ISIPOKUWA kitendo hiki kinaistua immunity ya mwili na kugundua kuna kitu kisichohusika kwenye mwili na kuanza kushambulia.
Immunity ikishatambua kuwa kitu fulani hakihitajiki basi inaweka memory hata baada ya miaka kikiingia tena kinakuwa kishatambulika na kushambuliwa.Ni kwa jinsi hiyo tunapata herd immunity.

So baadae hata akiingia virus mwenyewe as long as ana zile spike proteins ambazo immune imeshakuwa programmed kuzitambua kama antibodies anashambuliwa mapema kabla hajajizalisha zaidi na kwa namna hii ndivyo chanjo ya mRNA inasaidia.

HATA HIVYO kuna argument ya kisayansi kwamba kitendo cha seli ya mwili kugeuza DNA yake kuwa RNA ni kitendo kinachoweza kuwa reversed(reverse transcription) in presence of certain enzymes.Yaani under certain foreign influence inawezekana RNA ikageuka tena kuwa DNA.
Hapo ndipo huja hoja ya uhatari wa kutumia teknolojia hii ya kuinject foreign RNA kwenye human cell.

Kuna watu wanauliza hii mRNA ya vaccine ikishafanya kazi yake ya kuinstruct seli kutengeneza spike proteins yenyewe inakwenda wapi?
Wanaambiwa kuwa mwili ukianza kuzishighulikia zile spikes inashughulikia na hiyo RNA na host cell.
Linaulizwa swali jingine,sasa inakuwaje baadhi ya watu walioumwa na kupona covid wakipimwa kwa kile kipimo maalum kinachotambua genetic codes za virus wanaonekana kuwa positive ilhali damu zao ziko clean hazina viral load tena?hii imprint inayosomwa na kipimo inatokea wapi?kipimo kinasoma kitu gani?!!!

Kuna swali linaulizwa,je kitendo cha mwili kutegemea genetic instruction toka nje ili kutrigger immune response hakiathiri natural body immunity in the long run?
Na watu wamefanya research na kugundua wagonjwa waliopona covid kwa kuacha natural immunity response ifanye kazi wako stable na salama zaidi dhidi ya future infection kuliko wale ambao wamechanjwa.Watu wanachanjwa na bado wanaugua tena.Natural immunity ni strong hata kwa variants compared to vaccine immunity kwa mujibu wa baadhi ya research.So why hatuzungumzii kuwawezesha pia wale wenye natural immune(na ni wengi zaidi) badala yake tunawazodoa wasipochanja?kwanini hawawekwi kwenye jedwali na tunawalazimisha kuchanja?!

So you can see hii ni mijadala ya kisayansi na sio ya mere beliefs.

Inahitaji majibu na sio kuwa dragged.
 
Kirusi cha covid kimegunduliwa mwaka 2019.Kabla ya hapo kilionekana kwa popo kikiwa hakina uwezo wa kuhamia kwa human host.
So hili ni somo jipya kwa wanasayansi ambalo lilihitaji muda wa kutosha kuelewa nini kinaendelea kwa mgeni huyu kuingia kwa binadamu.
Kwanza mkuu hakuna kirusi kinachoitwa Covid kama ulivyokitaja. Najua umepitiwa kidogo. Kirusi cha sasa kinaitwa SARS-CoV-2 kilichoibuka mwaka 2019, kinafanana kwa 86% na SARS-CoV-1 kilichoibukia China mwaka 2002.

Familia ya virusi vya Corona inafanana sana. Vipo vinavyofanana hadi kwa 96% mfano hiki kinachosumbua sasa SARS-Cov-2 na RaTG13. So, study iliyoanza mwaka 2003 ingeweza kutoa dira hata kwa SARS-COV-2 na jamii nyingine ya Corona Virus.
 
Kwanza mkuu hakuna kirusi kinachoitwa Covid kama ulivyokitaja. Kirusi cha sasa kinaitwa SARS-CoV-2 cha 2019, kinafanana kwa 86% na SARS-CoV-1 kilichoibukia China mwaka 2002. Familia ya virusi vya Corona inafanana sana. Vipo vinavyofanana hadi kwa 96% mfano RaTG13. So, study iliyoanza mwaka 2013 ingeweza kutoa dira hata kwa SARS-COV-2 na jamii nyingine ya Corona Virus.
Safi sana mkuu,sema hawa watu wameaminishwa vibaya,so kuelewa somo sio kazi rahisi,wanaishi kwa hisia na sio kwa uhalisia.
 
Kuna Watu ambao achilia mbali tu Elimu zao kubwa bali hata uwezo wao mkubwa wa IQ na Kuchambua Masuala ya Kitaalam na Kitaaluma wakisema mambo GENTAMYCINE huwaamini na Kushawishika.

Kwa Ufafanuzi mzuri nilioupata kutoka kwa Mwanamama na Daktari Nguli Seche Malecela ( Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samuel Malecela ) kuhusu Chanjo hii ya UVIKO 19 Kesho asubuhi naanza Kuzunguka Hospitalini Kote Mkoani Dar es Salaam ili nikachanjwe nayo.

Nawatakieni kila la kheri wale Wote mnaomuamini Kibwetere aliyechangamka aliyeko Ubungo Mkoani Dar es Salaam ambaye anajinasibu ni Mchunga Kondoo wa Bwana wakati kumbe ni Tapeli tu wa Kiroho na Kiimani huku pia akiwa ni Muigizaji mzuri wa Sinema za Ngono Mitandaoni.

Ahsante sana Rais Samia kwa Chanjo hii.
Si kesho jumatatu ndio rasmi wanaanza, chanjo Ni muhimu Sana!
 
Tuna watu wa ajabu sana,mtu anakwambia hio ndio Chapa ya 666,kwahio ukiikwepa unasubiri kunyakuliwa na Yesu,mtu anasema hayo yupo baa analewa baadae anatafuta Malaya halafu anasema anasubiri kunyakuliwa.

Amesahau kwamba kuna amri kumi za Mungu.
Mungu akubariki sana Farolito .
 
Back
Top Bottom