Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 127
Heshima zenu wanaJF,
Nimesoma habari iliyotolewa na Chadema ya kutomtambua Rais na matokeo ya Urais kwa ujumla. Kitu ambacho kimenistaajabisha au sijakielewa nahitaji kueleweshwa pengine uwezo wangu wa kuchanganua mambo ni mdogo ni kuwa Rais ni sehemu ya Bunge na Wabunge hawawezi kufanya kazi bila kumshirikisha Rais. Unapopitshwa mswada na Bunge Rais anausaini na unakuwa sheria.
Kwa jinsi nionavyo mimi kitendo cha kumkataa Rais na kuendelea kufanya kazi nae kina walakini unless kuna interest ndani yake na hilo nadhani maslahi ndio yanayowafanya Chadema wawe watumwa wa kauli yao. Wanaogopa wakifreez hawatapata ruzuku hawata pata posho za ubunge na za KUB.
Nimefikiria sana na kujiuliza mbona Chadema walikuwa na mchecheto wa kukimbilia kuongoza kambi ya upinzani bungeni na Rais ni sehemu ya bunge na Rais huyo huyo wanadai leo hii hawamtambui? hivi mwenye akili timamu na mwenye ku reason out haoni kuna namna hapo? Mimi ndio maana nimeamua kuachana na sihasa za kibongo kwani zimejaa unafiki mwingi na unaweza kuumia kichwa kwa kufikiria mambo yanvyoenda. Kule visiwani vyama vimeungana hujui nani mshindi nani kashindwa tunaambiwa wote wameshinda. Huku Bara kuna chama kinakataa kumtambua Rais lakini wapo tayari kufanya kazi chini yake! Kuna wengine wanasema eti kile chama cha upinzani kule visiwani ni CCM B kwahili mie nataka nifikiri na hiki kinachofanya mambo kinafki ni CCM C !
Kule visiwani kuna kipindi kama sikosei mwaka 1995 chama kikuu cha upinzani kilisusia matokeo ya uchaguzi na shughuli zote za baraza la uwakilishi na wakatamka bayana hawamtambui Rais tena kwa vitendo sio kwa maneno. Sisemi na Chadema wafanye hivyo laaa maana adhari zake zilikuwa kubwa na zilizopelekea uhasama mkubwa baina ya wananchi huku viongozi wakikuta wanagonga tano refer to Slaa na Pinda nje ya viwanja vya bunge dodoma juzi!
Angalizo:
Wananchi wazalendo na wapenda maendeleo fanyeni kazi kwa bidii kuinua tija ya maisha yetu wanasiasa wapo zaidi kimaslahi kuliko kuwakwamua wananchi kwenye lindi la umasikini. Hakuna atakae fanya saruji ishuke bei na hakuna atakae leta maisha bora kwa kila mtanzania bila ya mtanzania huyo kufanya kazi itakayomletea kipato na kujihakikishia maisha bora.
Nawakilisha.