Baada ya kumkamata mchina*(ubaguzi) wenye mabwawa ya samaki, wafugaji na wamwagiliaji, eti kina cha maji kimeongezeka!

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,564
2,000
Kwahio huyo waziri mpenda sifa na Magu hawatofautiani sana,kama Jinsi alivyo okota vichwa vya treni pale bandarini?
Ni pipa na mfuniko!!msanii tu, jana anaulizwa kuhusu Ponds za samaki, hizo 26, ambazo wawekezaji wana vibari, vya kutumia maji hayo, anakimbia kimbia tu!!zigo anaenda kutwishwa mtendaji wa kata eti alikuwa wapi, watu wanatumia maji ovyo!!sasa watu wana vibali toka bodi ya bonde husika wewe mtendaji unasauti ipi tena?!!
 

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,441
2,000
Mamlaka ya maji inajitapa kuwa baada ya kuwakamata waliokuwa wanachepusha maji imewasja mtambo wa Ubungo baada ya kina cha maji kuongezeka! Sijui ni utaalamu gani huu au ni siasa. Kina cha maji kinawezaje kuongezeka wakati yanakoanzia maji hakuna ongezeko la maji! Jibu tutalipata wiki ijayo mgao wa maji utakapo isha.
Nikisema kuna watu ni Wapuuzi naambiwa eti Mimi sio Mzalendo, asante sana mleta mada
 

Thesis

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
1,605
2,000
Duu kumbe hata mabwawa ya kuhifadhi maji hakuna ?
Hao wataalamu bogus kabisa na mawaziri wote wa maji wamepita bila kuliona hilo

Sikulijua hili poleni sana
Tuanze na sisi wenyewe at individual level, Je huwa tunavuna kiasi gani cha maji msimu wa mvua kutoka kwenye maji yanayotiririka kwenye mapaa ya nyumba zetu? Kwa maoni yangu Nchi yetu haiwezi mudu Gharama za kutengeneza bwawa la kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya watu milioni 5 wa jiji la Dar kutumia mwaka mzima
 

Thesis

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
1,605
2,000
Ninakumbuka zamani mji wa Mbeya haukuwa na bwawa pamoja na maji kutiririka toka milimani, mji wa Iringa pia wanakinga maji kwenye mto Ruaha badala ya bwawa, Morogoro Mindu lilijengwa miaka ya tisini mwanzoni, nalo linanaharibiwa na wachimba dhahabu hivyo halijafikia lengo, Tabora Gombe lilijengwa na mwingereza kabla ya uhuru, Dodoma Mtera ingeweza kuipatia maji.
Maji ya Mtera huwezi kupeleka Dodoma kwasababu ndiyo hayo yakitoka hapo yanaenda kuzalisha umeme kwenye bwawa la kidatu. Ukipeleka Dodoma ina maana bwawa la kidatu life.
 

Thesis

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
1,605
2,000
Inanikumbusha wakati wa Nyerere kulikuwa na uhaba wa chakula, msako ulifanyika majumbani kutafuta wanaoficha chakula, wakapatika wenye ndoo za mchele na unga tukawaita wahujumu uchumi, nafaka hizo zikapelekwa kwenye maduka ya bidhaa muhimu watu na mawe wakajipanga foleni kununua, waliofanikiwa kuuziwa watu wachache tu zikaisha, tatizo likabaki palepale mpaka mmarekani akatuletea yanga na mchina akaleta kitumbo.
Hahaha walifanya maamuzi ya kidwanzi, walidhani wangelisha taifa kwa chakula walichohifadhi watu mia!! Tena kwenye vigunia kumi, ishirini!
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,292
2,000
Wewe at individual level huwa unavuna kiasi gani cha maji msimu wa mvua? Unajua gharama za kutengeneza bwawa la kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya watu milioni 5 wa jiji la dar?
Kwahiyo serikali haina uwezo wa kujenga bwawa! Kwa taarifa yako serikali inao uwezo huo.
 

Thesis

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
1,605
2,000
Kwahiyo serikali haina uwezo wa kujenga bwawa! Kwa taarifa yako serikali inao uwezo huo.
Mkuu, serikali yenyewe hapo ilipo ina madeni ambayo hata hatujui yataisha lini. Ukiachana na madeni bado kuna vipaumbele vingine vingi sana. Inawezekana lkn at the expense of other priorities au tuongeze tozo
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,292
2,000
Mkuu, serikali yenyewe hapo ilipo ina madeni ambayo hata hatujui yataisha lini. Ukiachana na madeni bado kuna vipaumbele vingine vingi sana. Inawezekana lkn at the expense of other priorities au tuongeze tozo
Tangu tumepata uhuru wangeweza kujenga endapo wangekuwa na akili hiyo, wao walibakia na walichoachiwa na mwingereza.
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
18,884
2,000
Tuanze na sisi wenyewe at individual level huwa tunavuna kiasi gani cha maji msimu wa mvua kutoka kwenye maji yanayotiririka kwenye mapaa ya nyumba zetu? Kwa maoni yangu Nchi yetu haiwezi mudu Gharama za kutengeneza bwawa la kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya watu milioni 5 wa jiji la Dar kutumia mwaka mzima

Kwa kweli hakuna tu
Maana kuhifadhi pipa la maji huko sio kuvuna na ndio wengi wanategemea pipa na madebe na ndoo tu

Kwa serikali Ina uwezo huo na zaidi ya hapo mkuu ila nani wa kusimamia na kutoa mwongozo?

Tatizo letu mambo hayaendi bila kufokewa na kutumbuliwa sijui kwa nini
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
7,959
2,000
Ukweli Ni kwamba sehemu nyingi Dar hakuna maji.
Jiongelesheni mtakavyo mkitegemea mileage za kisiasa lakini magonjwa ya mlipuko yatakapoanza ndio ukweli utakapo jitenga na blah blah za kufanya vikao vya kukurupuka usiku.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom