Baada ya kumjali na kupigania mafanikio yake, leo nimegeuka kuwa mshamba

Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,644
2,000
Nilimkuta akiwa ana stress za maisha baada ya kumaliza masomo yake katika chuo fulani. Nilimshika mkono, nikamfuta machozi kisha nikampenda na nikamfundisha kunipenda, nikaishi nae kwa zaidi ya miez kumi. sikuhitaji kumuona akiwa katika msongo wa mawazo bali nilitafiti nikagundua shauku yake ilikuwa ni kupata kazi au biashara ainue familia yake na ajenge mustakabali wa maisha yake.

Niliamini katika falsafa ya ushirikiano katika kujenga mustakabali wetu kwani kila mara alionyesha kuwa mimi ni chagua sahihi kwa kauli na matendo. Nilipambana kwa hali na Mali kwa kipato changu cha kawaida na hii exposure ndogo mpaka nikafanikiwa akapata kazi kwenye shirika moja la miradi ya afya hapa nchini akaenda kufanya kazi nje ya mkoa niliopo mimi.

Wiki mbili baada tu ya kuajiriwa alibadilika sana alibadilika sana, ninaweza kumpigia simu nakuta yuko busy kuanzia saa tano mpaka saa saba usiku na anaona simu yangu inaingia hapokei na akimaliza kuongea hanitafuti hata nikimuulza hatak kusema anaongea na nani, akaenda mbali zaid ukimtumia sms anakujib kwa mkato na ikafikia hatua hataki kunitafuta na nikimtafuta hapokei simu.

Nimewahi kwenda huko anakofanyia kazi nimekaa siku tatu yaani muda wote hajiamini na hawez kutoka nje akaongozana na mm. Dharau na kiburi ndio umekuwa mtindo wa maisha yake. Naishia kuitwa mshamba kwa kumfatilia eti nijiamini. Kifupi nimejitoa kwa mengi nikijua huyu atakuwa mke wangu halaf amekuja kunibadilikia ghafla, inauma sana na Niko katika wakati mgumu sana ukizingatia niko naandika tasnifu yangu niweze kumaliza shahada yangu ya uzamili lakini nashindwa hata kusimamia biashara zangu zinanishinda.

Nabaki muda wote ndani nimejifungia tu roho inaniuma sana kila nikiwaza mawazo yangu yananipeleka mbali zaidi ya jinsi ambavyo siwez kuelezea, nimepitia changamoto nyingi katika maisha yangu lakin hili naona linanizidi.. ndugu zangu naona kabisa jahazi linazama.

Mwenye ushauri mzuri utakaonisaidia na kunitoa ktk hii hali naomba aje PM au hapa hadharani anishauri. Jf naona ndio second home yangu naamini ndugu zangu wenye busara zaidi mtanisaidia.
Tafuta penzi jipya msahau Usonge mbele wanawake wapo wengi tu
 
SCE

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
6,676
2,000
Atakuwa ni mpenzi wako wa kwanza huyo.

Ukipata mwingine akakupiga tukio kama hilo tena ndo utakuwa umefuzu.

Utakuwa sawa muda si mrefu, ila ukiendelea na ujinga wako wa kukaa ndani utachelewa kuwa sawa.
Mamaee😂😂😂😂
 
mapanga25

JF-Expert Member
May 2, 2020
670
1,000
Ni bora udisco hyo masters maana unazingua,hiyo hesabu kama sadaka mwaego. pambana usijedisco kwa vitu vya kijingà
 
Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
14,865
2,000
Achana nae bro bora ukasaidia ndugu zako watakusaidia au hata watasaidia watoto wako huko mbeleni achana na wanawake.
 
steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
7,016
2,000
Akikuelewa hapa basi inatosha.

Tenda wema nenda zako usingoje fadhila.

Fadhila mfadhili mbuzi binadamu hutomweza ,mbuzi utamla nyama ,mchuzi na supu.

Unajipa stress komaa malizia tasnifu yako focus kwenye mitikasi yako .

Usiwaendekeze Hawa viumbe kachapiwa nikki wa pili wistaz utakuwa wewe

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Haswaaaaa
 
Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
853
1,000
Nilimkuta akiwa ana stress za maisha baada ya kumaliza masomo yake katika chuo fulani. Nilimshika mkono, nikamfuta machozi kisha nikampenda na nikamfundisha kunipenda, nikaishi nae kwa zaidi ya miez kumi. sikuhitaji kumuona akiwa katika msongo wa mawazo bali nilitafiti nikagundua shauku yake ilikuwa ni kupata kazi au biashara ainue familia yake na ajenge mustakabali wa maisha yake.

Niliamini katika falsafa ya ushirikiano katika kujenga mustakabali wetu kwani kila mara alionyesha kuwa mimi ni chagua sahihi kwa kauli na matendo. Nilipambana kwa hali na Mali kwa kipato changu cha kawaida na hii exposure ndogo mpaka nikafanikiwa akapata kazi kwenye shirika moja la miradi ya afya hapa nchini akaenda kufanya kazi nje ya mkoa niliopo mimi.

Wiki mbili baada tu ya kuajiriwa alibadilika sana alibadilika sana, ninaweza kumpigia simu nakuta yuko busy kuanzia saa tano mpaka saa saba usiku na anaona simu yangu inaingia hapokei na akimaliza kuongea hanitafuti hata nikimuulza hatak kusema anaongea na nani, akaenda mbali zaid ukimtumia sms anakujib kwa mkato na ikafikia hatua hataki kunitafuta na nikimtafuta hapokei simu.

Nimewahi kwenda huko anakofanyia kazi nimekaa siku tatu yaani muda wote hajiamini na hawez kutoka nje akaongozana na mm. Dharau na kiburi ndio umekuwa mtindo wa maisha yake. Naishia kuitwa mshamba kwa kumfatilia eti nijiamini. Kifupi nimejitoa kwa mengi nikijua huyu atakuwa mke wangu halaf amekuja kunibadilikia ghafla, inauma sana na Niko katika wakati mgumu sana ukizingatia niko naandika tasnifu yangu niweze kumaliza shahada yangu ya uzamili lakini nashindwa hata kusimamia biashara zangu zinanishinda.

Nabaki muda wote ndani nimejifungia tu roho inaniuma sana kila nikiwaza mawazo yangu yananipeleka mbali zaidi ya jinsi ambavyo siwez kuelezea, nimepitia changamoto nyingi katika maisha yangu lakin hili naona linanizidi.. ndugu zangu naona kabisa jahazi linazama.

Mwenye ushauri mzuri utakaonisaidia na kunitoa ktk hii hali naomba aje PM au hapa hadharani anishauri. Jf naona ndio second home yangu naamini ndugu zangu wenye busara zaidi mtanisaidia.
Bro kupenda hakuna thamani Tena.
Tongoza TOMB*** SEPA.

#YNWA
 
Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
853
1,000
Kama ni wa kwako atarudi, kama si wa kwako potezea. Na sio ndo ukae umsubiri. Fanya maisha yako jomba. Muache ajifunze na aone hayo anayoyafanya ni ya kawaida sana. Kama yana umuhimu kwake ataendelea nayo. Akiona wewe una umuhimu kwake atarudi.
Na usisahau kumwambia, wanawake wa siku hizii HAWAPENDEKI.
Just HIT and RUN

#YNWA
 
Pendael24

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
3,682
2,000
Pole Sana ndugu, Ni bahati mbaya Sana hawa wenzetu hawajui kumwacha mtu bila ya kumsababishia maumivu.

Kwa sisi wengine tuliopitia hali kama hio kweli tulipima hio changamoyo na kuona hakuna changamoto inayolingana na hio hali.

Lakini baadae tulipokaa sawa tuliona Ni kawaida sana tena Sana.

Hivyo tulia, endelea na Mambo yako ya muhimu.

Mimi nadhani sababu kubwa zaidi ya changamoto wanazokutana nazo wakina mama zinatokana na matendo yao ya awali, wamekua sababu ya maumivu kwa wengi , ndio maana kila leo wamejazana kwa wachungaji na manabii wakiendelea kupata mauvu.
 
clecla

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
733
1,000
Best option n pamoja n kukubali kumpoteza Kwa moyo mweupe,,,,, mkuu now days hatulazimishi penzi,,,, stay strong and move on
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
111,671
2,000
Hahahahaha eti KIMCHARUKO! 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Yaani uache kusimamia biashara Kwa kuwaza hiko kimcharuko?..
Seriously?...

Unatakiwa umshukuru Mungu umeona rangi zake mapema sana...asije kukusumbua huku ushazaa nae na ushamuoa
 
jaap

JF-Expert Member
Dec 25, 2018
1,201
2,000
Kila siku tunawaambia mwanamke hasomeshwi wala kumtafutia kazi
Wazazi wake hawakumtafutia kazi wanajua mapungufu ya mtoto wao

Sasa wewe mbuzi mmoja umeyavaa
Mkuu kwani kila wazaz wana uwezo kweli wa kuwatafutia Kaz watoto wao ?
 
Maya Angelou

JF-Expert Member
Oct 19, 2019
730
1,000
Sometimes letting go is the best way to go!!Kwa kuzingatia sasa Ana mshahara wake , nakushauri kama ifuatavyo

Embu wewe mwenyewe Jiondoe kwake.

Kata Nyuzi ya Mawasiliano iliyokuwepo.
Ndiooo ,usimtafute kwa meseji, kwa simu wala kwann,
Achana na hasra, chuki nakuwaza ulichowekeza, amini nakuambia kadri ambavyo unayawaza haya ndivo unazidi kuumia.

Kuwa Chanya...yaan jipende, kuanzia mavazi, mwonekano, maisha ,kazi ,kua mwenye furaha

HAKIKISHA UNAMUONYESHA KUA UNAFURAHA BILA KUMTAFUTA, ..WATU WABAYA WANAKAWAIDA YA KUTAKA KUONA UBAYA ALOKUFANYIA UNAKUONDOLEA FURAHA. NAHAPA UKIWAJULIA, NIWAO WENYEWE WATAUMIA ( ZINGATIA SANA HILI) .

Hakikisha Sanaaa Hauwi mtu wa mitandaoni sanaaaa , ila kua mtu wa mtandaon kwa 'Nadra yenye Uhakika".. Hapa lengo ni kumrudisha kama bado unamhitaj, nahapohapo lengo nikuendelea na Maisha yako wewe kama wewe.

Kwahiyo,
ACHA KUPOST POSTS ZINAKUONYESHA UNA HUDHUNI ,ACHA KABISAAAA.
kama ni jumbe ,tafuta zile jumbe zinazokuonyesha una furaha mfano"Life is full of surprises "..... Love and happiness ".
Yaaan ukipost leo, unatulia kama siku nne au wiki unapost tena , kama ni picha Weka zinazokuonyesha umecheka ,umetabasamu, uko na jamaa zako wakike au wakiume mkifurahi.

Hakikisha Asijue ratiba za Maisha yako kupitia mtandao..yaan hapa asijue upo wapi siku hizi, unafanya nn, upo na nani n.k

USITUMIE WATU KUMBEMBELEZA.

USIJE KUMBEMBELEZA, AU KUMUOMBA MSAMAHA, KUJARIBU KUHOJI KUNAN, KWANN KABADILIKA N.K ACHAAAAAAAAAAAAAA.

HIZI MBUZI ZISIZOJIELEWA ,HUJA KWENYE MAISHA KUFUNDISHA ..NAHIVO JIONE WEWE NI BORA, WA THAMAN, HB, MWENYE MAISHA. HUWEZ AMIN, ASIPOJIRUDI, ATAKUJA BOOOOONGE LA DEMU KISUUUUUUUU KIKALIIII PISI YENYE KUUMBWA NA KUUMBIKA, ACHANA NAHILO GARI LA MKAA.

katika ubora wako
 
Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
2,304
2,000
Wakati naanza kusoma nilihisi wewe ni Wakike ivo kuna Njemba opportunist imekutumia na kukudump kumbe sivo aisee, Nakushauri kwa sasa kaa pembeni na observe pengine huyo mwanamke yupo Kwenye Golden age ambayo hio age itapita very soon na mpaka ipite tayari atakuwa na Mtoto atakuwaza sana na kutamani kurudi kwako, Huo ndio wakati sasa wa wewe pia kumuumiza tena sana halafu unamuacha mzee
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom