LICHADI
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 4,124
- 11,114
Nikikaa nikifikiria hela yangu inavyopasuliwa kwenye mshahara wangu ambao ni jasho langu alafu anayechukua hizo hela ananipangia masharti ya kunilipa roho yangu inaniuma sana, Nikiangalia mshahara wangu kiwango nnachokatwa kwenda NSSF ni kikubwa.
Naona sio mafao tena bali ni sadaka hii natoa kwa mipango ya watu fulani na sio kwa manufaa yangu wallahi. Kama kipindi cha Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete watu walichukua pesa zao bila wasiwasi iweje sasa hii mifuko ikatae kuwalipa watu pesa zao wakati ni majasho ya watu.
Nawaambieni hili swala lilianza polepole kuwakumba watu wa sekta binafsi wenye mikataba mifupi, wale waliopo serikalini ambao wana mikataba ya kudumu wakajiona wapo salama kwa kuwa wanauhakika wakula mshahara hadi umri wa kustaafu na wakazoa mafao yao yote.
Lakini mda ulivyozidi kwenda kibao kikageuka tena yani sasa hata mzee mwenye miaka 55 analazimika kupewa mafao yake kwa 25% tu, mengine atapewa eti kidogo kidogo eti mpaka kifo.
Jamani huu si unyonyaji wa wazi wazi huu, hizi hela sio mali yenu, ni mali ya wafanyakazi. Mtueleze mnapozipeleka hadi hii mifuko inapumulia gesi maana hata mfanyakazi wa NSSF mwenyewe ukimwambia astaafu alafu mafao yake umpe asilimia 25 hawezi kukubali maana huo ni unyonyaji wa hali ya juu.
Wabunge wetu tulio wachagua sijui wanakazi gani jamani, Haya mambo ni mazito na ndio tuliyowatuma mkatutetee lakini kwa kujali matumbo yenu mmekaa kimya na mmethubutu kupitisha huu mswada mzito kwa wafanyakazi ambao mnajua hautowagusa nyie,