kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,991
- 17,888
Baada ya kula kipigo Israel, Yair Lapid asema, siku za Netanyahu zinahesabika
May 21, 2021 12:58 UTC
[https://media]
Yair Lapid aliyepewa jukumu la kuunda serikali ya utawala wa Kizayuni amekiri kwamba Wazayuni hawakupata matunda yoyote katika vita vya siku 11 vilivyoisha jana usiku na kusisitiza kuwa, wakati wa kuondoka Benjamin Netanyahu umewadia.
Shirika la habari la FARS limemnukuu Lapid akisema hayo leo Ijumaa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter na kuongeza kuwa, siku za waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, sasa zinahesabika.
Shirika la habari la Shahab la Palestina limefasiri baadhi ya ujumbe huo wa Twitter wa Yair Lapid, aliyepewa jukumu la kuunda serikali mpya ya utawala wa Kizayuni akisema: "Wakazi wa viongoji (vya Kizayuni) hasa wakazi wa vitongoji vilivyoko karibu na Ghaza, wamekumbwa na mvua ya makombora na maroketi na hakuna matunda yoyote yaliyopatikana."
[https://media]Yair Lapid
Amesema, kuboronga Netanyahu kumeshuhudiwa katika sehemu nyingi, kuanzia Meron (akikusudia kuangamizwa Wazayuni katika Mlima Merono huko Ghaza), hadi (katika Msikiti wa) al Aqsa na mpaka (mjini) Lod (akikusudia maandamano ya Wapalestina katika mji huo); kote huko Netanyahu ameboronga, hivyo wakati wa kuondoka umefika.
Lawama kali zimemuelemea waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu katika hali ambayo baada ya utawala wa Kizayuni kushindwa na makundi ya wanamapambano wa Palestina kwenye vita vya siku 11 vya "Saifil Quds" vilivyoisha jana usiku, televisheni ya Russia al Yaum imelinukuu gazeti la The Times of Israel likiripoti kuwa, Avigdor Lieberman, waziri wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni ambaye pia ni mkuu wa chama cha Yisrael Beiteinu na viongozi wengine mbalimbali wa utawala wa Kizayuni pamoja na wabunge wa Israel, wanaendelea kumlaumu vikali Netanyahu kwa kukubali kusimamisha vita kwa aibu na fedheha kubwa.