Baada ya kukamilika kwa gati lenye uwezo wa kuhudumia meli yenye magari 5,000: Meli kubwa zaidi itatua Dar wiki ijayo. Kushuhudiwa na Waziri

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
IMG_0329.JPG


IMG_0341.jpg

Muonekano wa Gati mpya Na. 1

Baada ya kukamilika kwa Gati Na. 1 kati ya 7 yanayojengwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwa gharama ya bilioni 33.7; ufunguzi unatarajiwa kufanyika wiki ijayo ha kuhudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe.

Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedith Kakoko, upanuzi huo wa gati lenye urefu wa mita 192 umeiongezea uwezo wa kubeba meli mbili kubwa za tani 45,000 - 60,000 kwa wakati mmoja, kutokana na kuongezwa kitako cha upana wa mita 11.5 kinachobebwa na nguzo imara za zege zilizochimbiwa mita 70 chini ya bahari.

Kukamilika kwa gati hilo kutaiwezesha Bandari kupokea magari 10,000 kwa siku, kiwango ambacho ni mara nne ya kiwango cha sasa cha magari 2,500 kwa siku na kwamba kwa mwaka kitakua cha magari 200,000 kutoka magari 90,000.

Kakoko alieleza kuwa: "Kukamilika kwa gati hili kutaleta mapinduzi makubwa kwani tunaweza kupokea meli ya magari 3,000 hadi 5,000 na ikapakuliwa kwa siku moja pekee."

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, upanuzi wa gati utakwenda sambamba na upanuzi wa lango la Bandari kwa kuongeza kina kutoka mita 10 hadi mita 16. "Nia yetu ni hadi kufikia Disemba mwakani tuwe na gati kuanzia sifuri hadi namba tatu na upanuzi wa lango uwe umekamilika ili tuweze kupokea meli za kimataifa zenye kina cha mita 15 na uwezo wa kubeba hadi makasha 6,000 kutoka meli za sasa zinazoweza kubeba makasha 2,500 tu."

IMG_0320.JPG
 
Hizo gati zikikamilika mara SGR per imekamilika! bara pah! ubungo interchange imesiha mara pah! ile Meli kubwa kule Ziwa victoria hiyo aaaaaahhhh mbona shida
Mara paa kikokotoleo chako 25% kimefutwa na kuwa kama zamani... Mara paa sheria zote kandamizi zimefyekelewa mbali!!.... Mara paa Rasimu ya Katiba ya Warioba imepitishwa kwa kishindo....
 
Pumbavu kweli kweli.

Hayo Magari 10,000 yatoke wapi wakati kodi kibao mara 2 ya bei ya kununulia gari
 
Hongera JPM
Almighty Supreme Creator chosen one walahi
 
Back
Top Bottom