Baada ya Kujifanya ' anakosoa ' sasa Mwandishi huyu ' amejirudi ' kwa kuwa ' typical sycophant ' ili Nduguye amteue Kisiwani Puerto Rico

Kumbe Mr. Hungry nae ni ' Jasiri ' Mkuu? Nilikuwa silijui hilo na itanibidi sasa niende BAKITA ili wakanipe ufafanuzi ' Kuntu ' wa neno ' Jasiri ' lako. Na kuhusu kutumia jina halisi nimeshasema Siku nyingi sana hapa ' Jamvini ' kuwa ' Kiuhalisia ' naitwa Mr. Kalemera Rwigyema Mazimpaka ila ' Kiubatizo ' naitwa GENTAMYCINE ANTIBIOTIQUE.

Nadhani nimekupa ufafanuzi uliokuwa unauhitaji.
Nimekusoma kalamera. Si lazima tufanane kwenye maana ya neno jasiri Ila kwa tafsiri yangu mm huyu mtu unayemuongelea ni jasiri. Ukumbuke pia ujasiri una mipaka. Ndo maana na sisi pamoja na ujasiri wetu wa kupambana na ushoga, waziri alimkana makonda na operesheni yake.
 
Mkuu mbona huku Kisiwani Puerto Rico nilipo Mimi hatuna Mtu aitwae Makonda na wala hapajawahi kuwa na ' Oparesheni ' ya aina yoyote ile? Samahani unazungumzia Puerto Rico au nchi nyingine?
 
Mbona Mr. Hungry hayuko hivyo!! Ila kila mtu na uoni wake. Wengine wana kile madkatari wanachokiita colour blindness i.e wakiona njano husema dhahabu
 
Mr Hungry ni mwandishi mwerevu sana na huwa makini kwa anachochangia iwe kwa kusifia au kukosoa hufanya kwa tahadhari kubwa.
 
Naona Waandishi wa Kweli, Wakosoaji na tusiokuwa Wanafiki na ' typical flatterers ' kama Mr. Hungry wa hapa Kisiwani Puerto Rico tunazidi tu Kukimbiwa kila Uchao. Tena bora Mwenzetu alikuwa na Ofisi yake na amepanga Floor nzima japo sasa amerejea ' Stoo ' Kujihifadhi kwa muda huku akisubiri ' Uteuzi ' ila Mimi GENTAMYCINE ndiyo hata pa Kulala tu sina na maisha yangu yenyewe nayo ni ya ' Kuunga Unga ' tu kama Mabehewa mabovu ya TRL ya hapa Kisiwani Puerto Rico. Sijui na Mimi nianze pia Kujipendekeza na Kujikomba masikini ya Mungu kwani kama Nyangumi kanyoosha mikono yake Mimi Samaki Tasi ni nani nami nisitii bila shuruti?
Sasa hivi kila nyuzi akiitoa lazima alambe sakafu za magogoni njaa imemsambaratisha sana
Endeleeni kumuombea Pascal hali ni tete hadi kaamua kula matapishi
 
Nimegundua kitu kimoja hapa Tanzania. Watu wengi hawapendi kufanya kazi na ni wazembe hata kwa kufikiri, hawataki kuambiwa what to do ili nchi isonge mbele. Wanapenda sana kufuata mkumbo bila hata kufikiri pia, wanshabikia sana ujinga na vitu visivyo na maana kwao. Kwa kweli Mkapa anastahili pongezi ya kutukana watanzania kila kukicha.
 
Naamini 100% Unamzungumzia mtaalamu Pascal Mayalla.Ngoja nikwambie,huyo unayemzungumzia ni moja ya great thinkers humu jukwaani na Tanzania kwa ujumla,sina shaka kabisa na uwezo wake.

Hizo hisia zako kwamba anawinda cheo kutokana na posts zake nikwambie tu umekosea sana na pengine huzielewi mada na uandishi wake.....huwa unajinadi kwamba wewe ni kichwa na wengine ni mapopoma...lakini kwavile umeshindwa kuelewa mada na uandishi wa Ndugu Pascal basis hauna tofauti na wale unaowaita mapopoma.
 
Kama ni P, he is very right!! anasoma nyakati, anang'ata na kupuliza kutokana na mazingira ya sasa. Kifupi anakula na kipofu. Mbona wewe umeng'anga'na visiwa vya puerto with fake ID, kwanini usiwe verified user then umchane live Magu uone moto wake! Sisi wenye ma fake ID inatupasa tuwapongeze wenzetu wanaojikakamua katika mazingira haya magumu.
 
Ukiwa mshabiki wa kisiasa huwezi muelewa Mr Hungry. Mfano Mr Kameat Shove alipokuwa kwenye kambi ilyokaribu na border ya Puerto Rico ukanda wa magharibi karibu na ziwa lenye kina kirefu alikuwa ni professor ila alipohamia kule kwenye nchi yenye jina kama zinapotoka ndege Seattle karibu na ziwa pana zaidi akwa ni leprofesseri. Pia hata Mr GreyHair na Mr Yule anaye tawala karibu na kambi ya urekebishaji karibu na eneo Maarufu la Kuuza Gongo la Moto.
 
Hatimaye yule Mwandishi wa Habari Mr. Hungry kutoka Kisiwani Puerto Rico ambaye mara nyingi alikuwa akionyesha yupo sana katika ' Ukosoaji ' wa Rais na Serikali yake hapa Kisiwani baada ya Yeye pia kuona hali yake ya Uchumi pamoja na Media yake ameamua sasa ' Kujirudi ' na Kuanza ' Kujikomba ' kwa Kuandika ' Makala ' za kuwa upande ule ambao mara nyingi alikuwa akiupinga japo wenye akili tulijua mapema kuwa nini alikuwa anakitafuta.

Ni matumaini yangu makubwa sana kuwa kuanzia sasa hasa baada ya Kuziona ' Makala ' zake mbili tatu mahala fulani huku nikiamini kuwa zingine kama hizi nyingi zipo njiani zinakuja basi si ajabu kama Rais wa Kisiwa cha Puerto Rico atafanya ' uteuzi ' wowote hivi karibuni nina uhakika safari hii hatomsahau ' Wa Nyumbani ' Kwake Mr. Hungry ambaye kutokana na Uchumi wa Puerto Rico kuwa mbaya hata Yeye pia ' ameathirika ' vilivyo kupelekea ' Kuhamahama ' Ofisi kama Ndege anayetafuta malisho ili tu kuendana na Kasi.

Laiti kama Waandishi wa Habari wa hapa Puerto Rico wangekuwa hawapendi Kujipendekeza na Kujikomba kama Wenzao wa Tanzania nina uhakika Puerto Rico ingekuwa na ' a very strong Media ' ila hali ni tofauti mno hadi nimekuwa nikitamani hata Siku moja tu Waandishi wa Habari makini, weledi, wasio na njaa wala wasiopelekeshwa wa Tanzania waje tu kufanya ' Ziara ' hapa ili ' wawaambukize ' huo ' Ujasiri ' wao hawa wa hapa wakiongozwa na Mr. Hungry.

Nawasilisha.
Njaa unaitwa huku Pascal Mayalla
 
Mkuu naona unajaribu kutumia technic za Pascal Mayalla... unajitahidi ila unajulikana mapema unakoelekea
 
Back
Top Bottom