Baada ya kujaziwa matukio ya Makinikia, IPTL, wananchi, wabunge, hawajaijadili bajeti!

chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,678
2,000
Ninadhani mtego huu umenasa wengi na umetutoa kwenye hoja,mpaka nawaza,je kwa nini matukio yamewekwa kwa wing I kipindi cha bajeti?

Kuna mhimili unaficha jinsi ulivyokwama kutekeleza bajeti iliyopita hivyo umeamua kutengeneza matukio kuhamisha watu katika mijadala? Tunajua bajeti imetekelezwa kwa asilimia 38,chini ya nusu kabisa na mwaka ujao itakuwa chini zaidi

Ukiangalia bunge,wabunge hawajadili bajeti, "nampongeza fulani". " nampongeza fulani" hatujiulizi maswali ya kibajeti na kiuchumi,mtu analipwa milioni 12 kwenda kuongeza!

Wapinzani pia,kiuhakika hawajafanikiwa kuwaeleza wananchi kiuhalisia mapungufu yaliyokuwepo,yaliyopo na nini maoni yao! Hawana mpango mkakati wowote hata ya kuitisha makongamano,wapo tu,wapo wapo wanaingia na kutoka bungeni,wanaelea angani.

Ila natabiri kwamba bajeti hii italeta mzozo mkubwa sana ndani ya miezi mitatu,

Wananchi tuanzishe bunge letu tujadili hii bajeti

N.B

Ukiona serikali ina makelele sana,ujue imekwama,mambo yamegoma,solution ni kuleta confusion,misinformation and disinformation
 
Laface77

JF-Expert Member
Jul 9, 2008
2,116
2,000
Another silly session kwa ajili ya kumuambia mtukufu mapambio na kumpongeza!
 
MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
3,774
2,000
Kama kawaida, si muda unasinga mbele na tayari watz wameshasema Huyu ndiye masia tuliyemngojea.
Yes another year is lost na ni business as usual! Who cares maana watu wanakesha wakiunda propaganda ili mambo ya msingi yasisikike. Basi hii ndio TZ.
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,283
2,000
Kibaya zaidi wapinzani wameingia ktk mtego huu wa kugombea kick na "serekale". Wao baada ya kujaza mabandiko na video clips nyingi za kuijadili bajeti wao wanakimbilia kuzima kick za huyu mheshimiwa "JEIPIIEEMUU". Mfano fuatilia jinsi "TUNDU" anavyokesha kutafuta kick kwa kujaribu kuzima kiki za baba J.
Angetafuta kick kwa kupitia kuichambua bajeti na hiyo ingeleta faida na unafuu wa maisha moja kwa moja kwa wapiga kura wake kule kijijini na Tanzania yote kiujumla.
 
BONGE BONGE

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
3,708
2,000
Ninadhani mtego huu umenasa wengi na umetutoa kwenye hoja,mpaka nawaza,je kwa nini matukio yamewekwa kwa wing I kipindi cha bajeti?

Kuna mhimili unaficha jinsi ulivyokwama kutekeleza bajeti iliyopita hivyo umeamua kutengeneza matukio kuhamisha watu katika mijadala? Tunajua bajeti imetekelezwa kwa asilimia 38,chini ya nusu kabisa na mwaka ujao itakuwa chini zaidi

Ukiangalia bunge,wabunge hawajadili bajeti, "nampongeza fulani". " nampongeza fulani" hatujiulizi maswali ya kibajeti na kiuchumi,mtu analipwa milioni 12 kwenda kuongeza!

Wapinzani pia,kiuhakika hawajafanikiwa kuwaeleza wananchi kiuhalisia mapungufu yaliyokuwepo,yaliyopo na nini maoni yao! Hawana mpango mkakati wowote hata ya kuitisha makongamano,wapo tu,wapo wapo wanaingia na kutoka bungeni,wanaelea angani.

Ila natabiri kwamba bajeti hii italeta mzozo mkubwa sana ndani ya miezi mitatu,

Wananchi tuanzishe bunge letu tujadili hii bajeti

N.B

Ukiona serikali ina makelele sana,ujue imekwama,mambo yamegoma,solution ni kuleta confusion,misinformation and disinformation

20dbf84eb36527ae6dcd74e2103ed6c1.jpg
 
chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,678
2,000
Kama kawaida, si muda unasinga mbele na tayari watz wameshasema Huyu ndiye masia tuliyemngojea.
Yes another year is lost na ni business as usual! Who cares maana watu wanakesha wakiunda propaganda ili mambo ya msingi yasisikike. Basi hii ndio TZ.
Safari hii ziliundwa propaganda kwa mpangilio kabisa,Siku wapinzani wanasoma bajeti,muda huo huo serikali inasoma ripoti ya pili ya makinikia,ripoti ya kwanza pia ilitolewa wakati muhimu kibunge,sasa hivi kwenye majumuisho ya bajeti ya nchi ,ameibuliwa singasinga na escrow,maana kipindi hiki ndio kigumu kwa bajeti

Watu hawana dawa,wanavurugwa na habari za kijinga,nchi imejaa shida za kiuchumi kila kona,

Ila mwisho wa Siku wajue wananchi hawatashiba propaganda,njaa zitawauma tuuu,hapo ndipo watakaa chini kujibu maswali
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
33,249
2,000
Hebu Chadema tuambieni ukweli mbona KUB hayupo ukumbini kupiga kura kwenye bajeti?

Kwa nini hamjaweka utaratabu wa kumpigia kura?
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,219
2,000
Hebu Chadema tuambieni ukweli mbona KUB hayupo ukumbini kupiga kura kwenye bajeti?

Kwa nini hamjaweka utaratabu wa kumpigia kura?
Kupiga kura bajeti anatoroka lakini kupokea ruzuku na posho anakuwa wa kwanza kuidai hajui kuwa ruzuku na posho ziko ndani ya bajeti kuwa anatakiwa awemo hadi mwisho? Ikishapita anakuwa wa kwanza kutaka ruzuku na posho iliyopitishwa kwenye bajeti alipwe posho na ruzuku iingizwe chap chap akaunti za chadema ambamo yeye ndie mtia sahihi kuzitoa. Looo baniani bajeti simpendi lakini kiatu chake ruzuku alichovaa bajeti nakipenda sana. Mmmmmm
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,851
2,000
Dawa yao ni kurekebisha tu sheria,asiepitisha bajeti chama chake hakipati ruzuku,bajeti wanapinga lakini posho na ruzuku ndio wa kwanza kudai
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,219
2,000
Kuna mbunge wa upinzani kapitisha bajet kwa kusema NDIO naombeni nimjue,kashangiliwa sana
Unafiki mtupu hawapigi lakini ikishapita wa kwanza kupiga yowe kuwa tulipwe posho chap chap kwani zilishapita kwenye bajeti. Na kelele kibao ohh kwa nini wizara inachelesha pesa za mfuko wa Jimbo na pesa za miradi jimboni kwangu wakati ilishapitishwa kwenye bajeti ambayo wao walitoroka kinafiki wakati wanaelewa fika kuwa bajeti imebeba hadi pesa za miradi Ya maendeleo majimboni mwao. Upinzani Tanzania ni zero.
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,149
2,000
Kuna mbunge wa upinzani kapitisha bajet kwa kusema NDIO naombeni nimjue,kashangiliwa sana
Yule wa kwanza alirekebisha akafuta ndio ikawa hapana .........Ila Magdalena Sakaya Kaunga mkono bajeti kwa ndio kubwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom