Baada ya kuitwa kodi ya majengo nafikiri ni bora iitwe kodi ya kujenga miundombinu ya mitaa

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
2,674
3,053
Kama wasomi wa nchii hi wamekaa na wakaona kodi za majengo sasa zilipwe na wapangaji kila wanaponunua umeme naona hi kodi ibadilishwe jina na ifanye kazi ya kujenga miundo mbinu ya mitaa ambayo hao wapangaji wanaolipa hii kodi wanaishi

Maana kuna majumba mengi wenyenyumba wamewaachia wapangaji wao kila mwezi wanachukua kodo zao tu katika vyumba au fremu za biashara tena unakuta kila mmpangaji amewekewa mita yake ya LUKU

Yani mpangaji alipe kodi ya pango kwa mwenye nyumba pia amlipie mwenye nyumba kodi ya jengo TRA kupitia LUKU hi sio sawa kabisa

Ni bora hi kodi ibadilishwe jina pamoja na matumizi yake hayo makusanyo yatumike kurekebisha miundo mbinu ya mitaa husika kulingana na makusanyo yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili hata Mimi nilikuwa nalifikilia Sana kuwa itakuwaje kwa wapangaji walipe Kodi ya majengo kupitia umeme wakati wao wanalipa Kodi ya nyumba. Hapa itabidi waziri wa fedha aje aifafanue zaidi kwenye issue ya wapangaji.
 
kodi ya majengo lazima itathiminiwe upya.
TRA hawajafanya utafiti mzuri kwa nani alipe kiasi gani na kwa njia gani.
unakuta mtu anamiliki nyumba ya kawaida hu huko pembezoni mwa Jiji lkn unakuta kodi iliyo pendekezwa ilo juu.
unakuta nyumba haina hati, jakuna namba za nyumba sasa unakusanyaje kodi?!
wekeni miundombinu kwanza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom