Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,981
- 45,902
Juhudi za Mh. Rais za kuhakikisha kua makandokando yote yaliyokua kizuizi cha kupeleka maendeleo kwa wananchi pamoja na huduma bora zikiwa zinaendelea na kuanza kuonekana matunda yake sasa macho na masikio ya kila mtu ni kuona namna juhudi hizi zitakavyokuja baada ya yeye kuachiwa kiti cha uenyekiti wa chama cha mapinduzi hapo baadae.
Kumekua na malalamiko ya chini chini na ya wazi kwa wapenzi wakereketwa, wafurukutwa mashabiki kindaki ndaki, na wananchama kua chama kimepotez misingi yake ya waanzilishi jambo ambalo limewafanya baadhi kukata tamaa, kuhama chama, kubaki kwa shingo upande na wengine kudiriki hata kukisaliti kwa kuchoshwa na baadhi ya mambo kama wanavyoona wahusika.
Ili kasi katika serikali ishike moto zaidi juhudi za wazi kabisa zinahitaika kuhakikisha kua chama nacho kinaendana na serikali iliyopo madarakani hivyo kama kuna majipu basi hakuna namna nyingine zaidi ya kuyatumbua.
Ni kina nani watatumbuliwa kwa faida ya chama, na kina nani watasalimika?
Ni jambo la kusubiri na kuona.