Baada ya kuibiwa simu nimefuata process zote kuipata ni shida

pilau

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
1,593
443
Pamoja na matangazo mamlaka ya mawasiliano wanayoyatoa nimeibiwa simu, nimeripoti polisi (RB) ninayo, risiti ya kununulia yenye imei namba ninayo, box la simu yenyewe ninalo ..... Tatizo wahusika wanaendelea kunipiga kalenda .... Nifanye nini zaidi ya kufuatilia kunakohusika au wanataka kitu kidogo? Waungwana wazoefu nipeni ishauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mamlaka ya mawasiliano wanatuambia process za kufuata baada ya kuibiwa simu nimefuata zote wahusika wananiambia subiri utaitwa na miezi inakatika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eneo ninaloishi kuna mzungu mmoja aliibiwa simu na vibaka. Akaenda polisi muda huo huo kutoa taarifa. Ndani ya masaa mawili yule mwizi alikutwa na simu mafichoni....
HAPO HUNA CHAKO TENA MKUU nunua ingine tu, hawa polisi wanaangalia sura.
 
Nenda kwa network provider wako kawaone It kama ni voda au tigo watakusaidia kuliko huko unakoenda bure bure husaidiwi

Kikubwa linganisha bei ya hiyo simu yako na utakachotoa ili uipate

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom