Baada ya kugundua jinsi Kijana alivyowafanyia wazazi wake, nimelia sana. Kwanini lakini mtu afanye hivi?

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Huyu ni kijana mdogo dereva wetu hapa ofisini. of course yeye ndo huwa ananiendesha maana alipata mafunzo ya udereva marekani na kuwa anaendesha mabalozi wa marekani n.k sasa tupo naye kazini mwezi wa tano sasa. juzi akawa anasema kuwa baba yake anaumwa mafua makali na kikohozi nikamuuliza amempeleka hospitali akajibu ndiyo. baada ya siku tatu akanambia bado hali ya baba yake inasua sua. nikamuuliza amempeleka hospital? akajibu ndiyo. nikamuuliza daktari wa wazazi wake anasemaje? nlishangaa anasema hawana daktari. yaani ameshindwa kuwawekea wazazi wake daktari? nlishtuka sana. kumuuliza mwanasheria wa familia. naye hana.nikamuuliza mchungaji/padre au sheikh wa familia. akajibu hana....nikaona tayari hapa kuna shida.jamaa hayupo serious kabisa na maisha ya wazazi wake.nlitokwa na machozi.nliumia sana.nililia...sikuamini.

Kwenda kufuatilia kumbe hajampeleka baba yake hospital kampeleka sehemu moja wanaita Amana... ipo Ilala. nikamwambia Hospital si ni Aga Khan au Muhimbili? hakuelewa kabisa. ndo kumchukua mzazi wake apelekwe Hospital Aga Khan. cha kushangaza yaani pamoja na kulelewa na wazazi wake mpaka umri huo anawaacha waendeshe Harrier. jamani haya maisha mzazi unashindwa mnunulia gari unamwacha aendeshe Harrier? kweli? hizi Toyota Harrier hivi hata upande wake wa safety ukoje? naona kama ni nyepesi sana.

Ndo kumwambia dereva wangu aende wachukua kwenye GMC yangu awapeleke hospital wote. nashukuru walifurahi sana kupanda gari.miaka yote walikuwa hawajawahi panda gari. wanatumia hizi Toyota na Nissan au Subaru .wazee wanaishi mazingira magumu huko sinza. sinza ni sehemu ya watu wa kipato cha chini sana...nikamshauri huyu bwana mdogo awahamishie angalau Mikocheni au Mbezi Beach maana nilimwambia kuna apartments za bei rahisi huku oysterbay.. tsh 10,000,000 kwa mwezi akashtuka kidogo ameze ulimi. anadai eti ni nyingi kwake... jamani wazazi tuwapende na kuwajali wanapofikia umri huu wa miaka 50 plus wanunulie gari kama hawana. wawekee daktari wao.mwanasheria,wafanyakazi,dereva n.k waache tu wafurahie maisha wasiwe na msongo wa mawazo. kwa mwaka angalau hakikisha mara tatu wanaenda tembelea mbuga,nchi nyingine n.k wapende wazazi wako hapa duniani usisubiri wafe uweke picha zao za kuwataka wa rest in peace. let them live in peace right now.

Jamaa nimempa somo kubwa sana. baba yake sasa amepona ananishukuru sana. nimemwambia jamaa ajitahidi hata kwa mwezi awe anatuma tsh 3,000,000 za matumizi kama hali yake ni ngumu sana. wata enjoy na kumbariki. sisi huwa tunawanunulia zawadi wazee wetu mpaka nao wanaenda kugawa kwa marais,mawaziri au wafanyabiashara wakubwa wakubwa.wala hatuudhiki kwa mambo hayo. maana nlishangaa kuiona saa flani ambayo nilinunua Uswisi akiwa amevaa Waziri mmoja hapa Tanzania. nlishtuka sana na kumpigia simu mzee akasema huyo waziri alienda Canada wakaonana akaona ile saa akaipenda sana. alipoulizia bei akatajiwa alipatwa na kigugumizi ghafla na kutoa gesi kwa mshtuko. anasema ni kama angefanya serving ya mishahara na malupulupu yake ndo aje apate hiyo saa miaka ijayo. mzee akavua akampa. huyo waziri kila siku huwa anapiga simu kwa mzee kumshukuru. mzee alishamkataza kuwa ni mambo ya kawaida asijali but haamini kuwa ana saa kama ile. mzee kaamua ku mblock maana ni usumbufu sasa.

Anyway..tuwapende wazazi wetu tusisubiri mpaka wafe na kuanza kuwapost.
 
huyu ni kijana mdogo dereva wetu hapa ofisini. of course yeye ndo huwa ananiendesha maana alipata mafunzo ya udereva marekani na kuwa anaendesha mabalozi wa marekani n.k sasa tupo naye kazini mwezi wa tano sasa. juzi akawa anasema kuwa baba yake anaumwa mafua makali na kikohozi nikamuuliza amempeleka hospitali akajibu ndiyo. baada ya siku tatu akanambia bado hali ya baba yake inasua sua. nikamuuliza amempeleka hospital? akajibu ndiyo. nikamuuliza daktari wa wazazi wake anasemaje? nlishangaa anasema hawana daktari. yaani ameshindwa kuwawekea wazazi wake daktari? nlishtuka sana. kumuuliza mwanasheria wa familia. naye hana.nikamuuliza mchungaji/padre au sheikh wa familia. akajibu hana....nikaona tayari hapa kuna shida.jamaa hayupo serious kabisa na maisha ya wazazi wake.nlitokwa na machozi.nliumia sana.nililia...sikuamini.

kwenda kufuatilia kumbe hajampeleka baba yake hospital kampeleka sehemu moja wanaita Amana... ipo Ilala. nikamwambia Hospital si ni Aga Khan au Muhimbili? hakuelewa kabisa. ndo kumchukua mzazi wake apelekwe Hospital Aga Khan. cha kushangaza yaani pamoja na kulelewa na wazazi wake mpaka umri huo anawaacha waendeshe Harrier. jamani haya maisha mzazi unashindwa mnunulia gari unamwacha aendeshe Harrier? kweli? hizi Toyota Harrier hivi hata upande wake wa safety ukoje? naona kama ni nyepesi sana.

ndo kumwambia dereva wangu aende wachukua kwenye GMC yangu awapeleke hospital wote. nashukuru walifurahi sana kupanda gari.miaka yote walikuwa hawajawahi panda gari. wanatumia hizi Toyota na Nissan au Subaru .wazee wanaishi mazingira magumu huko sinza. sinza ni sehemu ya watu wa kipato cha chini sana...nikamshauri huyu bwana mdogo awahamishie angalau Mikocheni au Mbezi Beach maana nilimwambia kuna apartments za bei rahisi huku oysterbay.. tsh 10,000,000 kwa mwezi akashtuka kidogo ameze ulimi. anadai eti ni nyingi kwake... jamani wazazi tuwapende na kuwajali wanapofikia umri huu wa miaka 50 plus wanunulie gari kama hawana. wawekee daktari wao.mwanasheria,wafanyakazi,dereva n.k waache tu wafurahie maisha wasiwe na msongo wa mawazo. kwa mwaka angalau hakikisha mara tatu wanaenda tembelea mbuga,nchi nyingine n.k wapende wazazi wako hapa duniani usisubiri wafe uweke picha zao za kuwataka wa rest in peace. let them live in peace right now.

jamaa nimempa somo kubwa sana. baba yake sasa amepona ananishukuru sana. nimemwambia jamaa ajitahidi hata kwa mwezi awe anatuma tsh 3,000,000 za matumizi kama hali yake ni ngumu sana. wata enjoy na kumbariki. sisi huwa tunawanunulia zawadi wazee wetu mpaka nao wanaenda kugawa kwa marais,mawaziri au wafanyabiashara wakubwa wakubwa.wala hatuudhiki kwa mambo hayo. maana nlishangaa kuiona saa flani ambayo nilinunua Uswisi akiwa amevaa Waziri mmoja hapa Tanzania. nlishtuka sana na kumpigia simu mzee akasema huyo waziri alienda Canada wakaonana akaona ile saa akaipenda sana. alipoulizia bei akatajiwa alipatwa na kigugumizi ghafla na kutoa gesi kwa mshtuko. anasema ni kama angefanya serving ya mishahara na malupulupu yake ndo aje apate hiyo saa miaka ijayo. mzee akavua akampa. huyo waziri kila siku huwa anapiga simu kwa mzee kumshukuru. mzee alishamkataza kuwa ni mambo ya kawaida asijali but haamini kuwa ana saa kama ile. mzee kaamua ku mblock maana ni usumbufu sasa.

anyway..tuwapende wazazi wetu tusisubir mpaka wafe na kuanza kuwapost.
Daah nmecheka sana JF kuna watu kwa kujikweza mpo vzuri
 
Back
Top Bottom