Baada ya kufungiwa Sumry watumia jina la Mbeya express

Mlendamboga

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
664
334
Kampuni ya usafirishaji ya Sumry imeifanyia Sumatra Mchezo wa kuigiza nakufanikiwa baada ya kusajiri magari manne ya injini nyuma kwa jina la Kampuni nyingine ya MBEYA express ambayo hufanya safari zake kati ya Mbeya Na sumbawanga.
Taarifa za kiintelijensia tulizonazo, hatua hiyo inalenga kutosimamisha Biashara ya usafirishaji baada ya kufungiwa Kwa mabasi yake Kwa barabara ya Mbeya hadi Dar kutokana Na matukioya ajali za mfululizo.
 
Mkuu, hayo mabasi yamebadilishwa namba kabla hayajasajiliwa au ni mapya kabisa? Manake kama ni yale yale na namba zile zile sumatra si wana rekodi zake?
 
Sumry alikuwa anamiliki kampuni mbili, sumry high class na hiyo Mbeya express. Hiyo Mbeya express wanaimiliki muda mrefu, hata sumatra watakuwa wanajua mmiliki wa sumry na mbeya express ni mmoja.
 
Ooh shukrani mdau Kwa kunipa PICHA kuwa wanakampuni mbili manake kila kitu ni Sumry tupu tangu watumishi hadi Rangi za GARI pamoja na parking
 
Ooh shukrani mdau Kwa kunipa PICHA kuwa wanakampuni mbili manake kila kitu ni Sumry tupu tangu watumishi hadi Rangi za GARI pamoja na parking
Ni kweli Sumry aliinunua Mby express kutoka kwa mmiliki wake wa awali na hakuyabadili jina.
 
hapo ndipo utakapoona jinsi wafanyabiashara walivyo na nguvu kuiliko serikali yetu, kama ni kampuni yake na hiyo ya mbeya expres safari za dar-mbeya zifungiwe tu
 
huo mchezo kampuni nyingi wanao , kampuni moja lkn inasajili majina
tofauti. mfano kampuni ya upendo, hao hao ni budget, mafinga express.
siju kwanini wanaruhusu hicho kitu.
 
Ooh shukrani mdau Kwa kunipa PICHA kuwa wanakampuni mbili manake kila kitu ni Sumry tupu tangu watumishi hadi Rangi za GARI pamoja na parking
Hapo zamani za kale kulikuwa na mabasi yanaitwa Nchambis ambayo yalikubuhu kwa ajali za mara kwa mara zilizosababisha vifo vya mamia,yalipoandamwa na kutishiwa kufungiwa na pia kususiwa na abiria,walibadili na kuyaita MOMBASA RAHA, serikali ikasahau ya Nchambi na abiria waliokuwa wakisusia Nchambi wakaanza kupanda Mombasa raha kwa bidii,Mchezo ni ule ule kwa sumry:OLD WINE IN A NEW BOTTLE
 
Mnakumbuka No challenge? Baada ya kupata ajali kubwa jiran na Muheza ktk miaka ya 90 walibadili na kujiita Tashrif. Hawa wafanyabiashara ndo zao!
 
Haukumbuki enzi za Air Msae, kwasasa inaitwa Metro. Uhuni mtupu.
 
naona wanaitangangaza kampuni yao mpya ya Mbeya Exp. kuna basi jipya limetanguliwa na gari ya matangazo
 
Back
Top Bottom