Baada ya kufungiwa misimu miwili kushiriki UEFA, huenda Manchester City ikapunguziwa alama za Ligi na kushushwa daraja

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,219
24,079
Timu ya Manchester City imefungiwa kushiriki mashindano ya European Champion League na Europa League katika misimu inayokuja ya mwaka 2020 / 2021 na 2021/ 2022.

Hii inatokana na timu hiyo tajiri ya Uingereza kukiuka kanuni za matumizi ya kiwango cha pesa ktk kusajili wachezaji.

Timu zote ulaya zimewekewa kiwango cha juu wanachoruhusiwa kutumia ktk kusajili ili kuzipa nafasi sawa timu zisizo tajiri kuweza kushindana kwa usawa ingawa hazina utajiri wa wa kutisha.

Timu hiyo ya Manchester City pia imepigwa faini ya Euro 20,000,000 kutokana na sakata hilo.

Vigogo wafadhili wa Manchester City waliichukua timu hiyo na kuingiza kiasi kikubwa cha fedha ktk bajeti ya timu ili iweze kushindana na klabu zingine kubwa ambazo zilikuwa zinatamba kwa kuchukua ubingwa wa European Champion League.

Hivyo kwa msimu huu 2019 / 2020 Manchester City itaweza kushiriki ktk mashindano ya European Champion League maana adhabu imetoka wakati ligi ya huko England ilishaanza na imefika katikati ya michuano ya England Premier League EPL.

UPDATE
Manchester City inaweza kupunguziwa alama kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kama sehemu ya adhabu ya uvunjaji mkubwa wa Kanuni za Financial Fair Play

Klabu hiyo imefungiwa kwa misimu miwili ijayo kushiriki mashindano yanayoandaliwa na UEFA na kupigwa faini ya takriban Tsh. Bilioni 75, na kwa kupatikana kwake na hatia ya kosa hilo inaashiria pia inaweza kuwa imevunja Kanuni za ndani za Ligi

Suala hilo linakuja kwa sababu klabu yoyote lazima itoe taarifa za kweli ili kupata leseni ya Ligi Kuu, na taarifa hizo zinalazimika kuwa sawa na zile zitolewazo katika Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA)

Aidha, itakumbukwa kuwa hivi karibuni Kamati ya Ligi Kuu England ilibadilisha Miongozo yake ili Klabu yoyote inayokutwa na hatia katika kosa kama hilo lazima ishushwe daraja

Historia ya Kashfa ya Man City:
 
EQwcfTYWoAA4OOG.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wataachiliwa kama walivyoachiliwa Chelsea kwenye usajili, wazungu hawaamini kwenye maadhabu makubwa
 
Iwapo epl ikiisha hiv team zipi zitaenda uefa
1.liverpool
2.Man city
3.leistercity
4.Tottenham
5.Chelsea
 
February 14, 2020.

Timu ya Manchester City imefungiwa kushiriki mashindano ya European Champion League na Europa League katika misimu inayokuja ya mwaka 2020 / 2021 na 2021/ 2022.

Hii inatokana na timu hiyo tajiri ya Uingereza kukiuka kanuni za matumizi ya kiwango cha pesa ktk kusajili wachezaji.

Timu zote ulaya zimewekewa kiwango cha juu wanachoruhusiwa kutumia ktk kusajili ili kuzipa nafasi sawa timu zisizo tajiri kuweza kushindana kwa usawa ingawa hazina utajiri wa wa kutisha.

Timu hiyo ya Manchester City pia imepigwa faini ya Euro 20,000,000 kutokana na sakata hilo.

Vigogo wafadhili wa Manchester City waliichukua timu hiyo na kuingiza kiasi kikubwa cha fedha ktk bajeti ya timu ili iweze kushindana na klabu zingine kubwa ambazo zilikuwa zinatamba kwa kuchukua ubingwa wa European Champion League.

Hivyo kwa msimu huu 2019 / 2020 Manchester City itaweza kushiriki ktk mashindano ya European Champion League maana adhabu imetoka wakati ligi ya huko England ilishaanza na imefika katikati ya michuano ya England Premier League EPL.

Historia ya Kashfa ya Man City:
Hata hivyo Manchester city imekuwa haifanyi vizur katka michezo ya UEFA Licha ya kutumia kiasi kikubwa cha pesa (Over budget)
Akomae tu na Lig ndiyo anaweza!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom