Baada ya kufungiwa, Gazeti la Mawio kwenda Mahakamani

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,245
2,000
Uongozi wa gazeti la MAWIO umeapa kwenda mahakamani kupinga uamuzi wa serikali kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa kipindi cha miezi 24.

Uamuzi wa kulifungia gazeti hilo ulitangazwa na serikali kupiti Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo sababu iliyotajwa ni gazeti hilo kukiuka maagizo ya serikali ya kutowahusisha marais wastaafu Mzee Mkapa na Dkt Kikwete katika ripoti za uchunguzi wa mchanga wa madini.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Victoria Media Services Ltd ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la MAWIO, Simon Martha Mkina, aliliambia The Citizen kuwa, amuzi huo si wa haki na utapingwa mahakamani.

“Bodi itakutakana kujadili uamuzi huo kama jambo la dharura, lakini tunachoweza kukwambia kwa sasa, tutakwenda mahakamani,” alisema Mkina.

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Dkt Mwakyembe iliyotolewa na Idara ya Habari (MAELEZO), Waziri alinukuliwa akisema, “Sina budi kulifungia gazeti lako, na kukutaka usitishe kuchapisha nakala ngumu au ya mtandaoni katika kipindi cha muda wa miezi ishirini na nne (24) tangu tarehe ya barua hii, kwa mamlaka niliyopewa chini ya Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016 kifungu cha 59.”

Gazeti hilo liliandika habari iliyokuwa na ujumbe wa jumla kuwa, marais hao wamelisababishia taifa hasara kubwa sana kutokana na usafirishaji wa mchanga nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 19.

 

kilambalambila

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
8,750
2,000
Magazeti ya kijinga yanayoandika taarifa kwa sifa ili yapate popularity yafungiwe tu tena ikiwezekana miaka mitano kabisa au maisha, whichever comes last
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
8,736
2,000
..ambapo sababu iliyotajwa ni gazeti hilo kukiuka maagizo ya serikali ya kutowahusisha marais wastaafu Mzee Mkapa na Dkt Kikwete katika ripoti za uchunguzi wa mchanga..
Sababu dhaifu kabisa kuwahi kutolewa. Kama Mahakama itaacha uboya na woga, MAWIO watashinda kesi hii asubuhi na mapema
 
  • Thanks
Reactions: MTK

forest zone

JF-Expert Member
Jun 10, 2017
253
250
Maajabu ya tanzania haya. Hatujapata mzalendo halisi wakuongoza hili taifa. Kesi ya ngedere ummbebeshe nyani?
 

chabusalu

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
7,311
2,000
Magazeti ya kijinga yanayoandika taarifa kwa sifa ili yapate popularity yafungiwe tu tena ikiwezekana miaka mitano kabisa au maisha, whichever comes last
Kwa akili yako Mawio walikuwa wanatafuta "popularity" walipoandika hiyo habari? Kwamba hawakuwa "popular" kabla ya kuandika hiyo habari, siyo? Halafu aliyeunda Kamati ikamkabidhi ripoti ambayo technically inawahusisha hao watu waliotajwa na Mawio yeye atakuwa alikuwa anatafuta nini?
 

Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,249
2,000
Wasiposhinda hiyo kesi nitajua hadi majaji wameanza kumuogopa baba bashite.
Ni kweli kabisa maana ni wai kuwa MAWIO hawana kosa lolote kando ya kuuambia umma wa watanania kuwa waliotajwa kwenye report ya pili ni waliokuwa wanatumwa na maraisi JHMK na BWM. Kwa hiyo ilikuwa sahihi kwa picha zao kuonekana front page!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom