Baada ya Kufanyiwa LEEP, ameingia Hedhi,ila Damu inatoka nyingi sana.

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
17,284
10,665
Kafanyiwa LEEP lakini Sasa alipoingia hedhi damu inatoka nyingi na siku zinapita tu hedhi haikomi.
Leo anaenda tena Kwa Daktari wake,je humu kuna wajuzi wa chochote kuhusu hii condition iliyojitokeza. Kwa wale wenye experience na hii Operesheni hii condition ni normal au lah?
 
Baada ya LEEP Hiyo Ni Menstruation Ya Ngap???
Hiyo Excision LEEP Alifanyiwa Lin??
Je anatumia Contraceptive???
Tumbo linauma??
Je Alikuwa Na Any Post Op Complication???
 
Ndiyo Menstruation ya kwanza
Na hii ni wiki ya tatu toka afanyiwe LEEP.
Alivyofanyiwa LEEP hakuwa na shida yeyote Ila kulikuwa kama na maji maji yaliyokuwa yanatoka kidogo sana.
kuhusu Contraceptives,alishawahi tumia Kijiti na toka atoe kijiti kuna zaidi ya miezi sita
 
Kafanyiwa LEEP lakini Sasa alipoingia hedhi damu inatoka nyingi na siku zinapita tu hedhi haikomi.
Leo anaenda tena Kwa Daktari wake,je humu kuna wajuzi wa chochote kuhusu hii condition iliyojitokeza. Kwa wale wenye experience na hii Operesheni hii condition ni normal au lah?
Una uhakika hiyo damu ni ya hedhi au inatoka kwenye shingo ya kizazi.? aende tu akafanyiwe uchunguzi wajue ni sehemu gani inapotoka hiyo damu
 
Fafanua LEEP ni nini
Loop Electrosurgical Excision Procedure

Ni operation ndogo inayofanywa kwa ajili ya wagonjwa wa kansa ya shingo ya kizazi katika hatua za mwanzo, inatumia waya wa umeme kuondoa seli zenye kansa kwenye shingo ya kizazi.
 
Kafanyiwa LEEP lakini Sasa alipoingia hedhi damu inatoka nyingi na siku zinapita tu hedhi haikomi.
Leo anaenda tena Kwa Daktari wake,je humu kuna wajuzi wa chochote kuhusu hii condition iliyojitokeza. Kwa wale wenye experience na hii Operesheni hii condition ni normal au lah?
Umefanya jambo zuri kwenda kumwona Dr.
Nategemea utapewa ushauri mzuri huko.
Kila la kheri
 
Una uhakika hiyo damu ni ya hedhi au inatoka kwenye shingo ya kizazi.? aende tu akafanyiwe uchunguzi wajue ni sehemu gani inapotoka hiyo damu
Aiseee hii ni kitu kipya.Sina uhakika hiyo damu inapotoka.Nilisema ni damu ya hedhi kulingana na kalenda yake.Lakini siku zinapitiliza na Bado inaendelea kutoka.Jana kaenda Hospital dr wake hakwepo hivyo anataraji kwenda kesho
 
Rudini hospitali haraka kabla hali haijawa mbaya zaidi. Poleni sana.

Mgonjwa alikuwa na kiuvimbe kidogo kwenye tumbo la uzazi hivyo wakafanya Operesheni ndogo ya kukitoa.Operesheni ilifanyika Bila kumchana walitumia sehemu za kike.
 
Umefanya jambo zuri kwenda kumwona Dr.
Nategemea utapewa ushauri mzuri huko.
Kila la kheri
Jana kaenda kumuona daktari wake Kwa bahati Mbaya weekend hii yote hakwepo hivyo anatarajia kwenda kesho.Damu inatoka na ni nyingi na tumeanza kuwa na hofu maana kama ni hedhi siku zinazidi kupitiliza na damu haiishi
 
Dah Hizi hospitali hizi siku hizi inabidi kuwa makini sana.
Kuna baadhi ya Madokta wapo kipesa zaidi.Hasa Magonjwa ya akina mama.Ukiona Mdada kaandikiwa Operesheni usikubali kufanyiwa Bila kwenda kujiuliza Kwa Madaktari wengine kadhaa.Kuna Daktari wa kiume Pale Regency wa kiume Kila Mdada anayeenda pale wengi wao wanaandikiwa Operesheni.Nawashauri wenzangu ukiiandikiwa Operesheni ni vizuri ukapata ushauri Kwa Madaktari wengine pia.
 
Kafanyiwa LEEP lakini Sasa alipoingia hedhi damu inatoka nyingi na siku zinapita tu hedhi haikomi.
Leo anaenda tena Kwa Daktari wake,je humu kuna wajuzi wa chochote kuhusu hii condition iliyojitokeza. Kwa wale wenye experience na hii Operesheni hii condition ni normal au lah?
huenda sio damu ya hedhi, huenda sehemu ni ile sehemu iliyotanyiwa kaoperation hako ndio kunatoa damu, ku a haja ya kwenda hospital kuchunguzwa
 
Jana kaenda kumuona daktari wake Kwa bahati Mbaya weekend hii yote hakwepo hivyo anatarajia kwenda kesho.Damu inatoka na ni nyingi na tumeanza kuwa na hofu maana kama ni hedhi siku zinazidi kupitiliza na damu haiishi
Siku imeisha. ..natarajia ulipata matibabu na mgonjwa yuko salama.
Usiache kurudi hapa na mrejesho kusaidia wengine katika Siku za usoni .

Kila la Kheri
 
Ameenda Hospital mara kadhaa Bila kumuona daktari mhusika aliyefanya Operesheni.Aliwaona Madaktari wengine ambao hawakutaka kumhudumia kuna ushauri walitoa lakini pia kuna kitu nilijifunza ,inavoonyesha hakukuwa na ulazima wa kufanya Operesheni.Inaonekana dr Ali suggest Operesheni Kwa maslahi binafsi.
Hata hivyo badaye alifanikiwa kumuona daktari husika alitoa maoni yake kuwa hii damu inatoka kwenye kidonda kilichofanyiwa alipofanyiwa Operesheni.Kwa hiyo kuna dawa kapewa za kutumia.Baada ya hapo tutaangalia maendeleo yake.
Ila nilichojifunza ni kuwa daktari anaweza suggest ufanye Kipimo ambacho Wala hakina uhusiano na Ugonjwa wako Ila atasuggest hicho Kipimo because ana maslahi nacho.
 
Poleni sana
 
Pole sana, Mungu azibariki na kuzitia nguvu dawa ili ziweze kumpatia uponyaji
 
Ameenda Hospital mara kadhaa Bila kumuona daktari mhusika aliyefanya Operesheni.Aliwaona Madaktari wengine ambao hawakutaka kumhudumia kuna ushauri walitoa lakini pia kuna kitu nilijifunza ,inavoonyesha hakukuwa na ulazima wa kufanya Operesheni.Inaonekana dr Ali suggest Operesheni Kwa maslahi binafsi.
Hata hivyo badaye alifanikiwa kumuona daktari husika alitoa maoni yake kuwa hii damu inatoka kwenye kidonda kilichofanyiwa alipofanyiwa Operesheni.Kwa hiyo kuna dawa kapewa za kutumia.Baada ya hapo tutaangalia maendeleo yake.
Ila nilichojifunza ni kuwa daktari anaweza suggest ufanye Kipimo ambacho Wala hakina uhusiano na Ugonjwa wako Ila atasuggest hicho Kipimo because ana maslahi nacho.
Poleni sana. Atumie dawa kwa muda mfupi km hakuna mabadiliko tafuteni gynaecologist mwingine awasaidie...
 
Super Sub Steve , poleni sana ila naamini mambo yatakaa sawa mkuu.
Hapo ndio huwa naona bora nionekane muoga au sifanyi maamuzi ya haraka linapokuja jambo la afya. Kama sio kitu ambacho kinaweza kugharimu uhai wa mtu na hayupo mahututi, napenda kupata ushauri sio chini ya mara tatu tena kutoka sehem tofautitofauti huku na mimi niki google (Thanks to google) ndio nafanya maamuzi.

Unaweza kwenda sehem wanakwambia hili jicho au sikio linatakiwa lifanyiwe upasuaji, sasa unajikuta unakubali kumbe hayo ni maoni ya huyo uliyemkuta lakini kungeweza kuwa na njia mbadala.

Tusiupuuze ule usemi wa zakuambiwa changanya na za kwako.
 
Back
Top Bottom