Baada ya Kufanya Mapenzi Ndani ya Bunge Waziri wa Australia Ajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya Kufanya Mapenzi Ndani ya Bunge Waziri wa Australia Ajiuzulu

Discussion in 'International Forum' started by TANMO, Sep 2, 2009.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,907
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 160
  Waziri wa Afya wa Australia John Della Bosca amejiuzulu uwaziri wake baada ya kimada wake kuyaanika mapenzi yao ya siri ya miezi sita kwenye gazeti.

  Della Bosca aliamua kujiuzulu baada ya gazeti la The Daily Telegraph la Australia kuchapisha habari ya mapenzi yake ya siri ya nje ya ndoa na mwanamke mwenye umri wa miaka 26.

  Della Bosca ambaye alikuwa akitegemewa kuwa mpinzani mkubwa wa waziri mkuu wa Australia katika uchaguzi ujao, alijiuzulu pia nafasi yake ya uenyekiti wa bunge.

  Kimada wa waziri huyo ambaye hakutajwa jina lake alisema kwamba alikuwa akiingia ndani ya ofisi za bunge bila ya kitambulisho chochote pamoja na ulinzi mkali uliopo na waliwahi kufanya mapenzi na waziri huyo kwenye makochi ya ndani ya ofisi za bunge.

  Kimada huyo katika kummaliza kabisa kisiasa waziri huyo alisema kwamba waziri huyo alikuwa akikwepa baadhi ya majukumu yake ya kazi ili watumbue raha.

  Kimada huyo alisema kwamba waziri huyo wa afya alijichelewesha ndege ya asubuhi kwenda mji mwingine ili asihudhurie ufunguzi wa hospitali moja kubwa nchini humo ili waweze kutumia muda pamoja.

  "Kwa jinsi alivyokuwa akitumia muda mwingi na mimi nashindwa kuelewa ni muda gani alikuwa akifanya kazi zake za ofisini" alisema kimada huyo.

  Kimada huyo alikuwa akijirusha na waziri huyo wakati wa mchana na nyakati za usiku waziri huyo alikuwa akirudi kwa mkewe.

  Ili kuuficha ukweli wa uhusiano wao wa siri, waziri huyo alimtaka kimada huyo ajitambulishe kwa watu wa karibu wa waziri huyo kuwa yeye ni mpwa wake.

  Kimada huyo alisema kwamba waziri huyo alikuwa akimwambia mara kwa mara kuwa atamuacha mkewe na kumuoa yeye.

  Kimada huyo alisema kuwa ameamua kuanika ukweli wa uhusiano huo baada ya kuona kuwa waziri huyo anamtumia kwaajili ya matamanio yake ya kimapenzi tu.

  Akiongea kwa mara ya kwanza baada ya skendo hilo kuibuliwa, bwana Della Bosca alisema kwamba anajutia maamuzi yake ya kuingia kwenye uhusiano huo haramu.

  "Nimechukua maamuzi mabaya. Kama utachukua maamuzi mabaya basi inabidi unywe vidonge vyake vichungu. Kwa sababu hii sitaki kuiteteresha serikali. Nahuzunika kwa kuiaibisha familia yangu" alisema waziri huyo wakati akitangaza kujiuzulu.


  Chanzo cha Habari Nifahamishe
   
 2. B

  Babuji Senior Member

  #2
  Sep 2, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanawake wanawake wanawake
   
 3. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ukilikoroga lazima ujue kuna siku utalinywa tu!
  Ila huyu dem ni kimeo live.
   
Loading...