Baada ya kufanya kazi kubwa, Mwamba anarudi kuitumikia nchi yake

John Gregory

JF-Expert Member
Jul 14, 2019
1,060
1,956
Kila la kheri kwa Jini, Predator.... mchezaji bora Afrika na katika ligi kuu ya Tanzania Bara.Tunashukuru kwa makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa ndani ya Tanzania na Afrika, sasa ni wakati wa kurejea nyumbani kuitumikia nchi yako wakati tukijipanga kufika fainali na kuchukua ubingwa CAFCC!

Daima mbele!

IMG_20230320_101210.jpg
IMG_20230320_101217.jpg
IMG_20230320_101210.jpg
IMG_20230320_101201.jpg
 
Huyu mwamba amsha amsha zake ananikumbusha aina ya washambuliaji ambao Tanzania ilikuwa nao miaka ya nyuma...

Madogo wa sasa wana kitu cha kujifunza toka kwa huyu mpambanaji...
Wapi? Mnaleta story za abunwasi kama yule jamaa wa Azam TV siku ya jumapili anachukua muda mwingi kureeemba mambo ya zamani na kuwaita watu wa Zamani. Tuambie hiyo hao wachezaji wa Zamani mnaowasifia waliletankombe gani bongo?
 
Kwa kweli siku za karibuni Fiston Mayele aneimarika na kuwa mshambuliaji hatari sana. Mwanzoni alipoanza kuichezea Yanga, alikuwa ni mchezaji wa kufunga magoli ya kuvizia.

Ila kwa hizi siku za karibuni, amebadilika kiuchezaji! Mara nyingi amekuwa anafunga magoli ya kuwachambua mabeki huku akiwa katika kasi ya ajabu, na mwisho wa siku anatafuta angle nzuri ya kufunga.

Kwa kweli anastahili pongezi.
 
Mayele kachukua kaweka waa aloo ukiangalia lile goli la pili unajikuta unajipiga kifua na kusema hakika atayeisumbua Gsm chini ya Eng Hersi Said apigwe mboko nyingi tu, jicho la skauti kwa huyu mwamba kongole kwao mwamba anatubeba sana lile goli la pili kusanya washambuliaji wote wa Simba na Nyongeza hakuna anayeweza kulifunga

All the best kwenye majukumu ya Timu ya Taifa the Leopards goli la jana kama lile alilozindulia style yake ya kutetema kwa Manula.
 
Aliyofanya Kagere kwenye ligi hii hata nusu tu huyo mchezaji wenu bado hajayafikia. Huyo ni mchezaji wa kihistoria kwenu na sio kwenye ligi achilia mbali Afrika.
Exactly mkuu. Wanaongelea kimapenzi zaidi lakini MK14 amefanya wonders sana.
Mayele anajitahidi, labda kadri mda unavyozidi kwenda atafanya makubwa zaidi huenda kumzidi MK14, John Bocco na Emmnauel Okwi.
 
Wapi? Mnaleta story za abunwasi kama yule jamaa wa Azam TV siku ya jumapili anachukua muda mwingi kureeemba mambo ya zamani na kuwaita watu wa Zamani. Tuambie hiyo hao wachezaji wa Zamani mnaowasifia waliletankombe gani bongo?

Umeandika kama mtu mwenye hasira kali...
 
Back
Top Bottom