Baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Bashiru Ally alipaswa kwenda "rasmi" kuipa pole familia ya Balozi Kijazi. Huu ndio uungwana

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Habari za wakati huu wanachama wa jamiiforums

Baada ya kuapishwa kuwa katibu mkuu kiongozi, mzee Bashiru Ally alipaswa kwenda "rasmi" kuipa pole familia ya Balozi Kijazi. Huu ndio uungwana wetu sisi waafrika. He was supposed to go and condole the family of his predecessor.

images (2).jpg

Nina imani kubwa sana na utendaji kazi, hekima pamoja na busara za Dr. Bashiru Ally Kakulwa sio tu baada ya kuwa katibu mkuu wa CCM bali hata alipokuwa Mhadhiri Muandamizi katika taaluma ya Sayansi ya Siasa pale chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mzee Bashiru ni moja kati ya wanazuoni makini na hazina kubwa ambayo Mwenyezi Mungu amelijalia taifa hili la Tanzania.

Mnano tarehe 17 February 2021 Tanzania ilifikwa na msibwa mkubwa wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi kwa wakati ule Mhe. Balozi John Kijazi. Kama ilivyo kawaida yetu sisi Watanzania, viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na chama walifika ukumbi wa Karimjee kumuaga Mh. Balozi.

Hata kama Mzee Bashiru alikuwapo siku ya mazishi au wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa Balozi Kijazi, basi alikuwapo pale kama kiongozi wa kisisasa yaaani katibu mkuu wa CCM na sio kama mtumishi wa umma/serikali aliyekalia kiti cha Kijazi (Katibu Mkuu Kiongozi). He was there as a political figure and not a public servant.

Kwa wale wadogo zangu wasiofahamu hii imekaa hivi, siku zote mtumishi anapokufa, hususan wa umma, anakuwa amekufa yeye lakini ofisi imebaki nikiwa na maana kwamba Balozi Kijazi alifariki lakini ofisi ya katibu mkuu kiongozi bado ilikuwepo, tofauti kabisa na ofisi za watu binafsi ambazo boss akifa basi na ofisi, kama ni duka, nayo inakufa.

Katika ofisi hiyo bila shaka kuna wafanyakazi wa kada mbalimbali waliokuwa chini yake, ambao sasa watakuwa chini ya mzee Bashiru, na bila shaka walifika moja kwa moja nyumbani kwa Hayati boss wao na kufikisha salamu za pole (sina uhakika lakini nina imani walifanya hivyo kutokana na utamaduni mwema wetu sisi watanzania) lakini ikumbukwe ya kwamba Pope John Paul II aliwahi kusema maneno haya "To maintain a joyful family requires much from both the parents and the children. Each member of the family has to become, in a special way, the servant of the others"

Mzee Bashiru as a new parent in the office (a new Chief Secretary) was supposed to serve his part the same way his children (fellow workmates in his new office) did to the ambassador Kijazi's family.

HUU NI MTAZAMO WANGU TU, NIPO TAYARI KUSAHIHISHWA (I STAND TO BE CORRECTED)

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Yanini Utumbo utupwe wakat wenyej tunaulia na ndizi.

Alisikika mlevi mmoja:
 
Kuwa muungwana ni kitu ambacho mtu anazaliwa nacho wala siyo elimu kama alivyo Bashiru.

Bashiru amejawa kiburi na dharau sana na ukichanganya na hayo madaraka aliyopewa ndiyo usiseme kabisa.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom