Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi...

Mkuu hivi majichumvi mradi wako unaufanyia wapi maana nimezunguka sana maeneo haya na mpaka mda huu nipo huku ila bado sijui upo eneo gani? Majichumvi kuna mfugaji mmoja tu mmama/mdada ambae anafuga nguruwe..
Hebu nielekeze boss nitembelee eneo lako mimi nipo karibu na kiwanda cha nyama kabisa..
 
Usijali mkuu. Nitakupm ili tuwasiliame. Tena kwa yeyote atayetaka mitiki nitamuunganishia miche Kwa sh 300 Kwa mche. Kipindi kipindi Cha kupanda mitiki ni kipindi Cha mvua.
Aisee mkuu ni safi sana, nahitaji kuunganishwa ili nijipatie mitiki, na kwa hekari moja miche mingapi yapaswa kupandwa.
 
Hongera kwa maamuzi uliyochukua naona baada ya muda mfupi itakua mbali mno
 
Safi jumamosi ijayo nawakaribisha mje kuona project.
Safi sana mkuu, Hiyo fursa ya kukutembelea tunaikosa tulio mbali Mungu akijaalia uzima na mimi nikiwa karibu nitakutafuta nije kukutembelea mkuu, Mungu azidi kukubariki na kukushushia baraka ufikie malengo yako kaka.
 
Hongera sana kwa kuwa mjasiriamali.

Naomba kujua kisima ulichimba kwa bei gani na ni vitu gani vya kuzingatia ?

Asante.
 
Ama kweli umenitia moyo na ujasiri, ingawa mafanikio yanaweza kuwepo au kutokuwepo,
Tulipo fikia vijana ni pazuri,yaani kusubutu, ningependa apatikane mtu au mtaaram atujuze yafuatayo
1) watoto wa nguruwe wanabei gani.
2)gharama ya kutengeneza banda la kawaida
3)gharama za kuwalisha kwa mwezi
4) eneo lenyeukubwa gani unaweza fuga ngurue wangapi
5)wanatosha kuliwa ktk umri gani
nazani mambo haya yatatusaidia.
Tuwasiliane
 
Miongoni mwa siku ambazo najivunia kuwa mwanachama wa JF ni leo!

Nikiri kuwa nimepata shule ya maana sana kwa leo, nina eneo la takribani ekari 12 mpango ilikuwa ni kuligawa.

Ekari 2 mazao ya chakula, yaani kuhakikisha kuwa ndani ya mwaka mmoja sinunui mahindi wala maharage kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya chakula, ziada nauza kwa ajili ya kununua aina nyingine za vyakula.

Ekari 5 kuzipanda mananasi, kila ekari inaingia karibu miche 3500 nanasi halina tabu sana kwenye kulilea, likiwa tayari unauza ukiwa shamba moja kwa sh 550/ ukipeleka mwenyewe sokoni ni sh 1000/= Hesabu inakuwa hivi miche, 3500 kwa hekari moja mara 5 = 17500, chukulia umepata mananasi 17000 mara 550 (ukiuuzia shamba) = 9,350,000/= (Mananasi si zaidi ya miezi 11).

Ekari 3 natupia mitiki hakiba ya baadae kwa ajili ya makamanda wangu 2, wakifikisha miaka 20 itakuwa tayari kuvuna.

Mifugo ekari 1, kipaumbele ni kuku, mbuzi na ng'ombe. Sasa hivi ukiwa na ng'ombe 4 ulio walisha vizuri kima cha chini ukiwauza wote ni karibu 1.6M, hapo bado kuku, na mbuzi.

Mpango ni kuwa na hekari 40 kabla ya kufikisha 35
Wazo zuri mkuu,Mungu akusimamie utimize ndoto yako.
 
Back
Top Bottom