Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi...

Naomba nithibitishe kuwa taarifa ya mm kushindwa project siyo ya kweli. Siamini katika kushindwa. Wala muhusika hajawahi kunitembelea.

Tunafurahi kuona umerejea na kukanusha, ilamkuu tunaomba utujuze uzoefu uliopata na haswa changamoto na mafanikio Itawatia moyo walio wengi kwani kitu ulichofanya kimsingi ndio ukombizi wenyewe wa kiuchumi.
 
Naomba nithibitishe kuwa taarifa ya mm kushindwa project siyo ya kweli. Siamini katika kushindwa. Wala muhusika hajawahi kunitembelea.

mkuu tueleze hadi sasa project yako inaendelea vipi?? hata kama umefulia unaweza simama tena kwani wakale walisema "barabara ndefu, haikosi kona" hivyo ili iyafikie mafanikio ya kweli lazima kuwa na kushindwa , lakini inakupasa kusimama na kuendelea na safiri....kuna muda mwingine barabara inakuwa na kona kana kwamba inarudi/inaelekea unakotoka, lakini kumbe ndo inaelekea unako kwenda..hivyo usikate tamaa ita tambua unako kwenda,....
tupe changamoto hadi sasa ambazo umekutana nazo katika safari yako nasi tupate kujifunza na si kukata tamaa..niko morogoro jirani na eneo lako huko maji chumvi pande za makunganya hapa.
 
Kaka naona utajiri uko mkonon mwako ongera sana kwa ushaidi Wa picha umenivutia sana ngoja nipate kamtaji
 
mkuu tueleze hadi sasa project yako inaendelea vipi?? hata kama umefulia unaweza simama tena kwani wakale walisema "barabara ndefu, haikosi kona" hivyo ili iyafikie mafanikio ya kweli lazima kuwa na kushindwa , lakini inakupasa kusimama na kuendelea na safiri....kuna muda mwingine barabara inakuwa na kona kana kwamba inarudi/inaelekea unakotoka, lakini kumbe ndo inaelekea unako kwenda..hivyo usikate tamaa ita tambua unako kwenda,....
tupe changamoto hadi sasa ambazo umekutana nazo katika safari yako nasi tupate kujifunza na si kukata tamaa..niko morogoro jirani na eneo lako huko maji chumvi pande za makunganya hapa.
Thank you for your concern. Sijafulia. Siamini katika kushindwa. Project iko sawa. Hata hivyo kwa sasa ninaendelea na project yangu ya shule tunayotarajia tutaifungua punde. Ninatumia muda meingi sana kufikiria ndiyo maana naamini katika mafanikio. Mawazo yangu juu ya ujasiriliamali kwa sasa ni ya juu sana. Nitawarushia picha.
 
Hongera mkuu, Sky is the limit
 
mtaji pia n tatizo wakuu,,,
kaka tafuta wazo. Jipime kama unaweza kulifanya. Angalia nazingira. Fikiria namna utakavyopata pesa. Omba Mungu tena omba tena. Uwe tayarihata kufanya Kazi ya kupiga kiwi. Anza taratibu. Anza project ambayo mtaji wake unaweza kuutafuta. Katika kuanzisha biashara/shughuli ya kujiongezea kipato hakuna kitu kikubwa na kigumu kama kutafuta wazo. Hapa panahitaji utulivu. Wengi wanafanya copy and paste which it too wrong. Be creative brother. Toka kivyako. Fany? ahort twrm and long term impact analysis for your project. Be a greater thinker. Think positive. Avoid negative thinkers. Waache watu wakuige maana hawataweza kufikia level yako na hats wakifikia wewe utakuwa umeshaondoka huko. Kama unashindwa kuunganisha mawazo yako come and see me. Nitakuchaji kidogo kama gharama ya kuusumbua ubongo wangu.
 
Asante sana!, kupanga ni kuchagua. Asante kwa kunitia moyo mm binafsi, one day nitapita hapo kuona kwa macho
 
Hongera sana mkuu shamba halimtupi mkulima wengine pia twafaidika kwa uzi huu tuta Ku join soon ktk agribusiness
 
Usijali mkuu. Nitakupm ili tuwasiliame. Tena kwa yeyote atayetaka mitiki nitamuunganishia miche Kwa sh 300 Kwa mche. Kipindi kipindi Cha kupanda mitiki ni kipindi Cha mvua.
Kaka nitumie namba yako,kuna msaada wako nauhitaji.
 
Mkuu na

Mkuu na wewe unaonekana ni mjanja fulani wa mjini tu, picha toka ulipoanzisha uzi mwaka 2013 mpaka leo hujawahi kutoa picha nyingine yoyote ya maendeleo ya mradi, siku hizi mambo ni marahisi sana kupiga picha na kuupload wangalau haichukui hata dk 10. Sasa wewe miaka miwili huna picha kuonyesha nini kinaendelea kwenye hiyo project!!? Inawezekana hiyo project sio yako labda ilikuwa ni ya jamaa yako hiyo siku uliyofika ndio ukapiga picha na kuleta post nzuri ya ujasiriamali. Basi hata kama sio ya kwako muombe huyo rafiki yako uturushie tuone amefikia wapi.

Nilichojifunza kwenye mambo ya ujasiriamali ni wakati unapoamua ama kuanza unapata darasa moja lenye kukuonyesha mafanikio tu, hivyo unakuwa na matarajio makubwa sana kiasi kwamba yale matarajio ndio unaanza kuhadithia watu lakini unapokuja kwenye uhalisia ndio inakuwa kinyume, matokeo yake hata kutoa taarifa kamili inakuwa ngumu. Kwa kweli kwa sisi tulioingia kwenye ujasiriamali tumejifunza mengi na tumeendelea kubaki kwa kuwa ni wito lakini kiukweli kuna maslahi duni. Kama mmewahi kufuatilia post zangu nyingi humu jukwaani huwa ninalalamika sana suala la maslahi duni kwenye mazao yetu. Miaka nenda rudi unakuta bei ya mazao ama mifugo haipandi lakini bidhaa nyingine kama za viwandani zinapanda kila wakati. Mfano mrahisi, bei ya kuku utakuta ni 8,000-15,000@. Lakini gharama ya mpaka umuuze haipungui sh 10,000-13,000. Bei ya mbogamboga haipandi kamwe lakini bei ya pembejeo za kilimo zinapanda mara kwa mara. Hali hii inawafanya wakulima na wafugaji kubaki hohehahe. Leo hii ni nadra mkulima kupata mkopo wenye maana kwani hata mabenki yameshaona wakulima huwa wanashindwa sana kurudisha mikopo. Nimekuwa nikipiga kelele sana kuhusu viongozi wetu kukalia kimya suala la uuzaji mazao kwa njia ya rumbesa, lakini wapi hawajali maana wao wako maofisini wanasaini hela kwa kutumia receipt fake. Kwa hiyo sishangai mleta mada kukutana na hali hii mpaka kuingia mitini.
 
Back
Top Bottom