Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi...

Eberhard

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
1,120
757
Baada ya kumaliza degree yangu ya pili na kuona kuwa ajira kama ajira haiwezi kuwa mkombozi wangu kiuchumi niliamua nifatilie mawazo mbalimbali ya ujasiriamali. Nikafikiria ujasiriamali wa kiubunifu wa hali ya juu ndiyo utakuwa mkomnozi wangu kiuchumi. Nimeanza Kwa kununua shamba lenye ukubwa wa hekari 12 nje kidogo ya mji wa Morogoro ( Kwamakunganya-majichumvu). Sehemu kubwa ya shamba langu nimepanda mitiki.

Baada ya kufatilia humu nikagundua kuwa mradi wa nguruwe na kuku wanalipa sana. Ninaomba kukili kwamba miongoni mwa post ambayo serious nilihaidi kuifanyia kazi ni Anza hivi mpwa wangu. Kwa kuwa imani yangu inaniruhusu nikaona ni laziima niifanya hii ya Anza hivi mpwa wangu. Hivyo nikaanza maandalizi ya kufuga nguruwe na kuku pia. Hivyo nilianza Kwa kuanzia kuchimba na kujengea tangi la maji chini. Ilichukua Muda wa miezi miwili tangu langu la maji kukamilika. Tangi langu la maji Lina uweze wa kujaza maji lita 30 elfu.

Baada ya hapo nikaanza maandalizi ya ujenzi wa banda la nguruwe na la kuku. Baada ya mabanda yangu kukamiliaka nilisafiri hadi singida kufata kuku. Bei ya kuku singida inalidhisha sana. Ili upate kuku wa bei rahisi inakupasa uende vijijini ambako kuku huuzwa cheap. Hivyo nilisafiri hadi kijijini ambako nililinunua kuku 31 ambao ndiyo nimeanza nao.. Kwa upande wa nguruwe nimeanza na 12 ambao niliwanunua wakiwa na miezi mitano. Pia nimeweka kanga na mbuzi Kwa ushauri wa marafiki.

Ninashukuru Mungu ninaanza kuwaona kuku wameanza kutaga Kwa fujo. Pia ninamshukuru Mungu Kwa kuwa ninaona ninaanza kuwa muajili pole pole. Pia ninamshukuru Mungu ninaona mawazo ya kunyanyasika( kuajiliwa) yanaanza kupotea taratibu.Kwa sasa nguruwe wangu wameshabeba mimba hivyo nategemea kuanza kuona mabanda yangu yakijaa vitoto vya nguruwe hivi punde.
Kupitia uzi wangu huu nitakuwa nawataarifu maendeleo ya mifugo yangu Kama sehemu ya kuwatia moyo wajasiriamali wenzangu. Morogoro ni sehemu ambayo wajasiriamali mnaweza kutimiza ndoto zenu Kwa kuwa Ardhi inapatikana Kwa bei nafuu na ni Karibu na Dar kwenye soko kubwa la bidhaa mbalimbali.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    73.4 KB · Views: 2,840
  • image.jpg
    image.jpg
    91.2 KB · Views: 3,092
  • image.jpg
    image.jpg
    73.4 KB · Views: 2,805
  • image.jpg
    image.jpg
    53.5 KB · Views: 2,795
  • image.jpg
    image.jpg
    122.1 KB · Views: 2,904
  • image.jpg
    image.jpg
    76 KB · Views: 2,680
  • image.jpg
    image.jpg
    89.7 KB · Views: 2,750
  • image.jpg
    image.jpg
    140.8 KB · Views: 2,586
  • image.jpg
    image.jpg
    140.5 KB · Views: 2,497
  • image.jpg
    image.jpg
    92.3 KB · Views: 2,345
  • image.jpg
    image.jpg
    103 KB · Views: 2,131
  • image.jpg
    image.jpg
    99.9 KB · Views: 2,057
  • image.jpg
    image.jpg
    102.2 KB · Views: 2,128
Safi sana mkuu, hiyo ndo Swaga yenyewe, na unachosema ni kweli Kuajiriwa ni utumwa wa hali ya juu kabisa na husababiha hadi kilema cha ubongo, hakuna jambo baya kama kukaa kusubili mwisho wa mwezi au kuwa chini ya himaya ya mtu mwingine,

Wewe pambana tu hakuna kisicho wezekana chini ya Jua
 
unaajiriwa kwa muda wa miaka 30 unapata pension lets say ya shs mil 40,wakati ukijipanga ktk ujasiriamali utahangaika mwaka mmoja wa kujiestablish,40 mil can be generated on year,bravo eberhard.

ndo hivyo mkuu, ila mtu hawezi amini kwamba kuajiriwa kunalemaza akili ni mpaka siku hiyo unakutana n barua ya kupunguzwa kazi ndo utajua kwamba ajira si ishu,

Mleta Maada hapo kaanza mdogo mdogo na nina amini baada ya miaka miwili mitatu jamaa atakuwa mbali sana na kuweza hata kuajiri mtu mwenye Masters
 
hongera sana mkuu Eberhard
vipi hilo tangi lako la maji unapataje maji? I mean unajaza mwenyewe, unavuna maji ya mvua au umevuta bomba la moruwasa?
ninanunua maji Kwa Yale magari makubwa yanayobeba maji. Lita 15 elfu ninazitumia Kwa miezi mitatu. Kipindi Cha mvua nitayakimga. mradi wangu sijaanza siku nyingi. Hatua zote nilizianza mwezi wa tatu. Tangu niiweke mifugo sasa nina mwezi mmoja.
 
Last edited by a moderator:
Hongera kaka.
Huko lilipo shamba lako ni wapi? Tafadhali elekeza yeye.
lipo Kwa makunganya. Ukiwa unaenda Dodoma ni kijiji kinachofata baada ya pale mizani. Kituo Cha kushukia kinaitwa stop. Pale utachukua pikipiki kueelekea sehemu inayoi majichumvu. Ni jirani sana na kiwanda Cha nyama.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    124.8 KB · Views: 1,231
  • image.jpg
    image.jpg
    123.7 KB · Views: 1,241
Dah imenishika jamii kubwa hasa ya Kitanzania hasa wenye elimu ya kutosha wamekumbwa na jinamizi hili je, tufanye nini ili kuepukana na janga hili lenye kupumbaza akili ya wengi bila kujali thamani zao?

Mc!

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Mkuu hongera sana!ukweli ni kua kwa wajasiriamali hasa sisi tunaotaka kufanya kilimo na ufugaji mkoa wa Morogoro ni potential sana!Mwenyewe nimechukua ka ardhi kidogo katika eneo la Msowelo,na nimeanza kijilimo cha bustani,ila kwa kweli naona kabisa kuna future ya kueleweka through kilimo na ufugaji,na target yangu ni kua mwakani niweze kununua hata heka 15 hivi!

Hili la mitiki umenifurahisha sana mkuu,maana ni moja ya wazo ambalo linaumiza kichwa yangu!ukweli ni kua thread yako imenivutia sana,kuna ya msingi kujifunza toka kwako!kama haitakua bughudha mkuu ningeomba uni PM contacts zako ili nikutafute na niweze kupata shule zaidi kwa yale yaliyo ndani ya uelewa wako lakini ni mageni kwangu
 
fanya mpango in lobg run ulipime upate tittle maana mafisadi wanataka vyote,wasije wakabadili matumizi ya ardhi,ujasiriamali ni kitu kizuri sana kwa maisha ya sasa,shughuli yoyote inayohusiana na chakula hakika haukutupi,

ni lazima kuwa na msimamo ktk maamuzi,

kupanua wigo wa mtandao wa habari sahihi(hii itasaidia kupata masoko pia)

ubunifu ni muhimu

kukubali changamoto mbalimbali zitokanazo ujasiriamali i.e masoko,rasilimali watu,vitendea kazi n.k

na zaidi miradi ya wajasiriamali iwe endelevu na kila siku ni muhimu kujifunza kitu kipya.
 
Nazani hili jukwaa limekusaidia vilivyo, hata mimi kama ningeijua JF tangu 2007 nisingethubutu kuajiriwa kamwe hata hivyo nilishaachana na utumwa, hongera sana mwenye uzi.
Ahsante mkuu. Maana nimesoma mpaka nikakaribia kumaliza madarasa yote lakini sikuona dalili za kutoka hasa hasa. Nimegundua ukishasoma inahitaji uwe na vitu vinavyoitwa connection, ufitina, kujikombakomba ndipo ule. Hata hivyo yote haya hayatoi mafanikio. Kwa mtu unayetaka kuwa mcha Mungu bila kuishi maisha ya kitapelitapeli Kama maaskari wa barabarani maisha yako yote ni bora kukimbilia kwenye ujasiriamali. Maana ukiajiriwa hata Kama iweje ndiyo lazima useme ndiyo mkuu, hivyo hivyo mkuu, Mimi sina Cha kuongeza na sawasawa ujue watoto hawataenda shule nzuri.
 
Mkuu hongera sana!ukweli ni kua kwa wajasiriamali hasa sisi tunaotaka kufanya kilimo na ufugaji mkoa wa Morogoro ni potential sana!Mwenyewe nimechukua ka ardhi kidogo katika eneo la Msowelo,na nimeanza kijilimo cha bustani,ila kwa kweli naona kabisa kuna future ya kueleweka through kilimo na ufugaji,na target yangu ni kua mwakani niweze kununua hata heka 15 hivi!ili la mitiki umenifurahisha sana mkuu,maana ni moja ya wazo ambalo linaumiza kichwa yangu!ukweli ni kua thread yako imenivutia sana,kuna ya msingi kujifunza toka kwako!kama haitakua bughudha mkuu ningeomba uni PM contacts zako ili nikutafute na niweze kupata shule zaidi kwa yale yaliyo ndani ya uelewa wako lakini ni mageni kwangu

Usijali mkuu. Nitakupm ili tuwasiliame. Tena kwa yeyote atayetaka mitiki nitamuunganishia miche Kwa sh 300 Kwa mche. Kipindi kipindi Cha kupanda mitiki ni kipindi Cha mvua.
 
Baada ya kumaliza degree yangu ya pili na kuona kuwa ajira kama ajira haiwezi kuwa mkombozi wangu kiuchumi niliamua nifatilie mawazo mbalimbali ya ujasiriamali. Nikafikiria ujasiriamali wa kiubunifu wa hali ya juu ndiyo utakuwa mkomnozi wangu kiuchumi. Nimeanza Kwa kununua shamba lenye ukubwa wa hekari 11 nje kidogo ya mji wa Morogoro ( Kwamakunganya-majichumvu). Imenigharimu 1.3 m kununua eneo hili lote.. Nililipia taratibu hata sasa bado nadaiwa sh 60 elfu nayotegemea kuimalizia after 2 weeks. Sehemu kubwa ya shamba langu nimepanda mitiki.

Baada ya kufatilia humu nikagundua kuwa mradi wa nguruwe na kuku unalipa sana. Kwa kuwa imani yangu inaniruhusu nikaona ni laziima niifanya hii yakiti moto pia. Hivyo nikaanza maandalizi ya kufuga nguruwe na kuku pia. Hivyo nilianza Kwa kuanzia kuchimba tangi la maji chini. Ilimigharimu Kama mwezi miwili tangu langu la maji kukamilika. Tangi langu la maji Lina uweze wa kujaza maji lita 30 elfu.

Baada ya hapo nikaanza maandalizi ya ujenzi wa banda la nguruwe na la kuku. Baada ya mabanda yangu kukamiliaka nilisafiri hadi singida kufata kuku. Bei ya kuku singida inalidhisha sana. Ili upate kuku wa bei rais inakupasa uende kijijini ambako kuu huuzwa cheap. Nimeanza na kuku 31. Kwa upande wa nguruwe nimeanza na 12 ambao niliwanunua wakiwa na mwezi 5. Pia nimeweka kanga na mbuzi Kwa ushauri wa marafiki.

Ninashukuru Mungu ninaanza kuwaona kuku wameanza kutaga Kwa fujo. Pia ninamshukuru Mungu Kwa kuwa ninaona ninaanza kuwa muajili pole pole. Pia ninamshukuru Mungu ninaona mawazo ya kunyanyasika( kuajiliwa) yanaanza kupotea taratibu.
Kupitia uzi wangu huu nitakuwa nawataarifu maendeleo ya mifugo yangu Kama sehemu ya kuwatia moyo wajasiriamali wenzangu. Morogoro ni sehemu ambayo wajasiriamali mnaweza kutimiza ndoto zenu Kwa kuwa Ardhi inapatikana Kwa bei nafuu na ni Karibu na Dar kwenye soko kubwa la bidhaa mbalimbali.

Mkuu asante sana kwa kutuhabarisha habari njema, ila mkuu nilikuwa na shida kuhusu shamba huko, na heka huanzia tsh ngapi?
 
Back
Top Bottom