Baada ya kuambiwa nilipe kwanza kodi ndio nianze biashara sasa nimeamua kuwa mkwepa kodi.

Tranquility State

Senior Member
Feb 14, 2018
121
96
Habari za muda huu ndugu zangu.
Mimi ni mkazi wa Dar es Salaam ila nilikuwa na wazo la kufanya biashara ndani ya wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani.

Kwa kifupi ni kwamba leo 26/03/2018 pale TRA Kisarawe nimeambiwa lazima nilipe kodi kwanza ndio nifungue biashara.
Makadirio ya kodi ya chini nimeambiwa ni Tsh150,000.

Hio kodi eti natakiwa kulipia kuanzia mwezi wa kwanza(01/01/2018) hata kama nilikuwa sijaanza biashara lakini ni sheria kulipa mwaka mzima na kabla ya kuanza biashara.

Kutokana na hali hii nimeamua kutafuta namna ya kufanya biashara yoyote ambayo nitakuwa nakwepa kodi ili niweze kuepukana na unyonyaji nilioambiwa leo pale TRA Kisarawe.

Naomba tushauriane namna ya kukwepa kodi pia biashara gani inafaa kuweza kukwepa kabisa kodi maana naona mfumo uliopo ni lazima ukwepe kodi ili uweze kufanikiwa kiuchumi.

Vijana mjiajiri ila tambua hata kama huna mtaji unatakiwa kulipa kodi kwanza sio kutoka kwenye faida.
Hii ndio Tanzania ya viwanda.
Mwisho tupeane mbinu za kukwepa kodi.
Mtaji nilionao ni siri yangu.
 
Mkuu ukitaka kufanya biashara lipa tuu kodi kwa Tin Mpya ambayo ndio kwanza unaanza biashara nilimsikia mwenyewe Mwandumbya mkuu wa kodi za ndani akizungumza miezi sita ya mwanzo haulipi kodi akiwa Mafinga...nenda kwa Afisa mwingine sio lazima huyo aliekukatisha tamaa maana ukikamatwa kwa kukwepa kulipa kodi adhabu yao ni kubwa sana...
 
Unalipaje kodi kabla ya kuanza biashara,yaani una mtaji kidogo halafu unaanza kwa kulipa kodi.

Kukwepa kodi ni bora zaidi ili kuinuka kiuchumi.
Mkuu ukitaka kufanya biashara lipa tuu kodi kwa Tin Mpya ambayo ndio kwanza unaanza biashara nilimsikia mwenyewe Mwandumbya mkuu wa kodi za ndani akizungumza miezi sita ya mwanzo haulipi kodi akiwa Mafinga...nenda kwa Afisa mwingine sio lazima huyo aliekukatisha tamaa maana ukikamatwa kwa kukwepa kulipa kodi adhabu yao ni kubwa sana...
 
Mkuu ukitaka kufanya biashara lipa tuu kodi kwa Tin Mpya ambayo ndio kwanza unaanza biashara nilimsikia mwenyewe Mwandumbya mkuu wa kodi za ndani akizungumza miezi sita ya mwanzo haulipi kodi akiwa Mafinga...nenda kwa Afisa mwingine sio lazima huyo aliekukatisha tamaa maana ukikamatwa kwa kukwepa kulipa kodi adhabu yao ni kubwa sana...
Kwapa tu
 
Habari za muda huu ndugu zangu.
Mimi ni mkazi wa Dar es Salaam ila nilikuwa na wazo la kufanya biashara ndani ya wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani.

Kwa kifupi ni kwamba leo 26/03/2018 pale TRA Kisarawe nimeambiwa lazima nilipe kodi kwanza ndio nifungue biashara.
Makadirio ya kodi ya chini nimeambiwa ni Tsh150,000.

Hio kodi eti natakiwa kulipia kuanzia mwezi wa kwanza(01/01/2018) hata kama nilikuwa sijaanza biashara lakini ni sheria kulipa mwaka mzima na kabla ya kuanza biashara.

Kutokana na hali hii nimeamua kutafuta namna ya kufanya biashara yoyote ambayo nitakuwa nakwepa kodi ili niweze kuepukana na unyonyaji nilioambiwa leo pale TRA Kisarawe.

Naomba tushauriane namna ya kukwepa kodi pia biashara gani inafaa kuweza kukwepa kabisa kodi maana naona mfumo uliopo ni lazima ukwepe kodi ili uweze kufanikiwa kiuchumi.

Vijana mjiajiri ila tambua hata kama huna mtaji unatakiwa kulipa kodi kwanza sio kutoka kwenye faida.
Hii ndio Tanzania ya viwanda.
Mwisho tupeane mbinu za kukwepa kodi.
Mtaji nilionao ni siri yangu.
Fremu ya biashara umeanza kuitumia kabla ya kulipia?
 
Kumbuka tu kwa Tanzania suala la kodi ya mapato halihusiani na faida,

Cha muhimu zingatia yafuatayo;

mbinu ya ukwepaji kodi ni tofauti kutokana na mazingira, ulizia kwa majirani zako wanakwepaje kodi, kumbuka mbinu za mwanza zinaweza zisifae huko,

halafu hujasema unataka kufanya biashara ya aina gani,

Tabia za wateja wa sehemu husika.

Location la goli lako, ukiwa mwanzoni sana utakuwa kila Siku unabambwa

Mawasiliano na wafanyabiashara wenzako

Hawapiti kila siku, inakuwa kwa kipindi fulani kama zimamoto, maranyingi mwaka wa fedha unapoisha ili waongeze makusanyo
 
Asante kwa mchango wa mawazo

Huu uzi unanihusu sana mkuu maana mie mwenyewe yalinikuta wakt nataka kuanzisha biashara ila napga mishe hadi sahz cjalipa kodi nina week tu
 
Back
Top Bottom