Kichwa Kichafu
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 44,560
- 188,751
Asante mleta mada kuna watu wabishi sana
Mwache aendelee kulea watoto kizembe zembe... Tena hawa wakiume ndio asijaribu... Wenzao wanatembe saa nzima yy anashangaa 25Unashangaa dakika 25 mkuu?? kuna watoto ambao wanatembea hadi saa zima,
Yani unataka usimlishe mtoto? Akifa je?Ivi jamani mwisho wa kumlisha mtoto ni miaka mingapi?
Mkuu wewe kama baba ukizembea kwenye malezi ya mtoto hasa wa kiume jua unaandaa bomu litakalo kulipukia huko baadae.Bado sijutii uamuzi nliofanya,
Hapo awali mtoto nlikuwa namlea kimayai huku nikijioa moyo sitaki apitie shida nlizopitia kumbe nlikuwa navuka mipaka kabisa ambayo haikuwa vema kwa mtoto,
Nikabadili malezi na kweli dhana yangu ya kutotaka mtoto asipate ahida nlizopitia nliendelea nayo ila iliishia tu kuhakikisha mtoto anapata chakula, anavaa, anapata elimu, n.k na sio kuvuka mipaka.
Schoolbus nliacha kulipia maana shule ipo karibu tu kutembea ni dakika 25, kuna wenzake wanaosoma shule za kata hutembea masaa sasa mimi nikaona kwani huyu ni kilema hadi asitembee??
anajifulia,,, Zamani lilikuwa jukum la haus gel ila nikaona huu upuuzi tu, kwani mikono yake imevunjika?? mama yake alisema namtesa ila nikamkumbusha adha atayopata mtoto endapo asipokua na msaada.
anapalilia bustani ndogo .
, anafyeka nyasi (sio ombi)...Saizi silipi mtubaje kufyeka,
kutandika kitanda,...Ashazoea kabisa,
kufagia uwanja ... Hapa saus gel nae kapunguza mzigo
Zamani mchana mama yake alipendelea kumwekea ratiba apikiwe wali au chips, nikaona hayo ndio ni mapenzi ya mama hasa ukiangalia uwezo wa kumudu hivi vitu upo lakini kama baba niliingilia kati hii ishu, Saizi mchana ni ugali kwa kwenda mbele nimempiga marufuku house girl kumpikia wali au chips, Saizi ni ugali tu na hii ni kwa faida ya mtoto.
Kucheza nje na wenzake,..ni haki yake, tatizo wazazibwenye uwezo huwa tunawaona watotot wetu ni kama malaika wasicheze nje na wenzao, Nlikuwa namfungia ndani nikamnunulia Playstation kuchezea game na kuangalia katuni ila kiukweli maisha halisi sio katuni bali ni watu, japo kwa tahadhari.
Shule kwangu nataka mtoto awe na uwezo kawaida tu, kipimo changu huwa ni wastani, yeye hushika nafasi ya tano kati ya wanafunzi 30 na mimi wala sina shida kabisa, sina mambo ya kuhakikisha anashika nafasi gani, ilimradi ana wastani unaoridhisha wala sina shida, ila huo wastani asipoufikia hata awe wa kwanza hapo nina shida.
Huu ni mwaka wa pili nadhani tangu nibadili style ya malezi na sijaona anakosa chochote zaidi ya kupata vingi zaidi.
Ushauri wangu kwa wazazi wenzangu ni kwamba wazazi wenye uwezo msitumie visingizio vya sitaki mwanangu aishi shida nlizopitia huku mkivuka mpaka huo na kutengeneza mtoto ambae ni mayai mayai.
hata maua ukiyamwagilia sana maji mizizi yake huwa mifupi maana maji yapo tele ila mvua kali au upepo mkali ukipita maua yanatoka kwasababu mizizi haijaenda chini kutafuta maji kama maua yanayomwagiwa wastani tu yenye mizizi mirefu inayotafuta maji yaliyo chini hata mvua kali au upepo mkali ukipita mizizi inashikilia ua halitoki.
Miaka miwili anaanza kujifunza kula mwenyewe akifika mitatu tayari fundi.Ivi jamani mwisho wa kumlisha mtoto ni miaka mingapi?
Mazao ya awamu ya tano ndio Kama hivi wenyewe Kila kitu mtu anaona ana onewa na kutambishiwa pole mzeeSiku zingine mnapotaka 'Kujimwambafai' Kwetu kutokana na kupata 'Vipesa' vyenu vya Ngama ( Kubahatisha ) msiwe mnazunguka sana katika kutaka Kututangazia kwani wengine huwa tunawashtukieni mapema tu.
Miaka miwili anaanza kujifunza kula mwenyewe akifika mitatu tayari fundi.
Duh pole mama yake anamuona bado hawezi.Waacha..!!! Mi mbona wangu ana miaka minne na nusu saiz na bado naona analishwa kila kitu kuanzia uji mpaka chakula.?🙆♀️🙆♀️🙄🙄
Hahaaaaa!!!Hao si ndio wale mnawapaga majina ya JUNIOR, au SEAN?
Unadhani kuwinda kunguru napo ni rahisi hivyoKwa hali inavyoendelea hivi huyo mtoto utamnunulia manati aanze kuwinda kunguru
Hamna ulichojifunza?Tumefaham una uwezo haina shida
Naitikia ni vizuri sana.Wazazi wengine baadhi hawajui kulea watoto katika njia zipasazo... Huu usasa/utandawazi pia unachangia
"Mtoto mayai" unakuta hata chai kuchemsha hawezi, kujipikia hawezi, kufua, kudeki, kuosha vyombo hawezi pia
Wazazi msijisahau sana, tekelezeni wajibu wenu wa malezi, mfundishe shida na raha azijue pia akiwa mkubwa asijutie (Ajifunze kupitia changamoto zimkomaze, sina maana ya kumtesa)
Majukumu na kazi ndogondogo zitamjenga vizuri kujitegemea mwenyewe
Inasikitisha sanaNaitikia ni vizuri sana.
Unajua watu wanafikiri watoto tutakuwa nao milele, kumbe sivyo, ataondoka kwako kwenda kujitegemea. Ajifunze vitu hivuoy ni muhimu. Naamini wengine wanaodrkeza watoto wafuate.
Nimeona kwa jursni binyi smezaa akiwa nyimbani kwa mama yske. Hajui kumtinza hata mtoto wake, smemwachia mama yake amlee mjukuu. Huyu hata akoolewa sidhani majukumu ya mke ataweza kuyamudu?