Baada ya korosho, sasa zao la pamba limekosa wanunuzi nchini. Ni hujuma au ndio vita ya kiuchumi? Wanaogopa TRA kuwalundikia kodi na kuwafilisi?

Nadhani vijana watanzania mngejua kuwa hii ni fursa kwenu kwa namna yoyote msingekaa hapa kulalamika.

Hebu jiulizeni kuna kampuni ngapi za watanzania zinazojihusisha na manunuzi na uuzaji wa haya mazao ya biashara nje ya mipaka ya Tanzania kwenye soko halisi?!

Ukitazama hawa wanaoshikiria hizi biashara ni wahindi, wachina na wazungu ambao zinawapatia multimillion returns baada ya kufikisha katika soko.

Ngoojeni niwaambie jambo, hao wakulima wahafeli wala kukwama kwasababu ya TRA, serikali wala magufuri. Wanafeli sababu vijana ambao mlisomeshwa kwa kodi za serikali mnashindwa kubuni mbinu na mikakati mbadala ya kufunika hilo gepu kati ya mkulima wa Tanzania na mnunuzi aliyepo nje ya nchi. Vijana wa Tanzania especially wasomi ni disgrace hata kwa wazazi wenu sembuse serikali. Sikatai kuna changamoto za hapa na pale, figisu na viroho vya korosho tunafanyiana but hii ni kawaida popote duniani ukiwa unayatafuta mafanikio.

Leo masanja ameanzisha processing factory ya mchele na anauza mchele ukiwa kama finished product tayari kwa mtumiaji wa mwisho kuitumia. Na anamfikia hadi mteja wa mwisho. Analima hekali nyingi sana.

Kwann hamuwezi kuelewa kuwa huyu raisi wa sasa anawatengenezea platform ya kuanza kuziba magepu ya kiuchumi ambayo kwa miaka nenda rudi huwa yanazibwa na raia wa kihindi ambao wanajifanya ni raia wa tz ila ni kinafiki tu wapo hapa kuchuma na wakineemeka haooo wanakwenda ulaya kuishi?!

Hivi itakugharimu kiasi gani ukijifunza namna hilo zao la pamba linalimwa bei zake na uhitaji wake upo vipi lakini pia soko lake lipo wapi ili hawa wanaokimbia watupishe sisi tushike nafasi zetu. Si lazima uanze na manunuzi makubwa ila unaweza anza kidogo kidogo kwa kununua mzigo wa laki na hatimae utafika mamilioni.

Tuache kutumia muda kulalamika kwasababu tu tumepewa taarifa za lawama. Wakati watu wanasema wawekezaji wa korosho wanakimbia nenda katafiti nini kimewakimbiza. Mfano swala la korosho ukitazama hadi sasa serikali inatafuta wanunuzi. Na hao wanaosema wakienda wanabaniwa am telling you 100% guarantee huwa wanakuwa ni madalali wa wachina na wahindi.

These business za mazao zina hela sana tofauti na mnavyojazwa ujinga ujinga humu. Nendeni huko mashambani mkatalii mjionee uhalisia badala ya kujificha kwenye smartphone vyumbani mwenu mkisoma maneno ya kuambiwa na kujipa mastress yasiyo na lazima.

Oooh watu wanafilisika wanafeli awamu hii. Guys, juzi hapa kuna bwana mdogo analima ufuta alikuwa bandalini pale anafanya clearance ya kutoa gari yake Suzuki Grand, gari ya zaidi ya 15 million na yupo busy na kilimo cha ufuta na maharage.

Average Joe's mpo ndani tu mnalia lia uchumi mgumu na hali ngumu. Mara sijui tra wanabana. Kisa tu umeomba kazi vikampuni vitano na kadegree kako haujafanikiwa. Kisa TRA walikufuata katika flame yako na kukudai ulipe laki tano ambayo utailipa mwaka mzima.

Badili platforms, zunguka mikoa hii hakuna mtu kakufunga kamba ni pesa yako tu na jeuri ya kusafiri na namna unajipanga.

Neno la mwisho. Vijana wenzangu,huu umri ukienda haurudi. Kama vile unavyopuliza mshumaa wa keki yako ya birthday ule moto unapozima unakwenda na umri wako.

Ipo siku utashtuka ukiwa na miaka 70,bado unaishi nyumba ya kupanga, mwili umechoka unasikia kulala muda wote, hauwezi kufikiria sana tena maana kutakuwa na mabadiliko sana ya kiuchumi, biashara, technology na mengineyo. Wale watoto vichanga watakuwa ni watu wazima sasa na watakuwa ndio wapo. Katika prime age ya kutafuta. Wewe upo hapo hauna pension maana ulitumia miaka yako ya ujana kulalamika na kutukanana na watu usiowajua mtandaoni.

Lets go out there, twendeni tukafanye mipango safi na halali ya kupata pesa..... Hii hali ya sasa ya kiuchumi kama hamjajua tu ni fursa kuubwa sana kuwahi kutokea kwa vijana wa kitanzania kujiimalisha. Kwa wale waliozoea kuishi kimazoea hawataelewa na wataona nawapigia kelele ila kwa watu wenye utashi na kufikiri kwa busara watajua najaribu kuweka bayana jambo gani hapa.
mkuu umesema yote na hongera ila nakuomba tu embu jaribu kufungua ka kampuni kadogo tu ujionee mwenyewe urasimu uliopo na gharama pia ndio utajua kuwa hata nia njema ya JPM inakwamishwa na watenadaji wake.
 
Waziri wa biashara yeye yuko Dar kwenye maonyesho ya sabasaba.badala ya kuandaa kikao cha wanunuzi wa pamba mwezi mmoja kabla ya mavuno au miwili,anateuliwa anakimbia mtwara kwwnye korosho ambazo wakulima walishalipwa,waziri anatakiwa awe makini sana anapaswa kutambua mazao ya biashara na namna ya kutafuta soko la wakulima,waziri wa kilimo yeye kazi yake ni kuhakikisha wakulima wanalima na kupata pembejeo,waziri wa biashara ninkutafuta masoko ya wakulima
 
mkuu umesema yote na hongera ila nakuomba tu embu jaribu kufungua ka kampuni kadogo tu ujionee mwenyewe urasimu uliopo na gharama pia ndio utajua kuwa hata nia njema ya JPM inakwamishwa na watenadaji wake.
Napambana nao mkuu, vita ni kubwa nipo kwenye vita hapa
 
Hahaha kaka umetisha, hatuna namna inabidi tuwasujudie tu ili maisha yaendelee
Sisi wakuja tunapopambana Na watu walioushika ulimwengu tunaumia sie, mabeberu wangekuwa Na roho ya kiafrica wangetunyima condom tu ili tuangamie wote
 
Huyu anaweza kuwa afisa mwandamizi wa Bodi ya Pamba, well said. Jiwe ameshajifunza kwenye koroshoo ndo maana hajasema chochote hadi muda huu ninandandika.
Ni kweli hii ndiyo hali halisi, soko la pamba ni kama ilivyokuwa kwa korosho...

Mimi naishi Shinyanga. Pamba ndiyo zao kuu la biashara. Kwa hiyo nisemacho hapa ni kwa kuona na kuthibitisha mwenyewe....

Na ishu iko hivi;

1. Kwanza serikali iliwapangia wafanyabiashara (wanunuzi) wanunue kwa bei ya Tshs. 1,200 kwa kilo

2. Muda mfupi kabla ya msimu kuanza, soko la dunia likaelekeza vingine.....bei ikashuka

3. Wanunuzi watangaza kununua kwa bei ya kati ya Tshs. 800 na 900 pungufu ya kati ya Tshs. 200 na 300 kulinganisha na bei elekezi ya serikali na ya msimu wa mwaka jana 2018

4. Kuona hivyo, serikali ikatia mkwara na ndiyo mgogoro uliopo mpaka sasa huku wakulima wakiwa kwenye dilemma wasijue la kufanya!!

5. Kinachoendelea kwa sasa kwenye baadhi ya maeneo, wakulima wanauza pamba yao kiaina kwa aidha apokee hiyo 800 akamalize shida zake za kifedha au wanauza kwa mkopo kwa imani kuwa majadiliano kati ya serikali na wanunuzi yakikamilika, watalipwa kwa bei ya ya 1,200@kg

TATIZO LIKO WAPI?

√ Kwa maoni yangu tatizo siyo la TRA kama ulivyojaribu kusema ktk post hii...

√ TRA ni watekeleza sheria tu, kuwalaumu sina hakika kama ni sahihi. Wao hata wakiambiwa leo wasichaji chochote, they will simply do that....

√ Matatizo na lawama zote zinapaswa kuelekezwa kwa serikali chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutokuwa na Sera na mipango thabiti ya kuwasimamia wakulima wa nchi hii na masoko ya mazao yao. Kama ipo, basi itakuwa ina mashimo sana, haifai...

√ Usishangae kwenye hili yakafanyika makosa kama yalivyofanyika kwenye korosho kwa kuwa na plans za zimamoto alimaarufu za "kukurupuka" kwa malengo ya kisiasa....

√ Kwa maoni yangu, kuliko kuwaweka wakulima ktk dilemma na kuwakatisha tamaa kuendelea kulima zao hili miaka ijayo.....

Serikali kwa dharura ikubali ku - subsidize bei ya tofauti ya Tshs. 200 au hiyo 300 kwa kilo wakati huohuo ikiwa inandaa sera na mipango endelevu namna ya kulinda masoko ya mazao ya wakulima wetu....

√ John Pombe Magufuli (Mr President) asije jaribu kuingilia na sekta ya zao la pamba kwa style ile aliyoitumia kwenye korosho....

Else, it will be another disaster kwa wakulima na wananchi zaidi ya karibu milioni 10 wa mikoa ya kanda ya ziwa wanaotegemea kilimo cha pamba na pia kwa uchumi wa nchi kwa ujumla wake....

Badala yake he should better be calm when making any decisions.....

Akae na watu wake serikalini, awasikilize na kufanya maamuzi sahihi.....

Wajaribu sana kufikiri nje ya box la kisiasa na waje na sustainable solutions juu ya ishu hii badala ya maamuzi ya zimamoto.....

Serikali lazima ijifunze kutokana na makosa. Ameshavuruga na kuharibu maeneo mengi na kusabisha athari kubwa kwa wananchi wake kwa sababu tu ya "political focused high tempered decisions" anazozifanya.....

Tunamwomba kwa hili awe mtulivu. Mungu wetu yupo ni mwema na mwenye upendo mkuu kwa nchi yetu....

Kila changamoto inayokuja, basi yeye (Mungu) anakuwa ameweka na suluhu yake lakini ni pale tu tunapokuwa tunasikiliza sauti yake, kuitii na kuwa wanyenyekevu kwake...!
 
Sisi wakuja tunapopambana Na watu walioushika ulimwengu tunaumia sie, mabeberu wangekuwa Na roho ya kiafrica wangetunyima condom tu ili tuangamie wote
Kwakweli hali ni mbaya ngoja tupambane tu ughaibuni maana upepo wa kwetu hauleweki.
 
Huwa ni Furaha kuu Kwa masikini wanyonge wakisomeshwa namba maana Hakuna namna shetani hana rafiki,waliwacheka sana matajiri wakishushwa.
 
Kwakweli hali ni mbaya ngoja tupambane tu ughaibuni maana upepo wa kwetu hauleweki.
Heri kubeba box ughaibuni Lkn unaishi Na watu positive wakupe challenge ya kuendelea kuliko kuishi kwenye jamii ambayo Furaha ya kiongozi ni kuwaoneni mkiwa fukara masikini dhoofu hali wanaitwa kunyooshwa,sasa wakishanyooshwa end then? What next?
 
Hapana, sipo kabisa na hilo zao. Ila kama ulinipata vema kuna kipande nilizungumzia swala la vijana maamuzi yao kuwa influenced zaidi na taarifa za kupewa bila kujua nani alizichakata badala ya kutumia tafiti zao binafsi.

Kimsingi, mentality zetu zimelala sana. Tuna amini kila tatizo solution yake huwa inapatikana kirahisi na ni ya siku moja.

Wataka nambia hawa wachina na wahindi ambao wamefungua maviwanda huko kwao wanatagemea inputs kutoka kwetu kwamba haya mazao kwao sio muhimu katika shughuli zao.

Na kushindwa kwao ndio kushindwa kwetu. Hawa jamaa wengi wao wamefanya biashara muda mrefu sana na sasa wanadaiwa kodi na malimbikizo yake, so lazima watoke baluti. Ila wewe young business man hii kwako ni nafasi.

Wewe unadhani wao walianza na mitaji ya mamilioni at once.....?!

Na usipoanza, unategemea vipi kuendelea?!
Natamani utuonyeshe mfano kwa kwenda kunujua na kutafuta masoko ya Pam a..maana umeng'ang'ania nadharia zako hizoo mbaka Basi. Humu JF wapo hai wafanyabiashara wakubwa hizo tena wakubwa tuu..umeshaambiwa kuwa vijana na mtaji wa kukurupuka hata wewe ukipewa haiwezekani biashara hii inahitaji uzoefu na mazingira rafiki Kama Yale ya zamani. Ukiambiwa toa mfano wa mfanyabiashara anayedaiwa malimbikizo ya Kodi na TRA Hadi ameshindwa kufanya biashara ya Pamba..utatoa macho kama umekamatwa nanihinoo..


Acha nadharia na siasa hebu njoo na mkakati mwingine kuisahuri kujikwamua na hili. Sio wakati wa kulaumu kwa kutumia nadharia tumsaidie JPM katika hili.
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari TBC jana kuhusu pamba.
Kuna kampuni imeingia makubaliano ya kunua pamba yote iliyo zalishwa.

Ingawa vikundi vya wakulima wa pamba wakiomba kampuni nyingine zijitokeze kuongeza ushindani.
 
Upuuzi sana huu Wa kuropoka kitu usichokijua,msimu Wa ununuzi pamba bado,Mimi ni mkulima Wa paamba sina hofu na bei
Mkuu mwenzangu mkulima wa Pamba ndani ya Jamii Forum..😃😃😃..mtoa mada hajaropoka hata kidogo..amesema source Ni taarifa ya Habari TBC na ITV pia wameitoa..sijui unalimia Pamba Jukwaa gani hapa JF..😂😂😂
 
Back
Top Bottom