Ngisibara
JF-Expert Member
- Jan 2, 2009
- 3,298
- 2,074
PTER sielewi umri wako lakini ningekuomba usome tena historia ya zao la pamba ukianzia mwaka ilipoanza kulimwa, Kwa ufupi Pamba Tabora inalimwa zaidi Igunga, Nzega/Bukene na kidogo Uyui, Shinyanga & Simiyu naweza sema ndio namba one Kwa uzalishaji ikifuatiwa na Mwanza & Musoma...nashukuru wajerumani kwa Kulwa zao Hilo ambalo lilichangamsha sana mikoa hiyoHili nilikuwa nalitegemea sana pale Tabora.
Kwanza Tabora kiasili hawakuwa wanalima pamba ila imeletwa baada ya serikali kuharibu mfumo wa masoko ya Tumbaku na wakulima kuacha kulima zao hilo.
Pili vyama vya ushirika mkoa wa Tabora karibu vyote vimelala kwa madeni makubwa sana ambayo hayalipiki kirahisi hivyo.
Tatu wakati wanaleta zao la pamba Tabora hawakuandaa mfumo wa soko walichowahadaa wananchi ni kuwaambia walime serikali itatafuta wanunuzi jambo ambalo mpaka sasa hawajafanya.
Nne hawakufanya utafiti wa kutosha sana kwani pamba inayolimwa Tabora hata ubora haina kutokana na ardhi kutokuwa na rutuba ya kutosha na wadudu wengi sana wanaoshambulia pamba.
Kimsingi serikali iliamua kuwafukarisha wanatabora kwa makusudi ilipoharibu mfumo wa masoko ya tumbaku na kutaka tumbaku iuzwe kwa mnada kama mbuzi au kondoo.
Nchi imewashinda.