Baada ya kipigo cha newcastle: Shabiki wa man united ajiua kwa kujirusha kutoka ghorofa ya saba

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,070
2,000
[h=3]
[/h]
Kijana mmoja anayeaminika kuwa shabiki wa Manchester United Football Club amejiua jana usiku jijini Nairobi baada ya timu yake kufungwa 1-0 to Newcastle.
Polisi imesema kwamba John Jimmy Macharia, 23, alijirusha kutoka ghorofa ya 7 baada ya kujua timu yake imepoteza mchezo wa jana jioni. Kwa mujibu wa mkuu wa polisi jiji la Nairobi Benson Kibue, Macharia aliwaambia rafiki zake hawezi kuendelea kuangalia timu yake ikifungwa kila siku kabla ya kuruka ghorofani. “Mashahidi wote waliokuwepo wakati wa tukio bado wapo mikononi mwa polisi wanahojiwa,” alisema. Kibue aliwashauri vijana wa jiji la Nairobi kufahamu English Premier League ni mchezo tu kama ilivyo michezo mingine na hivyo waache kuchukua hatua za namna hii kisa michezo. Hii si mara ya kwanza kwa kwa kijana kupoteza maisha kwa ajili ya michezo inayochezwa England,” alisema Kibue.

sister

JF-Expert Member
Nov 23, 2011
9,018
2,000
Aisee pole kwa familia husika..naomba Mungu anisaidie nisifikie hatua ya kujiua kwa sababu yoyote..
 
Amiliki

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,085
1,195
Mpaka hii ligi iishe, watajirusha wengi sana. Walizoea kubebwa, sasa mwenye mbinu za kuhonga marefa kawaficha wenzie ili aendelee kuonekana kwamba yeye alikuwa bora zaidi. Kikosi ni kile kile, wachezaji ni wale wale plus Fellaini.
 
Sanoyet

JF-Expert Member
Apr 3, 2013
1,324
1,225

Man u 8-Arsenal 1
{Man u<>20bpl cups} nyambaf it's all opponents!
 
Sanoyet

JF-Expert Member
Apr 3, 2013
1,324
1,225
[h=3]
[/h]
Kijana mmoja anayeaminika kuwa shabiki wa Manchester United Football Club amejiua jana usiku jijini Nairobi baada ya timu yake kufungwa 1-0 to Newcastle.
Polisi imesema kwamba John Jimmy Macharia, 23, alijirusha kutoka ghorofa ya 7 baada ya kujua timu yake imepoteza mchezo wa jana jioni.
Each and every one of we human beings is INSANE but the degree of INSANITY differs from one person to another!
 
Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,485
2,000
Watu wanaojiua kwa 7bu za kijinga na kizembe kama hizi tena kwa mambo yasiyokuwa na maslahi kwao ningekuwa malaika wa azabu ningeongeza azabu mara 100 zaidi, mtu anajifanya ana uchungu kuliko wenye timu ama wachezaji na kocha
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,070
2,000
Watu wanaojiua kwa 7bu za kijinga na kizembe kama hizi tena kwa mambo yasiyokuwa na maslahi kwao ningekuwa malaika wa azabu ningeongeza azabu mara 100 zaidi, mtu anajifanya ana uchungu kuliko wenye timu ama wachezaji na kocha

si ndio hapo sasa,wangeanza kujiua wachezaji,kocha,wenye timu na mashabiki wa uingereza yeye angekuwa wa mwisho apo ingekuwa sawa,lakin kitendo alichofanya ata wachezaji wanamshangaa
 
fakenology

JF-Expert Member
May 3, 2012
924
1,000
kwenye mitandao ulaya kuna comments za baadhi ya mashabiki wanadai MOYES huwa anacheza kamali na ile mechi na EVATON aliweka dau kubwa hvyo ingekuwa hasara kubwa kama ingeshinda MAN .
nmeumia sana kama shabiki wa man yan anatusaliti kama ZITTO
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom