Baada ya kili stars kutinga fainali: Tufanyeje ili kombe libaki tz? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya kili stars kutinga fainali: Tufanyeje ili kombe libaki tz?

Discussion in 'Sports' started by ChiefmTz, Dec 11, 2010.

 1. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,520
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Wanajf na wapenzi wa mpira wa miguu, naamini kuwa sote ni wenye furaha baada ya ushindi wa timu yetu. Hata hivyo naamini kuwa ushindi huo hautakuwa na maana yoyote, iwapo Tanzania haitakuwa bingwa wa Tusker Challenge Cup kwa 2010. Kwa kuwa kushinda au kushindwa kwa Stars hapo kesho ni furaha au huzuni kwetu sote, Naombeni maoni yenu ya nini kifanyike ili kuhakikisha kuwa Kombe linabaki nchini. Maoni haya yatapelekwa kwa wahusika, kwa yale yatakayokuwa nje ya uwezo wetu.
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  tatizo letu ni kujadili utekelezaji BAADA..............
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280

  CHA KWANZA KABISA KUFANYIKA AOMBWE BENJAMIN MKAPA NDIO AWE MGENI RASMI KESHO, KWA SABABU YEYE NDIO ALIOUJENGA ULE UWANJA, HAKUNA NJIA MUHAFAKA YA KUMUENZI KAMA HII YA YEYE KESHO KWENDA KUTUKABIZI KOMBE LETU
  ANGALIZO, KWA WALE WALIOZOEA KUJIPENDEKEZA KWA MKWERE, KAMA WATAMUALIKA NDIO AWE MGENI RASMI BASI MJUWE KOMBE LINAONDOKA KWENDA IVORY COAST, KWA NINI? KWA SABABU MKWERE ANA GUNDU, SIO CHAGUO LA MUNGU KAMA TULIVYOAMINISHWA MWANZONI, KWAHIYO MUNGU HUJIDHIHIRISHAGA KWA VITENDO. ANAEBISHANA NA UKWELI HUU NA WAMUALIKE MKWERE KESHO, AMTAAMINI MACHO YENU. NATOA HOJA.:A S crown-1:
   
 4. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kuna mawili, Aidha tuliibe au tushinde uwanjani. Kushinda kunataka ari ya wachezaji na support ya watazamaji.
  Kuliiba rahisi, wapo wataalam wake!!
   
 5. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na Matola. JK akija tu uwanjani kombe linaondoka! Walah
   
 6. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Kwanza:kocha apange timu iliyo bora na yenye ari. Pili:kocha atumie mfumo wa 4-4-2 ili timu iwe inacheza kwa lengo la kutafuta goli,na si kujihami kwa 4-5-1. Tatu:mashabiki washangilie mwanza mwisho na wasiwazomee wachezaji (pia waache kuleta usimba na yanga siku iyo). Nne:TFF wasijifanye kuweka kiingilio kikubwa,kwani uwanja utawavundia. Tano:TFF wajitaidi kumleta BWM awe mgeni rasmi,na HASILETWE mkwere.
   
 7. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,520
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Je mwaonaje madereva Hiace, Coaster na Tax wakipeperusha bendera kuanzia leo?
   
 8. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  QUOTE=ChiefmTz;Je mwaonaje madereva Hiace, Coaster na Tax wakipeperusha bendera kuanzia leo?

  Ni wazo zuri,kwani litajenga hamasa na uzalendo miongoni mwa washabiki. Ila suala la kuzomea wachezaji lisijitokeze uwanjani.
   
 9. S

  SWADO Member

  #9
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabisa lazima tuisapoti timu yetu kwa kuishangilia kwa nguvu muda wote wa mchezo, TFF wapange kiinglio ambacho watanzania wengi watamudu kulipa, pia wachezaji wajitume na waweke uzalendo mbele hapo kombe lazima libaki tz, Swala la nani kuwa mgeni rasmi ni imani tu halina mantiki hata akiwa nani wachezaji wakijituma kombe litabaki tu.
   
 10. S

  SWADO Member

  #10
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kili stars hoyeeeeeeeeee hope kombe litabaki home tujitiokeze kwa wingi kesho ili kuwapa moyo wachezaji big up sana kocha
   
 11. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hatuwezi kuchakachua matokeo? Tuwaombe nec watusaidie
   
 12. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,520
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Tumejiandaje na hujuma za CECAFA? Kwani yawezekana members kama Uganda are not happy na wanaweza kuja na hoja ya tukose wote
   
 13. Kilakshari

  Kilakshari JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mmmh! Wabongo tuna mambo.
   
 14. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,520
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Kila saa tunafikiria siasa tu hata kwenye mambo yasiyohusika.
   
 15. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  .........nafikiri kuna ile kanuni ya CECAFA kwamba mgeni mualikwa (in this time Ivory Coast, malawi na zambia) hawezi kubeba Kombe hata kama akishinda hivyo kama kanuni hito bado ina-hold then matokeo yoyote ya kesho, kombe linabaki Tanganyika (sio Tanzania)
   
 16. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #16
  Dec 11, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,520
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Lakini ubingwa utanoga zaidi kama tukishinda
   
 17. M

  Matarese JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Enhee, kula tano Afande, hilo ndiyo neno, tuwakodi NEC wachakachue matokeo hata tukifungwa labda 2-0, tunageuza ubao wa matokeo usomeke tumeshinda labda 2-1 au 1-0.
   
 18. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #18
  Dec 11, 2010
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,812
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  ni mechi ya kukamilisha ratiba, KILIMANJARO BINGWA TAYARI
   
 19. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #19
  Dec 11, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tuwe Makini katika Kuteua Mgeni Rasmi
   
 20. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #20
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,035
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Kwani sheria za mpira hazifanani na za NEC? kwamba mtangazaji akikosea akasema KILIMANJARO imeshinda hakuna wa kubisha hata mahakamani
   
Loading...