Baada ya kikao na Maseneta kuhusu North Korea, Marekani yashindwa tena kuamua kuishambulia

msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,761
5,877
Marekani Yashindwa Tena kuamua Kuishambulia North Korea Na Kuendelea Kusisitiza Kuhusu Vikwazo.

Mamlaka ya rais Donald Trump imewaelezea maseneta wote 100 wa bunge la taifa hilo kuhusu tishio la Korea Kaskazini na kubaini mikakati ya kuishinikiza Pyongyang kupitia vikwazo vya kiuchumi na vile vya kidiplomasia.

Lengo ni kuilazimu Korea Kaskazini kusitisha mpango wa makombora ya masafa marefu pampja na ule wa Kinyuklia.

Mwandishi wa BBC mjini Washington anasema kuwa mkakati muhimu pia utakuwa kuirai China kuishinikiza Pyongyang.

Seneta mmoja alisema kuwa habari hiyo kuhusu Korea Kaskazini ilikuwa muhimu sana.

Taarifa iliotolewa kwa niaba ya wizara ya Ulinzi na ile ya kigeni ilisema kuwa Marekani bado itaendelea na mazungumzo lakini imejiandaa kujitetea pamoja na washirika wake.

Awali kamanda mkuu wa Marekani katika eneo la Pacific alitetea kupelekwa kwa mfumo wa silaha za kisasa nchini Korea Kusini.

Hali ya wasiwasi imepanda huku kukiwa na hofu kwamba Korea Kaskazini inapanga kujaribu makombora mapya.

''Marekani inataka uthabiti na kutoenea kwa silaha za kinyuklia katika rasi ya Korea'', ilisema taarifa ya pamoja iliotolewa na waziri wa maswala ya kigeni REx Tillerson, waziri wa Ulinzi Jim Mattis na Mkurugenzi wa maswala ya ya ujasusi Dan Coats.


Chanzo: BBC Swahili
 
Wanakumbukumbu mbaya sana na vita vya Vietnam.
Walipigwa hadi wakaanza kubeba RAIA mitaani wakapigane vita
Wakataka mbeba Mohamed Ali, akawaambia nikapigane na mvietcong wakati hajawai nislave wala kuninyanyapaa, wakamfungulia kesi na kumpokonya mataji yake, akashinda kesi akakimbilia London.

Washenzi sana hawa, wacha wamchokoze mkorea, awatumie li nuclear missile likifika anga ya marekani lisplit into several mini nuke missile, tuone watadaka mangapi, shenzi
 
Shida sio kua mvumilivu shida haiwezkorea.wamarekan wanamitambo narada zakisasa kabisa lazima watakua wamefanya utafit nakubain yule kijana yuko vizur.hivo sio kwamba anapenda kukaa kimya bila kumpiga bali hawez kumpiga yule mtt.atampa hasara kubwa sana marekan amewekeza sana japan na korea ya kusin uchumi wake utaporomoka
 
Hahahahabaa marekan ni muoga sana ukiona amepigana ujue keshajua huyu ana kitu kabisa kama alibyofanya kwa sadam au afghanistan taifa masikin na halina silah zaid ya ak47 na tumakombora twa kuangulia boing hatta vifaru hawana
 
UKWELI NI KWAMBA KOREA KASKAZINI NI TAIFA DOGO MBELE YA MAREKANI NA MAREKANI AKIAMUA KUISHAMBULIA KOREA ATAISHAMBULIA TUU.

LAKINI MAREKANI HAWEZI KUBAKI SALAMA KWA SABABU. DOGO ANA UWEZO KUIVURUGA MAREKANI VIBAYA MNO NA MWISHO ,......
 
Shida sio kua mvumilivu shida haiwezkorea.wamarekan wanamitambo narada zakisasa kabisa lazima watakua wamefanya utafit nakubain yule kijana yuko vizur.hivo sio kwamba anapenda kukaa kimya bila kumpiga bali hawez kumpiga yule mtt.atampa hasara kubwa sana marekan amewekeza sana japan na korea ya kusin uchumi wake utaporomoka
Ndo maana N korea walisema hawana cha kuloose ila marekani kawekeza sehemu nyingi anaweza loose sehemu kubwa sana na anaweza kuyumba kiuchumi sana..
 
Back
Top Bottom