Poleni sana Watanzania wenzangu kwa kuondokewa na Rais wetu kipenzi. Mungu amlaze mahali pema peponi, Amina.

Kutokana na hali ilivyo, automatically Mama Samia aliyekuwa Makamu wa Rais ndo anakuwa Rais kamili kwa kipindi cha miaka minne iliyobaki.

Je, nani anayefaa kuwa Makamu wa Rais ukizingatia kuwa lazima atoke Bara kwani Mama Samia ametokea Zanzibar?

Mimi binafsi nahisi Mheshimiwa January Makamba anafaa sana kuchukua hiyo nafasi ukizingatia ameshafanya kazi kwa karibu na Mama Samia kwa muda mrefu kipindi akiwa Waziri.

R.I.P Magufuli.
Suala la dini kuwa moja na Rais na Waziri Mkuu litakuwa kikwazo kwa January, japo nami naona angelifaa sana.
 
Itapendeza ,kufumba macho ,kubadilisha baadhi ya vifungu , makamu atoke vyama vya upinzani ikiwa ni pamoja kuvunja bunge , namanisha uchaguzi wa wabunge na madiwani urudiwe upya.

Lengo kuleta mshikamano wa kitaifa, hata huwe malaika kuongoza nchi ikiwa imagawanyika ni ngum Sana, wazee ,wastahafu kutoka CCM, hapa simameni imara kwa maslahi mapana ya taifa.

Acha bangi inakuharibu.
 
Nasikia Wasukuma wanataka hiyo nafasi kwa udi na uvumba. Waziri wa ujenzi ndio chaguo lao ikishindikana basi hata Askofu Rashid au Makonda.
Kuliko turudushwe tena kwenye aliyepasua nchi kwa ukanda na ukabila bora tuongozwe bila makamu tubaki na mama anatosha sana. Msituletee tena maumivu ya kutugawa watanzania. Imetosha.
 
1. Jakaya Mrisho Kikwete, apewe umakamu wa rais

2. Butiku

3. Kimei

4. Kinana

5. Warioba

6. Prof Muhongo

7. Makinda

7. Mwamunyange

8. Lissu

9. Chikawe

10. Mwandosya

Hao akina January, mwigulu sijui kabudi bado sana. Anatakiwa mkongwe na mwenye busara ya kumwongoza mama kuliweka taifa pazuri

Lissu 🤣. Kwa kutumia katiba gani?
 
Balozi Mahiga alifariki tar 1 May 2020, kesho yake tar 2 May Rais akamteua Nchemba kuziba hiyo nafasi (kabla hata ya mazishi).

Naamini huko Magufuli aliko, angependa tumuenzi kwa kuziba nafasi hizo haraka sana tena kabla ya mazishi.
Alikuwa hampendi kabisa. Chuki ya wazi. Yasni Aisee ngoja tunyamaze. Ninakumbuka jinsi pia mke wa Mahiga alivyodhalilika? Acha tusifukue makaburi maana ni mengi mno.
 
Kangi lugola aliyemtaka Mungu kumshukuru magufuli.

Kweli ccm ni chama cha kishetani
 
Poleni Watanzania kwa msiba mzito,lakini nchi itaendelea na maisha lazima yaendelee.

Kwa mujibu wa katiba sasa Rais ni mama anatokea Zanzibar na makamo anapaswa atokee bara.

Mzee kabudi anafaa kwa nafasi hiyo, tunaomba CCM mlifanyie hili kazi.
Hafai hafai. Sipendi watu wanaotolewa majalalani mimi.
 
Tuanze na rais kwanza kabla ya makamo. Rais anayefaa kuiongoza Tanzania ni Tundu Lissu tu
 
Back
Top Bottom