Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ndamo emmanuel, Sep 21, 2012.

 1. n

  ndamo emmanuel Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 12, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ilikuwa Jumapili ya tarehe 9 Dec 2011 saa kumi na mbili asubuhi, nilikuwa nikitembelea bustani iliyoko nyuma ya Nyumba yangu. Miguu yangu ilipata mshituko wa ghafula niliposhuhudia jambo hili lililonikosesha amani, hadi nikaamua kuomba maoni kwa wasomaji wenzangu ili kupata nini hasa maana ya nilichokiona. Nilisikia mshindo mkubwa uliotokana na mwanguko wa kitu fulani kutoka katika mti mkubwa wa Mzambazau uliokuwa karibu yangu! Nilipotazama mbele yangu, nilimwona kinyonga aliyepasuka tumbo huku mayai yakitapakaa mahali pale, na alikuwa katika hatua za mwisho wa uhai wake. Mengi ya mayai hayo, yalikuwa yamepasuka yakiwa na mchanganyiko wa chembe za damu na ute mweupe kama wa yai la kuku lililoanza kutunga kifaranga! Wazo liliniijia kichwani niangalie kwa umakini zaidi,kwa maana niliwahi kusimuliwa na babu yangu kuwa kinyonga jike akipata mimba na mimba ile ikikua na kufikia muda wa kuzaa, kinyonga huyo hupanda mtini, juu kabisa ya matawi akaangalia chini na kulenga palipo na jiwe kubwa, au sehemu iliyo ngumu na akajiachia kutoka kwenye matawi ya mti huo. ili aangukiapo mwamba huo, tumbo lipasuke ili mayai yaliyokomaa tumboni mwake yapasuke vilevile ili watoke watoto walio hai baada ya yeye kufa, maana tumbo lipasukapo na uhai wake hufikia mwisho! Baada ya uchunguzi uliodumu kwa zaidi ya nusu hivi, ndipo nilipogundua yafuatayo: 1.Mzoga wa Kinyonga yule ulikuwa na mchanganyiko wa rangi ya KIJANI na MANJANO! 2. Kinyonga Yule mayai yake yalikuwa hayana dalili yoyote ya kukomaa, hivyo kupoteza matumaini na bahati nadra ya kushuhudia tukio la mwanzo wa maisha ya Vinyonga wengi watoto, walio matokeo ya mwisho wa maisha ya kinyonga jike mama yao! 3.Kifo cha kinyonga yule kilitokana na ajali baada ya kukatika tawi la mti lililoonekana pembeni kidogo ya mzoga ule! Nilikumbuka siku ya mdahalo ulioandaliwa na kituo cha katiba UDSM, mwezi mmoja kabla ya Rais kuridhia uandikwaji wa Katiba Mpya, Mchangiaji wa mwisho kabisa katika mdahalo huo Uliorushwa na kituo cha I.T.V, alikuwa mzee niliyemkadiria umri wa miaka 80 hivi, Na alisema yafuatayo………''Ili kinyoga aweze kuzaa na kuendeleza kizazi, lazima afe kabla ya watoto wake kuanza maisha.'' Akamaliza kwa kusema ‘’SITAKUFA HADI NITAKAPOSHUHUDIA KIFO CHA C.C.M’’ Niliondoka kwa huzuni bustanini, huku nikibaki na maswali mengi kadhaa yasiyo na majibu! Baadhi ya maswali yaliyokuwa yakipita kichwani mwangu ni kama yafuatayo! Nilijiuliza kuwa, Ikiwa kupasuka kwa tumbo la kinyonga yule yalikuwa ni maono juu ya kufa kwa C.C.M, Je mbona nisione mayai yakitoa watoto wa kinyonga kama ilivyo ada? Nini kitatokea ikiwa C.C.M itakufa na Isipate mrithi wa kuendeleza kizazi? Na ikiwa Mama atakufa na watoto tumboni, Nini Itakuwa Mustakabali wa kizazi kijacho kama sio GIZA? IKIWA MSOMAJI MWENZANGU UTAFIKIRIA MAONO JUU YA MAANA HALISI YA KIFO NA MATOKEO YA KINYONGA HUYU ‘’WA KIJANI NA MANJANO’’ KWA MUKTADHA WA KISIASA NCHINI TANZANIA, NISAIDIE KUBORESHA TAFSIRI YA MAONO HAYA. NOTE: NO PART OF THIS ARTICLE SHOULD BE REPRINTED NOR REPRODUCED FOR BUSINESS USES OTHER THAN IN JAMII FORUM WITHOUT PRIOR CONSENT OF THE AUTHOR. THANK U 0759-069406
   
 2. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Jameni hata kama tunaichukia ccm lakini hatuna budi ku stick kwenye mipango, masimulizi na strategy zenye kuzalisha fikra chanya, hizi simulizi nadharia tuwaachie sekondari, jiulize wewe mwenyewe baada ya kumshuhudia kinyonga mfu, hukuona cha mtoto wala watoto wakitokea kwenye huo mzoga
   
 3. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Nmependa simulizi ya kinadharia. Hao watoto sasa..hmm na iv knyonga hazai bata..hatuna budi kuwaangamiza vinyonga watoto..
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,599
  Likes Received: 18,608
  Trophy Points: 280
  Maadam kinyonga huyo alikufa kwa ajali ndio maana hukuona watoto!. Kinyonga halisi ni reptilia kwanza huyaga mayai, kisha huyameza for gestation period yote na hali kitu na mayai hayo huangulia tumboni akiwa bado hai na yakishaangua ndipo hujitupa tumbo kupasuka na watoto kusambaa!.

  Huyu kinyonga halisi aliyepo hafi kwa sababu hata hayo mayai ya kumeza hayapo!. 2015 ataendelea kudunda only if watamsimamisha mgombea wangu fulani! hivyo ulichoshuhudia ni ajali tuu ya masikini kinyonga na wala sio maono yoyote!.
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Ni coincidence tu hiyo, ila hata kama usingemwona huyo kinyonga ni wazi kuwa ccm kwa heri
   
 6. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Huyo kinyonga wa kijani na manjano atakufa na mayai yake
   
 7. d

  dotto JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  HAta kama vinyonga wengine wadogo wanegetokea kungekuwa na mwewe wa kuvimeza vizionekane tena. Ni hatari kuwa na vinyonga wa rangi hiyo.
   
 8. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,729
  Likes Received: 8,312
  Trophy Points: 280
  Hahahah...leo nimeujua msimamo wako!
   
 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Haya kapitie posho yako pale KINONDONI MTAA WA UFIPA sisi tunasonga mbele na ujenzi wa taifa letu.
   
 10. G

  Ginner JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 1,139
  Likes Received: 263
  Trophy Points: 180
  kutokana na uelewa wangu mdogo, nimeelewa ya kwamba....kinyonga wa kijani na njano alianguka toka juu ya mti na kufa (ni kwa ajali ya kuvunjika ka tawi la mti na sio kuwa wakati wake muafaka wa kuzaa watoto kuwa umefika)

  baada ya mama kupoteza uhai, mayai yaliopasuka yenye chembe za damu yalitapakaa kila mahali katika eneo lile...( kwa mtizamo wangu ni utitiri wa vyama vya siasa vilivyopo ambavyo vingine ni vichanga vinavyokusudiwa kuwa mrithi wa mama na kuendelea na maisha ya kila siku)

  "lakini baada ya uchunguzi wa kina wa muda zaidi ya nusu saa , ikagundulika kuwa yale mayai hayakuwa yamekomaa kuweza kufanya vile vichanga kuendelea kuishi baada ya kifo cha mama yao (hapa nimeelewa kwamba...kwa mtu atakae tumia muda mwingi kutafakari, kufanya uchambuzi yakinifu, na utafiti wa kutosha.. haita mchukua zaidi ya nusu saa kwa yeye kutambua kwamba vyama vilivyopo bado havina uwezo wa kendeleza gurudumu hili la maisha kwa vile havijakomaa bado na wakati wake haujafika kwa wao kujitegemea na kuitegemeza nchi kwa ujumla)

  hiyo ni tafakari yangu ndogo tu na sio ya mleta mada. kwa maana na mimi nimeaminishwa kuwa maana ya neno ipo kwa mpokeaji wa neno na sio mtamkaji.
   
 11. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Natafakari kwa kina
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Nani huyo??
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hadithi nzuri sana, lakini siku nyengine jaribu kutenganisha aya katka maandishi yako ili iwe rahisi kwa wasomaji, vyengine mtu analazimika kurejea mstari huo huo mara tatu.

  Hapo nyekundu, hicho kishindo kikubwa kilitokana na uzito wa kinyonga au na mpasuko wake?

  Na blue je, mbona ghafla umetuwekea Kidhungudhungu?
   
Loading...