Baada ya Kibanda:POLISI wajeruhi Mwandishi Mwingine wa Habari


WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Messages
4,225
Likes
8
Points
135
Age
40
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2011
4,225 8 135
WANAJAMVI:

KUNDI la Askari polisi wapatao 10 wa kituo kikuu cha Polisi Geita wamemjeruhi vibaya Mwandishi wa Habari wa Redio Free Afrika Mkoani Geita Salum Maige baada ya kumshambulia kwa magumi na Mteke.

Mwandishi huyo kwa sasa amelezwa wodi namba mbili katika hospitali ya wilaya ya Geita akiendelea na matibabu ambapo ameumizwa jicho la kushoto,kwa mujibu wa daktari aliyemfanyia uchunguzi mishipa mingi ya kichwani imepasuka hali iliyosababisha jicho lake kuvia damu kwa ndani!

sababu za kumkamata Mwandishi huyo kwa mujibu wa polisi ni baada ya kwenda kulalamikiwa na mkewe katika kituo cha polisi kutokana na mgogoro wao wa ndoa.

Polisi walimfuata wakamkamata na kumtia pingu kisha kumtupia ndani ya gari na kuanza kumshambulia,mbaya zaidi hata jalada alikuwa bado hajafunguliwa polisi.

Polisi walikataa kumpatia PF3 kwa ajili ya kwenda kupata matibabu,hadi jana ambapo waandishi wenzake baada ya kupata taarifa waliandamana hadi polisi na kudai apatiwe PF3 na kumpeleka kupata matibabu.

Hata hivyo tukio hilo limewaacha na maswali mengi wananchi pamoja na waandishi wenyewe wa mkoa wa Geita kwamba ,Je?.mgogoro baina ya mwandishi huyo na mkewe ilikuwa ni sababu tosha za yeye kukamatwa na zaidi ya polisi 10,tena wakiwa na silaha na kumtia pingu?!

Pili kwa nini polisi wamshambulie na kujeruhi vibaya mwandishi huyo kiasi cha kupelekea kulazwa hospitalini,na hasa ikizingatiwa kwamba mwandishi huyo ni miongoni mwa waandishi ambao wamekuwa wakifichua uovu unaofanywa na jeshi la polisi mkoani Geita.

Miongoni mwa maduu ya polisi aliyowahi kufichua katika siku za hivi karibuni ni polisi kudaiwa kumuua mfanyabiashara wa dhahabu geita kwa risasi na kisha kumpora zaidi ya shilingi milioni 300,polisi kumuachia mtuhumiwa aliyekuwa anakabiliwa na tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi baada ya kutoa rushwa ya shilingi milioni 2.

CHANZO:MIMI MWENYEWE,nimezungumza na Mwandishi huyo mwenyewe,nimezungumza na Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Geita Pudensiana Protas,nimezungumza na Daktari anayemtibu Mwandishi huyo,na Nimezungumza na baadhi ya waandishi wenzake wa Mkoa wa Geita.nitaendelea kuwajuza kadri nitakavyokuwa napata taarifa kutoka huko Geita.
 
Domy

Domy

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
4,701
Likes
12
Points
135
Domy

Domy

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
4,701 12 135
Huyo mwanamke ni zaidi ya Shetani,mambo ya ndoa atapelekaje polisi...... Yawezekana anatembea na mmoja wa askari hao,Pole Salum mkeo amekuponza.
 

Forum statistics

Threads 1,250,713
Members 481,465
Posts 29,742,876