Baada ya kesherehekea miaka 50 ya Tanganyika isiyokuwepo tutafakari kuiunda upya kwa kutumia katiba

nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
4,281
3,243
Baada ya kumaliza kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa iliyokuwa Tanganyika...huu ni wakati muafaka wa kutafakari kuiunda upya Tanganyika kwa kutumia fursa pekee tuliyo nayo ya katiba mpya inayokuja.

My takes on the matter:
  • Ifike mahali watawala wetu wafungue nafsi na nyoyo zao na kuona umuhimu wa kuwepo kwa serikali (nchi)ya Tanganyika kama ilivyo kwa uwepo wa serikali(nchi)ya Zanzibar.
  • Watawala wetu wafike mahali waelewe kuwa mabadiliko ya kisiasa hayakwepeki (siasa ni dhana dynamic na siyo static) na ni fursa mojawapo kwa nchi kujizatiti katika kujitaftia maendeleo.
  • Ifike mahali watawala wetu waelewe na waamini kuwa uwepo wa serikali (nchi)ya Tanganyika ni mojawapo ya mabadiliko ya kiutawala tu na si kuvunjika kwa muungano uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar kama ilivyo hapa chini:
  • Sioni kutakuwa na tatizo gani endapo kutakuwa na serikali (nchi)ya Tanganyika katika Tanzania wakati tayari kuna serikali (nchi)ya Zanzibar katika Tanzania.
  • Sioni kutakuwa na shida gani endapo kutakuwa na rais wa serikali (nchi) ya Tanganyika wakati tayari kuna rais wa serikali(nchi) ya Zanzibar katika Tanzania.
  • Sioni kwanini kusiwe na katiba ya Tanganyika wakati tayari kuna katiba ya Zanzibar.
  • Sioni kutakuwa na shida gani kama kutakuwa na bunge la Tanganyika wakati tayari kuna bunge la Zanzibar.
  • Sioni kutakuwa na shida gani kama kutabaki kuwa na rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania (kama ilivyo sasa) atakayeziongoza serikali 2 za Tanganyika na Zanzibar kwa yale mambo ya muungano tu.
  • Sioni kutakuwa na shida gani kama vilevile kutabaki kuwa na bunge la muungano la Tanzania (kama ilivyo sasa) litakalosimamia mambo ya muungano tu.
  • Sioni kutakuwa na shida gani kama kutakuwa na katiba ya jamhuri ya muungano ya Tanzania(kama ilivyo sasa)itakayosimamia yale mambo ya muungano tu.
  • Sioni kutakuwa na shida gani kama watawala wetu watachukulia suala la uwepo wa serikali (nchi)ya Tanganyika kama suala la mabadiliko ya kiutawala tu na si vinginevyo (muungano na nchi ya Tanzania vinabaki pale pale).
Maswali ya kujiuliza:

  • Kama watawala wameweza kufanya mabadiliko mengi makubwa yanayohusu mustakabali wa taifa bila kigugumizi iweje hili la Tanganyika linakuwa shida hata kulijadili?????tuangalie mifano hii:
  • Kama watawala wameweza kuua ujamaa na kujitegemea tulioachiwa na Nyerere vipi hili la uwepo wa Tanganyika liwe nongwa hata kulijadili??
  • Kama watawala wameweza kuua azimio la arusha bila hata kigugumizi(na hatimaye kuachia raslimali za nchi zikiporwa na wageni) leo iweje suala la uwepo wa Tanganyika liwe gumu kujadilika?
  • Mbona watawala wameweza kugawa mikoa na wilaya za Tanzania na kuanzisha mikoa na wilaya mpya???
  • Mbona Zanzibar wameweza kujitengenezea nchi(serikali) ya umoja wa kitaifa tena kwa kupitia katiba mpya na referendum?????kama Zanzibar imewezekana vipi Tanganyika ishindikane????
  • Mbona watawala walikubali uwepo wa vyama vingi Tanzania pamoja na kwamba asilimia 80% ya watanzania walikataa???kwani kumekua na tatizo gani mpaka sasa?
Tutafakari.......
 
Back
Top Bottom