Baada ya kenya,sasa Zimbabwe,Je Tanzania Inawezekana??

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
162
Heshima Mbele,
Jana wakati naangalia Kipindi cha straight Talk Africa katika VOA,nilipata kumsikia Mwandishi wa gazeti la Herald la Zimbabwe(obi_ ambaye alikuwa akimtetea sana Mugabe,hata kama wanachi ambao hawamtaki.akitoa sababu ya wapinzani kupewa pesa na nchi za ulaya ili amng'oe Mugabe.wanachi wengi hawajagundua hili suala ila Mugabe ana nia Njema na Wazim,Mugabe anakataa sabbu hakuna mtu wa kumuachia nchi.

Nilitafakari sana kuhusu hili na kugundua kwamba Itakuwa ni vigumu kwa Mugabe Kuachia nchi kwa Morgan sababu hata jeshi la nchi hiyo limekataa kuhusu hili.Baada ya kutazama sula la kenya pia,ni kwanini Mwai Kibaki alikataa kumrushusu Odinga kutawala ile nchi.

Nimeshagundua ni kwanini ni vigumu kwa vyama vya Upinzani kushinda na sasa nimeshagundua kwanini CCM walikuwa wanasema Wapinzani wakipewe nchi itatokea Vita.Wapinzani hawaaminiki na 'system' hata kidogo sababu ni watu wa kukurupuka.

1.Wapinzani wengi ukiondoa CUF,wanaongozwa kwa emotional za watu ambao ni viongozi wa juu wenye tabia ya kupenda sifa nakujikweza na vimekuwa vikidhaminiwa na nchi za ulaya kuendesha shughuli zao.Hili suala ni la kukaribisha Neo-colonialism katika nchi za Afrika.

2.Napenda Wapinzani wapewe sana madaraka ila sioni watu wakutengeneza timu ya kuongoza labda kama vyama vyote viungane na kama CCm ikimeguka.ila upiznani kama upinzani kwa TZ bara ni vigumu kwa chama chochote kushinda mpaka watakapojenga umoja wa kitaifa.bali kwa Zanzibara naamini CUF imekomaa na ianwatu wanofaa kuongoza na muda umeshafika watakabidhiwa Zanzibar.

napenda kuhitimisha kwa kusema,Chama cha upinzani ni kimoja tu na ni CUF,naomba vyama vingine viungane nacho kuikabali CCM
 
Umechemka. Si wapinzani tu ambao ni wakurupukaji bali CCM pia. Kama huamini fikiria maamuzi mangapi serikali ya CCM imefanya kwa kukurupuka na huwa inayajutia baadae. Ni suala la kukubali kuwa hakuna aliyezaliwa atawale milele. Kuna siku CCM itakuwa chama cha upinzani, japo sijui ni lini. Natumaini utaendelea kusema 'wapinzani ni wakurupukaji'.
1.Wapinzani wengi ukiondoa CUF,wanaongozwa kwa emotional za watu ambao ni viongozi wa juu wenye tabia ya kupenda sifa nakujikweza na vimekuwa vikidhaminiwa na nchi za ulaya kuendesha shughuli zao.Hili suala ni la kukaribisha Neo-colonialism katika nchi za Afrika.
Kwanini unawaondoa CUF? Unataka kusema hao mshaelewana? Au ukiongelea wapinzani unamaanisha watu gani?

2.Napenda Wapinzani wapewe sana madaraka ila sioni watu wakutengeneza timu ya kuongoza labda kama vyama vyote viungane na kama CCm ikimeguka.ila upiznani kama upinzani kwa TZ bara ni vigumu kwa chama chochote kushinda mpaka watakapojenga umoja wa kitaifa.bali kwa Zanzibara naamini CUF imekomaa na ianwatu wanofaa kuongoza na muda umeshafika watakabidhiwa Zanzibar.
Zanzibar si kama CUF imekomaa, inashindwa nini bara? Think big! Kuna zaidi ya hapo. Mwenzio Shy anawaona CUF kuwa chama cha waasi. Mnatofautiana? Tukubaliane taifa hili linahitaji mabadiliko makubwa katika siasa zetu ili tupunguze kero kubwa za watanzania. Inawezekana hata kupitia CCM lakini si kwa kukitanguliza chama badala ya taifa. Naamini CCM ina watu wengi wazuri lakini wachache wabovu huwameza hao wazuri.

napenda kuhitimisha kwa kusema,Chama cha upinzani ni kimoja tu na ni CUF,naomba vyama vingine viungane nacho kuikabali CCM
Uko upande gani? CCM au CUF? Kila chama kinachokuwa na hoja pinzani dhidi ya chama kilicho madarakani kwangu nakiona chama cha upinzani. Siku CCM wakiwa si chama tawala basi nao nitawaita chama cha upinzani na endapo hao unaowapigia debe (CUF) watakuwa madarakani basi mkuu uta-enjoy sana.
 
Back
Top Bottom