Baada ya kauli ya Mzee Kikwete ningekuwa Mbunge wa Mbeya ningefanya haya

Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
3,108
2,000
Kwa nini wasibomoe wajenge nyumba Nzuri na za kisasa!

Acha kutetea ujinga! Watu wa Mbeya badilikeni mtaendelea kuwa nyuma kila siku kwa u shamba wenu
We unadhani wanabomoa bila utaratibu mkuu.

Baadhi ya maeneo yameshaboreshwa na bado yanaendelea kuboreshwa. Kwa akili zako unadhani unaweza wakimbiza watu kwa siku moja tu.

Tatizo lako we jamaa ushakalili kua jiji ni maghorofa na majumba mazuri tu. Hayo mambo yanafanywa taratibu hapa jijini, ukienda leo mbeya ni tofauti na ile ya mwaka jana. We unabwabwaja wakati mbeya umeenda 2013 tena umepita tu na sio kuishi.

Usikalili mkuu za kuambiwa changanya na zako.
 
Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
9,065

Mbeya nakuja sana! Mwaka huu nimekuja Mbeya zaidi ya mara 10 na Mara ya mwisho ilikuwa mwezi Novemba juzi tu
 
Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
3,108
2,000
Mbeya nakuja sana! Mwaka huu nimekuja Mbeya zaidi ya mara 10 na Mara ya mwisho ilikuwa mwezi Novemba juzi tu
Sio kweli, kama unakuja mara nyingi nisingetemea povu lako hilo ilhali mbeya bado inaendelea kubadilika kila leo.

Sio mmoja kati ya miji inayojengeka kwa kasi, unajengeka taratibu tu ila mbeya ya mwaka jana si ya mwaka huu vivyo hivyo hadi mwakani mwezi kama huu mambo mengi yatakua yashabadilika.

Au unataka uamke kesho tu ukute kila unachokitaka kipo.??
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
9,348
2,000
Heka 500 ni Chache nina mashamba zaidi ya hekari izo kwa chuo barabara majengo ni eneo la kawaida
Kutoka krampus moja had nyingine ni trip like University of dodoma nazan unaona kinavyo contribute uchumi wa watu wa Dodoma so watu wa Mbeya changamkenibmkishindwa sisi Tabora tunakitaka
Kujenga campus tu huwezi kuhitaji eneo lote hilo, labda wanataka kujenga University of Mbeya (UMB) badala ya UD......
 
griffin griffith

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
549
500
Mtoa mada umesahau kusema Mbeya walichokufanyia. Ninawasiwasi mtoa mada umeoa Mbeya kama hujaoa Mbeya basi kuna ndugu yako kaoa Mbeya na amebanwa haswa.

Binafsi nakupenda Mbeya kwasababu zifuatazo.
1. Mbeya kuna hali ya hewa nzuri ambayo hata mgeni kutoka ulaya lazima aipende.
2. Mbeya kuna vyakula vingi vitamu na vya kila aina na vya bei ndogo.
3. Mbeya kuna mazingira mazuri ya kusomea
4. Mbeya unakunywa maji ya kisimaMbeya unafulia maji ya kisima.
5. Mbeya ukiagiza chakula hotelini maji ya kunywa unamiminiwa kutoka kwenye majagi maalumu. Na hayo maji yanachotwa kwenye ndoo tu.

Japo naishi Dar ila huwa napenda sana ningeishi Mbeya. Dar kuna mbu sana mpaka kero nyieee, Dar unalala ndani ya chandarua. Dar maji ya kunywa ni shida, Dar maji ya kufulia ni shida, Dar maji ya kuoga ni shida.

Hii ndio imenipa akili ya kuanza mkakati wa kufungua kiwanda cha Kuchukua maji ya bahari ya Hindi na kuondoa chumvi, ili kupata maji safi na salama. Lakini pia kuna vimashine nitawauzia wakazi wa Dar es salaam waliochimba visima vyenye maji ya chumvi, vitakua vinatumia solar kutoa chumvi kwenye maji ya kisima. Sasa wakazi wataweza kupata maji ya kunywa, kufulia na kuoga majumbani mwao.

Hujajibu hoja, tuache ushabiki wa ajabu na uzalendo fake!

Chuo hiki kikija mbeya kitaichangumusha mbeya kwa fursa mbali mbali
 
Bondinear

Member
Jan 29, 2021
48
125
Wapewe ? Kwa nini wasinunue? Bila ya kubadilisha hii sera ya kijamaa kwamba ardhi haina thamani hatuwezi kuondokana na umaskini. Yaani mtu anatamka kabisa apewe ekari 500 wtf ?

Ni lazima ardhi yetu iwe na thamani, turuhusiwe kumiliki Ardhi ndiyo tutaondokana na umaskini na hatimaye kujikomboa kwangu mimi mtu anaposema apewe ardhi ina maana kuna ardhi haina mtu wala matumizi imekaa tu inasubiri kugawiwa mtu, tunaishi ujima bado.
Kumbuka kuwa kitu kinachowekezwa ni kwa manufaaa ya jiji la mbeya, hapo inajengwa hospital ya kisasa humohumo chuon, mzunguko wa pesa utaongezeka, wawekezaji wataongezeka, harafu ni chuo cha serikali sasa nan aiuzie serikali ardhi?????... Mi nmchanaga live tulia ackson ig huko ni upuuz huo, watoe ardhi mbeya ipo waz saaana
 
Bondinear

Member
Jan 29, 2021
48
125
Izo picha Mbona zinaweza tu kutengenezwa!

Kawafundisheni watu wenu namna gani ya kujenga bora na kupangilia miji yenu! Acheni pia ushirikina na kutopenda maendeleo ya wenzenu
Aiseee tunashukuru kwa kutuchana live 😂😂😂😂😂😂 lakini kwa saizi mji unakimbia saana kimaendeleo, kuhusu kuupamga mji, mji wa mbeya ulijengwa zamani saana kabla hata ya mipango miji kuwepo ndo maana n vigumu kuupangua lakini kwa sasa ukienda baadhi ya maeneo ambayo yanajengwa saiz kumepangwa vizuri tuu, mafano, Forest ya zaman, forest mpya, sae, isyesye, veta na kungineko, lakini pia serikali ilisha tia sign na kampun ya Urban solution ya Tanzania kwa ajili ya kuupanga upya mji wa mbeya nafikir wapo kwenye mchakato huo kwa sasa NB: viongozi mbeya wana uroho wa madaraka ko mmoja wao akishika madaraka bc wanafanya figusu ili tuu yule mwingine aferi,, huo ndo uchawi wa fikra wa viongozi wetu, miradi mingi saana wanakimbiza hapa mbeya, ukiwemo mradi wa Halmashauri wa ujenzi wa mbeya city mall,,na kuliendeleza eneo la bustani ya mkoa kujenga hotel ya kisasa na bustani ya kisasa na michezo ya watoto, lkn pia ujenzi wa Chuo kikuu tawi la udsm mpka saiz viongozi wetu hawaeleweki kama watatoa hizo ekar mia tano kwa ajili ya ujenzi huo,,, yaani hawaeleweki kbsaaa
 
Bondinear

Member
Jan 29, 2021
48
125
Sio lazima kuwa na Ardhi kubwa Lord Denning... cha msingi ni kwamba hiyo waliyopewa wataitumiaje... siku hizi madarasa hufanyika hata mitandaoni, wajenge tu magorofa sehum hiyo ya ekari 50 hata ikibidi design ya lile gorofa la Dubai, watoto watasoma tu.. hii habari ya kutaka ekari zaidi ya 100 ni uchuro mtuou wa namna yake... hivi wanakwenda kusoma au kupunga hewa? wanataka wawe na misitu halafu mabinti waendelee kutoa kinyama ugomvi ili hali Salma kikwete mwenyewe amesema hakubaliani na wajawazito kurudi shuleni ? Kauli ya Kikwete ni kukataa kiana au kinamna jinsi ya kuendeleza campus ya Mbeya kwa kisingizio hafifu.. si wakubali tu hizo 50 na waendelee kuongeza kadri ya mahitaji au shida iko wapi?
Sio tuu kinajengwa chuo, I mean madarasa ya kusomea tuu, kulingana na speech ya kikwete ni kwamba anataka ajenge, chuo kikubwa cha afyae, hopital kubwa ya mafunzo Africa, mabweni ya wanafunzi, office za chuo na hospital pamoja na nyumba za wafanyakazi za kuishi... Kwa hekal hamsin ni ndogo saaana
 
Izia maji

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
500
1,000
Kumbuka kuwa kitu kinachowekezwa ni kwa manufaaa ya jiji la mbeya, hapo inajengwa hospital ya kisasa humohumo chuon, mzunguko wa pesa utaongezeka, wawekezaji wataongezeka, harafu ni chuo cha serikali sasa nan aiuzie serikali ardhi?????... Mi nmchanaga live tulia ackson ig huko ni upuuz huo, watoe ardhi mbeya ipo waz saaana
Akili za kitoto na kindezi hizi! Kwa hiyo watu waathirike kwa manufaa ya umma! Hujawahi kusikia watu wanalipwa compensation na serikali inapochukuwa mali za watu?
 
Bondinear

Member
Jan 29, 2021
48
125
Kwani wapi nimesema wachukue ardhi ya watu mimi, mm nmetoa hoja kuwa mbeya inamaeneo mengi saaana ya wazi ya kiserikali mfano, Tanganyika pekers kule karibu na uwanja wa songwe, kuna kilimo eneo kubwa sana lile wanalima tuu mahind na ngano na wakiwa wametenga eneo dogo saana kwa ajili ya utafit ambayo ni tari, CBE wamepewa huko milimani huko iganzo na wanabomoa milima chuo kinajengwa mpka saiz so kwa nini nao wasitafutiwe maeneo ka hayo???? Sio kukimbiza watu, hata kule mbele ya ituha ambako inatarajiwa kupita Barabara ya mchepuko wajenge tuu kwan shida iko wapi
Akili za kitoto na kindezi hizi! Kwa hiyo watu waathirike kwa manufaa ya umma! Hujawahi kusikia watu wanalipwa compensation na serikali inapochukuwa mali za watu?
 
Sep 18, 2020
77
125
Akiwa jijini Mbeya Rais Mstaafu wa JMT Jakaya Mrisho Kikwete aliulaumu uongozi wa Mkoa wa Mbeya kwa kutokuwa serious kwa kutoa eneo la ekari 50 juu Kwa ajiri ya kujenga Tawi la chuo kikuu cha Dsm.

Kusema kweli asante sana Rais Mstaafu Mhe Kikwete Kwa kuwaambia ukweli watu wa Mbeya. Watu wa Mbeya wana sifa zifuatazo

1. Kujiona wana maendeleo wakati hawana lolote

2. Kujiona wanajua kila kitu wakati hakuna chochote wanachojua

Ukiwa hujafika Mbeya unaweza sema Mbeya ni jiji la kipekee sana Kwa namna watu wa Mkoa wanavyojiweka kwa wengine ila ukifika ndo utaona kumbe ni Mkoa wa hovyo kupindukia. Mbeya hawajali mipango miji, hawajui hata kujenga nyumba Nzuri za kisasa! Wanashindwa hata na Mkoa wa juzi Njombe. Mbeya imejaa uchafu sana na ujengaji wa nyumba wa hovyo kupindukia wanajifanya wana makanisa mengi kumbe wamejaa ushirikina kupindukia na hawapendi maendeleo ya wengine!

Nirudi kwenye Mada!
Tangu JK aongelee lile suala nilitegemea wabunge wa Mbeya watakuwa Wameshaitisha kikao na kujadili jinsi gani watapata ilo eneo la kuwapa Chuo kikuu cha Dsm.

Kwa wasiojua, uwepo wa Chuo kikuu kikubwa Kama UDSM sehemu, sio tu unahamasisha maendeleo, Ila unaleta chachu ya ukuaji wa kiuchumi na kifikra sehemu husika! Mikoa mingi shule na vyuo ndo vimewafanya hata waachane na Mila potofu na kujikita kwenye maendeleo

Leo hii ningekuwa Mbunge wa Mbeya, ningewakusanya wabunge wenzangu na tukaenda kwa Mkuu wa Mkoa kujadiliana nae kwa mapana sehemu gani tuitoe ili tujenge kampasi ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam
Kwa masengenyo hayo, kamwe usingeweza kuwa Mbunge jimbo lolote mkoani humo.
 
Mtoto wa Shule

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
8,557

Wasomi wao kama Prof. Mark Mwandosya alijikita kumsema Hayati Magufuli badala ya kutetea maendeleo ya mkoa wake. Mwisho wa siku anakuwa kama Prof. Maji Marefu tu!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom