Baada ya kauli ya Mzee Kikwete ningekuwa Mbunge wa Mbeya ningefanya haya

Akiwa jijini Mbeya Rais Mstaafu wa JMT Jakaya Mrisho Kikwete aliulaumu uongozi wa Mkoa wa Mbeya kwa kutokuwa serious kwa kutoa eneo la ekari 50 juu Kwa ajiri ya kujenga Tawi la chuo kikuu cha Dsm.

Kusema kweli asante sana Rais Mstaafu Mhe Kikwete Kwa kuwaambia ukweli watu wa Mbeya. Watu wa Mbeya wana sifa zifuatazo

1. Kujiona wana maendeleo wakati hawana lolote

2. Kujiona wanajua kila kitu wakati hakuna chochote wanachojua

Ukiwa hujafika Mbeya unaweza sema Mbeya ni jiji la kipekee sana Kwa namna watu wa Mkoa wanavyojiweka kwa wengine ila ukifika ndo utaona kumbe ni Mkoa wa hovyo kupindukia. Mbeya hawajali mipango miji, hawajui hata kujenga nyumba Nzuri za kisasa! Wanashindwa hata na Mkoa wa juzi Njombe. Mbeya imejaa uchafu sana na ujengaji wa nyumba wa hovyo kupindukia wanajifanya wana makanisa mengi kumbe wamejaa ushirikina kupindukia na hawapendi maendeleo ya wengine!

Nirudi kwenye Mada!
Tangu JK aongelee lile suala nilitegemea wabunge wa Mbeya watakuwa Wameshaitisha kikao na kujadili jinsi gani watapata ilo eneo la kuwapa Chuo kikuu cha Dsm.

Kwa wasiojua, uwepo wa Chuo kikuu kikubwa Kama UDSM sehemu, sio tu unahamasisha maendeleo, Ila unaleta chachu ya ukuaji wa kiuchumi na kifikra sehemu husika! Mikoa mingi shule na vyuo ndo vimewafanya hata waachane na Mila potofu na kujikita kwenye maendeleo

Leo hii ningekuwa Mbunge wa Mbeya, ningewakusanya wabunge wenzangu na tukaenda kwa Mkuu wa Mkoa kujadiliana nae kwa mapana sehemu gani tuitoe ili tujenge kampasi ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam....
......umesahau uchawi. mijitu ya mbeya michawi sana. hata ukimkuta mtu ana biashara ya mtaji wa sh laki nane, utaambiwa aliua ndugu yake au alifanya hiki au kile.
 
Chuo cha jalalani kina matumizi gani na hekta 500? ingekuwa SUA ningeelewa huenda wanahiaji ardhi kubwa kwa ajili ya mashamba darasa na maeneo ya kufanyia tafiti za kilimo, mifugo, misitu na mazingira........hapo wanataka kuhalalisha uporaji wa ardhi ya wananchi ili wajitwalie maeneo kwa maslahi yao binafsi.
Sikuiz tunaelekea kwenye nyuklia sayansi
Yanahitajika maeneo makubwa
 
Kwani lazima kijengwe mbeya? Tayari mbeya tech ipo mnaingeza chuo cha nini? Mwanza Geita Kagera yaani kanda ya ziwa hamna chuo kikuu kumejazana vyuo vy ualimu wa primary halafu mnapeleka mbeya hivi tunawaza sawasawa kweli? Au kuna Prof mstaafu anataka kugombea ubunge
Master plan yao iko huko
But wakizungua maeneo yapo nchi hii ina maeneo mengi
 
Mbeya wanajiona, wanajikweza , hawatak kutoa eneo , hawawezi kuwafikia watu wa kilimanjaro, hawependi maendeleo ya wengine naona umakaririshwa tu , Ni non sense tupu
Hapo watakuwa wajinga sababu chuo ni kwa faida ya uchumi wa mkoa wao
 
Ainisha hizo hekta 500 mnataka kuzifanyia nini, siyo kujiropokea tu kama walevi wa chimpumu.....
Heka 500 ni Chache nina mashamba zaidi ya hekari izo kwa chuo barabara majengo ni eneo la kawaida
Kutoka krampus moja had nyingine ni trip like University of dodoma nazan unaona kinavyo contribute uchumi wa watu wa Dodoma so watu wa Mbeya changamkenibmkishindwa sisi Tabora tunakitaka
 
Yeye anaongelea Mbeya Jiji wewe unasema mambo ya kulisha mikoa. Kwani huko Soweto na Mafiat mnalima
Ndio maana nikamwambia na sasa nakwambia wewe kua mlifika mbeya kwa wiki na mkasepa.

Jiji la mbeya linaanzia wapi na kuishi wapi?? Ukijua jiulize uyole ni mbeya ama si mbeya?? Sido ni mbeya ama si mbeya?? Na huko kote shughuli za kilimo zipo ama hazipo??

Au umekalili kua kilimo ni mashamba makubwa tu, hayo maeneo kuna mashine kibao za kuchakata mpunga kua mchele . Ni sawa na kusema dsm kumeendelea bila kuvitaja viwanda vilivyopo.

Mji si maghorofa tu ndgu yangu ohooo, kalagabaho.
 
Heka 500 ni Chache nina mashamba zaidi ya hekari izo kwa chuo barabara majengo ni eneo la kawaida
Kutoka krampus moja had nyingine ni trip like University of dodoma nazan unaona kinavyo contribute uchumi wa watu wa Dodoma so watu wa Mbeya changamkenibmkishindwa sisi Tabora tunakitaka
Waache waendelee kulala washamba hawa!

Kama hawajajifunza kuchangamkia fursa na kupenda kuishi vizuri watakuja kuwa wa mwisho kwa maendeleo hapa Tanzania!
 
Huo sio ukweli. Mbeya imejengwa kiholela sikatai ila hiyo ya kutojua kujenga nyumba nzuri si kweli mkuu. Nyumba nzuri zipo kibao.

Tatizo la ujenzi holela wa mbeya sio wa juzi wala jana ni toka kitambi hicho. Na ndio maana nyumba nyingi zinazoonekana pembezoni mwa barabara ni mbaya kwasababu ni za zamani. Ndio mana nasema mtu kama wewe ni wale ambao wamekaa mbeya mda mfupi sana hawaijui vyema, pembezoni mwa barabara nyumba nyingi ni za kitambo hicho ila huko ndani kuna maeneo kuna nyumba kali tu. Huu sasa ndo ukweli ishi nao.
Kwa nini wasibomoe wajenge nyumba Nzuri na za kisasa!

Acha kutetea ujinga! Watu wa Mbeya badilikeni mtaendelea kuwa nyuma kila siku kwa u shamba wenu
 
mwaka 2001 nilikodi nyumba kwa mzee Mwakalibile kwa Tshs 2500 pale mbalizi ngoja niishie hapo.
 
Ana mume na watoto? Ndiye huyu enzi zake
Mbunge mwenyewe ni wa promotion.
FB_IMG_16295418581944308.jpeg
 
Kazi ushirikina, majungu na kutopenda maendeleo ya wengine! Hawana Tofauti na watu wa Kagera

Ndo mana hawawezi wafikia watu wa Kilimanjaro hata siku moja! Kilimanjaro wao priority ni maendeleo
Mkuu we una tofauti gani na hao watu wa mbeya?
 
Mtoa mada itakua ulitoswa na binti wa kinyaki anayeishi sinde, ivyo kwa kua misele yako ilikua inaishia sinde ndio unakuja na kebehi. Mitaa ya uswahilini uwa haikosi mahali popote mzee. Wakati mwingine jifunze kuwa mstaarabu kwenye kutoa hoja zako.
 
Akiwa jijini Mbeya Rais Mstaafu wa JMT Jakaya Mrisho Kikwete aliulaumu uongozi wa Mkoa wa Mbeya kwa kutokuwa serious kwa kutoa eneo la ekari 50 juu Kwa ajiri ya kujenga Tawi la chuo kikuu cha Dsm.

Kusema kweli asante sana Rais Mstaafu Mhe Kikwete Kwa kuwaambia ukweli watu wa Mbeya. Watu wa Mbeya wana sifa zifuatazo

1. Kujiona wana maendeleo wakati hawana lolote

2. Kujiona wanajua kila kitu wakati hakuna chochote wanachojua

Ukiwa hujafika Mbeya unaweza sema Mbeya ni jiji la kipekee sana Kwa namna watu wa Mkoa wanavyojiweka kwa wengine ila ukifika ndo utaona kumbe ni Mkoa wa hovyo kupindukia. Mbeya hawajali mipango miji, hawajui hata kujenga nyumba Nzuri za kisasa! Wanashindwa hata na Mkoa wa juzi Njombe. Mbeya imejaa uchafu sana na ujengaji wa nyumba wa hovyo kupindukia wanajifanya wana makanisa mengi kumbe wamejaa ushirikina kupindukia na hawapendi maendeleo ya wengine!

Nirudi kwenye Mada!
Tangu JK aongelee lile suala nilitegemea wabunge wa Mbeya watakuwa Wameshaitisha kikao na kujadili jinsi gani watapata ilo eneo la kuwapa Chuo kikuu cha Dsm.

Kwa wasiojua, uwepo wa Chuo kikuu kikubwa Kama UDSM sehemu, sio tu unahamasisha maendeleo, Ila unaleta chachu ya ukuaji wa kiuchumi na kifikra sehemu husika! Mikoa mingi shule na vyuo ndo vimewafanya hata waachane na Mila potofu na kujikita kwenye maendeleo

Leo hii ningekuwa Mbunge wa Mbeya, ningewakusanya wabunge wenzangu na tukaenda kwa Mkuu wa Mkoa kujadiliana nae kwa mapana sehemu gani tuitoe ili tujenge kampasi ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam

Umeshahau Jambo Moja Mbeya Ndiyo Ngome Kuu Ya Upinzani
 
Mtoa mada umesahau kusema Mbeya walichokufanyia. Ninawasiwasi mtoa mada umeoa Mbeya kama hujaoa Mbeya basi kuna ndugu yako kaoa Mbeya na amebanwa haswa.

Binafsi nakupenda Mbeya kwasababu zifuatazo.
1. Mbeya kuna hali ya hewa nzuri ambayo hata mgeni kutoka ulaya lazima aipende.
2. Mbeya kuna vyakula vingi vitamu na vya kila aina na vya bei ndogo.
3. Mbeya kuna mazingira mazuri ya kusomea
4. Mbeya unakunywa maji ya kisimaMbeya unafulia maji ya kisima.
5. Mbeya ukiagiza chakula hotelini maji ya kunywa unamiminiwa kutoka kwenye majagi maalumu. Na hayo maji yanachotwa kwenye ndoo tu.

Japo naishi Dar ila huwa napenda sana ningeishi Mbeya. Dar kuna mbu sana mpaka kero nyieee, Dar unalala ndani ya chandarua. Dar maji ya kunywa ni shida, Dar maji ya kufulia ni shida, Dar maji ya kuoga ni shida.

Hii ndio imenipa akili ya kuanza mkakati wa kufungua kiwanda cha Kuchukua maji ya bahari ya Hindi na kuondoa chumvi, ili kupata maji safi na salama. Lakini pia kuna vimashine nitawauzia wakazi wa Dar es salaam waliochimba visima vyenye maji ya chumvi, vitakua vinatumia solar kutoa chumvi kwenye maji ya kisima. Sasa wakazi wataweza kupata maji ya kunywa, kufulia na kuoga majumbani mwao.
Kwa hiyo hali ya hewa na chakula bei chee ndio maendeleo?
 
Back
Top Bottom