Baada ya Kangi Lugola, nani kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani?

Baada ya mbabe kubabuliwa na kutumbuliwa hadharani tena kwa aibu kubwa, nani atavaa mikoba ya Waziri wa Mambo ya Ndani?

Tukumbe Waziri atateuliwa kwa jicho la uchaguzi mkuu, 2020. Atakuwa mtu mpya kabisa? Au mmoja wa ma naibu waziri atapandishwa cheo? Au kuna mmoja atahamishiwa hapo toka wizara nyingine? Bila shaka tutashuhudia kuapishwa kwake ndani siku chache pale Ikulu Dar es Salaam.

Kunaweza kuwa na "movement" kwenye baraza la mawaziri. Wengine kuhamishwa nk. Lakini inaweza kuwa nafasi ya Jiwe kumuondoa self confessed Mzee wa Matunguli ambayo hulennga kumroga Jiwe ili asimwondoe kwenye wizara zente ulaji mkubwa labda kupita zote.

Kikubwa kilichonifurahisha ni kwamba Jiwe ameanza kutambua kwamba watu wanaopenda kumsifia sana wana mambo wanayaficha. Wanaandaa makongamano ya vitu hewa lakini lakini ni kumsifia ili kufunika uozo wao.
Hiyo wizara inahitaji sana mtu mkomavu na anayeweza kuwa na upendo wa mzazi kwa wanawe; kati ya Mh George Mkuchika au Mh William Lukuvi mmojawapo watafaa sana; hata yule Waziri wa Sheria na Katiba atapamudu sana hapo wizarani. Akiwekwa mtu mwenye UKADA uliopitiliza sana anaweza chukulia majeshi yetu kama vikundi vya kulinda chama.
 
Imebaki miezi michache sana
J.ndalichako, Hamis kigwangala, Prof mbarawa, waziri wa uwekezaji sijui anaitwa nani, mkurugenzi Halmashauri ya nzera,mufindi,Moshi manispaa, Serengeti, nyang'wale, Tabora manispaa,igunga, Gairo, ikungi, babati mji, tanga jiji, Ras morogoro, Das geita mji, Das Moshi, DC Serengeti,iringa mjini, mbeya jiji, RC njombe, RC Kilimanjaro, RC iringa, RC Lindi, hii ni orodha ya watakao ondolewa awamu hii kwenye nafasi zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba chawene
Baada ya mbabe kubabuliwa na kutumbuliwa hadharani tena kwa aibu kubwa, nani atavaa mikoba ya Waziri wa Mambo ya Ndani?

Tukumbuke Waziri atateuliwa kwa jicho la uchaguzi mkuu, 2020. Atakuwa mtu mpya kabisa? Au mmoja wa ma naibu waziri atapandishwa cheo? Au kuna mmoja atahamishiwa hapo toka wizara nyingine? Bila shaka tutashuhudia kuapishwa kwake ndani siku chache pale Ikulu Dar es Salaam.

Kunaweza kuwa na "movement" kwenye baraza la mawaziri. Wengine kuhamishwa nk. Lakini inaweza kuwa nafasi ya Jiwe kumuondoa self confessed Mzee wa Matunguli ambayo hulennga kumroga Jiwe ili asimwondoe kwenye wizara zente ulaji mkubwa labda kupita zote.

Kikubwa kilichonifurahisha ni kwamba Jiwe ameanza kutambua kwamba watu wanaopenda kumsifia sana wana mambo wanayaficha. Wanaandaa makongamano ya vitu hewa lakini lakini ni kumsifia ili kufunika uozo wao.

Update:

Jibu limepatikana. Simbachawene ndiye waziri mpya wa mambo ya ndani na nafasi ya uwaziri ya Makamu wa Rais (Muungano na Mzingira) imechuliwa na Iddi Azan Zungu.

Jr
 
Back
Top Bottom