Baada ya JK kusaini mswada ni chombo gani ameunda cha kupokea maoni ya marekebisho ya sheria hiyo?

matongo manawa

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
336
79
Mswada umesainiwa na kuwa sheria na Mh JK,kelele za baadhi ya wanasiasa,wanaharakati,wanasheria na watu mashuhuri
kumtaka jk asiusaini zimegonga mwamba.

Ktk yaliyomo kwenye taarifa fupi ya ikulu Rais amewataka
watanzania wawe huru kutoa maoni yao kurekebisha na kuiboresha
sheria hiyo.Ninavyojua mimi Rais pamoja na busara aliyonayo lkn pia anaweza kutumia
busara ya washauri wake.
Nini kilichosababisha sasa mswada asiusaini kwanza ili kupokea maoni ya wadau na kuufanyia marekebisho
kabla haujawa sheria?
Je wananchi wanatakiwa wapeleke wapi maoni yao yakuboresha sheria hiyo?
Wayapeleke ikulu moja kwa moja?na kama maoni na sauti
za kumsihi raisi asiusaini mswada huu hazikuzaa matunda
ktk hatua ya hapa ulipofikia wananchi watasikilizwa?

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom