Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Kama mnakumbuka vizuri, Watanzania tulionekana ni kikwazo katika kasi ya kuziunganisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ilisemwa kuwa Watanzania wana hofu na ardhi yao kukwapuliwa na wageni, kwamba ajira nyingi zitakwenda kwa Wakenya au hata tulikuwa na hofu na migogoro ya kikabila ya Rwanda. Mtanzania alikuwa akiwaza kuongozwa na Kagame au Museveni, nafsi yake ilikuwa inajaa hofu.
Janga la Korona limetengeneza uhalisia mpya katika fikra za Watanzania. Tunashuhudia Rwanda, Kenya na Uganda wakilikabili janga hili kwa ufanisi zaidi yetu pamoja na kwamba hapo mwanzo walipata changamoto za hapa na pale.
Ninachoona ni kuwa baada ya janga hili kuisha, vuguvugu kali la kisiasa nchini litawalazimisha CCM kukimbilia kuharakisha na kufufua mipango ya East African Federation na hiyo ndiyo inaweza kuwa pona yao, at least kwa muda.
Tegemea kuona mazungumzo ya kisiasa yakianza kutawaliwa na habari za East African Federation na habari za siasa za ndani kupewa nafasi ndogo. Hii inaweza kuwapunguzia ari kwa kiasi fulani vyama vya upinzani ila wakicheza karata zao vizuri bado watakuwa na nafasi nzuri ya kuendelea kuwa na impact.
Viongozi makini huwa wanatumia majanga na adui wa nje (adui wa kweli au wa kutunga) kurudisha imani ya watu kwao ambayo ilikiwa imeanza kupotea. Ni mbinu ambayo wabobezi wa mambo ya kiinteligensia wanaijua vizuri sana. Yoweri Museveni naona anafanya hivyo hadi amemfunika kabisa Bobby Wine. Bill Clinton alijaribu kufanya hivyo wakati wa skendo ya Monica Lewinsky alipoenda kumshambulia Osama bin Laden kule Sudan.
Rais Magufuli alikuwa na nafasi nzuri sana ya kulitumia hili janga kwa faida za kisiasa ila ndiyo hivyo tena, wote tunaona kinachotokea.
Tutegemee baada ya janga hili, hatua za fast track kwenda kwenye East African Federation.